Zijue Sababu 7 Zinazopelekea Mwanaume Kushindwa Kutungisha Mimba.

Kama ilivyo kawaida kwenye jamii zetu watu wengi wamekuwa wakidhani kuwa mwanamke pekee ndiye mwenye wajibu wa kuhakikisha anapata mimba na ikitokea akakaa muda mrefu kwenye ndoa bila hilo kutokea, basi jamii inamtupia lawama wakiamini tatizo ni lake na siyo mumewe. Lakini kiukweli tatizo linaweza kuwa kwa mwanaume au mwanamke au wote wawili (mwanamke na mwanaume).

Tatizo la mwanaume kushindwa kutungisha mimba hujulikana kama ugumba. Tatizo hili pia hujlikana kwa kitalaamu kama infertility. Ugumba kwa wanaume hutokana na tatizo katika mbegu za kiume, manii kuwa kidogo, manii kushindwa kutembea, manii kuwa na umbo lisilo la kawaida au kuziba kwa mirija ya mbegu za kiume.

Soma pia hii makala: Fahamu Kiwango Sahihi Cha Mbegu Za Kiume Kutungisha Mimba.

Leo katika mada yetu ya blogu hii tutazungumzia sababu zinazochangia mwanaume kushindwa kutungisha mimba. Ungana nami katika kuchambua sababu hizi.

Sababu Za Mwanaume Kushindwa Kutungisha Mimba:

Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazoweza kuchangia mwanaume kushindwa kutungisha mimba ambazo ni pamoja na;

1) Uvutaji Wa Sigara Na Matumizi Ya Pombe Kupita Kiasi.

Baadhi ya mitindo ya kimaisha (lifestyle) kwa wanaume kama vile uvutaji wa sigara, bangi, matumizi ya madawa ya kulevya, matumizi ya pombe kupita kiasi yanaweza kuchangia ugumba kwa mwanaume kwani husababisha hitilafu katika uzalishwaji wa mbegu za kiume. Lakini pia kukaa masaa mengi au kila mara sehemu zenye joto sana hasa joto la kutengenezwa (saunas and hot tubs) kunaweza kuchangia ugumba kwa mwanaume na hivyo kushindwa kutungisha mimba.

pombe na sigara
Whiskey and cigarette

2) Mazingira.

Baadhi ya mazingira anayoishi mwanaume yanaweza kumpelekea kupoteza uwezo wa kutungisha mimba. Japokuwa ni kwa asilimia chache lakini kama mwanaume anajihusisha na umwagiliaji wa dawa za kuulia wadudu mashambani zijulikanazo kwa kitaalamu kama Dichlorodiphenyltrichloroethane (DDT) kwa kipindi kirefu kunaweza kuchangia mwanaume kupoteza uwezo wa kutungisha mimba.

Lakini pia kama mwanaume anafanya kazi kwenye ofisi au kiwanda ambako mionzi (radiations) ni vitu anavyotakiwa akutane navyo kila siku basi hali hii inaweza kumuandalia ugumba polepole na hatimaye akaishiwa kabisa uwezo wa kutungisha mimba.

DDT bottle
DDT bottle insect spray

3) Madhara Ya Saratani Ya Matibabu Yake.

Madhara yatokanayo na ugonjwa wa saratani pamoja na matibabu yake hasa matibabu yanayohusisha mionzi (radiotherapy or chemotherapy) vinaweza kuwa ndiyo sababu ya ugumba kwa mwanaume. Matibabu hayo ya saratani yanaweza kuharibu uzalishaji wa mbegu za kiume zenye afya na hivyo kumpelekea mwanaume kupoteza uwezo wa kutungisha mimba.

Soma pia hii makala: Mambo 9 Muhimu Usiyo yajua Kuhusu Saratani.

4) Magonjwa Ya Zinaa (Sexually Transmitted Infections).

Magonjwa ya zinaa kama vile kaswende, kisonono, pangusa yanaweza kupelekea mwanaume kupoteza uwezo wa kutungisha kwani magonjwa haya huchangia kuziba kwa mirija ya mbegu za kiume.

pangusa

Soma pia hizi makala:

5) Magonjwa Ya Muda Mrefu (Chronic Diseases).

Magonjwa ya muda mrefu kama vile kisukari, shinikizo la juu la damu yanaweza kupelekea uzalishwaji wa mbegu za kiume za kiume usio wa kawaida. Pia hata uwepo wa uvimbe kwenye korodani kunaweza kuathiri uzalishwaji wa mbegu za kiume na hatimaye kumpelekea mwanaume kupoteza uwezo wa kutungisha mimba.

Soma pia hizi makala:

6) Matatizo Katika Kusafiri Kwa Mbegu Za Kiume.

Kuna nyakati wanaume anaweza kuwa anatoa mbegu za kiume lakini mbegu hizo zikawa aidha hazifiki sehemu husika kwenye viungo vya uzazi wa mwanamke au zinafika sehemu hizo kwa kuchelewa na hivyo kupelekea mbegu za kiume nyingi kufia njiani.

Tatizo hili la mbegu za kiume kutokufika haraka sehemu husika kwenye viungo vya uzazi wa mwanamke linaweza kusababishwa na tatizo la mwanaume kuwahi kufika kileleni anaposhiriki tendo la ndoa (yaani ndani ya sekunde, dakika 1 au 2 tayari ameshafika kileleni). Mwanaume mwenye changamoto ya kuwahi  kufika kileleni anaweza kushindwa kutungisha mimba.

Tatizo la mwanaume kuwahi kufika kileleni linaweza kusabishwa na upigaji wa kunyeto kupita kiasi, kuangalia video za ngono kupita kiasi, kukaa muda mrefu bila kushiriki tendo la ndoa n.k.

mbegu za kkume

Soma pia hizi makala:

7) Mvurugiko Wa Homoni.

Kama ilivyo kwa mwanamke, mwanaume pia anaweza kupata tatizo la mvurugiko wa homoni ya uzazi ijulikanayo kama testosterone na hivyo kushindwa kuungisha mimba. Dalili za mvuugiko wa homoni kwa mwanaume ni pamoja na; mwanaume kuota matiti (gynecomastia), mwanaume kushindwa kusimamisha uume (erectile dysfunction), kuwa na hasira kupita kiasi bila sababu, msongo wa mawazo.

gynecomastia

Kumbuka:

Mwanaume kushindwa kumpa mimba mwanamke pia kunaweza kukasababishwa na matatizo ya kuzaliwa nayo kama vile korodani kushindwa kushuka kwenda kwenye mapumbu (scrotum) kabla ya kuzaliwa, hali ijulikanayo kwa kitaalamu kama Undescended testes (cryptorchidism).

undescended testes

Tatizo lingine linaloweza kusabisha mwanaume kushindwa kutungisha mimba ni la kimaumbile ambapo kwenye mrija wa kutolea mbegu, pamoja na mkojo uitwao urethra huota sehemu ya chini ya uume, hivyo kusababisha mbegu kutoweza kufika sehemu ya ndani ya uke, tatizo hili kitaalamu huitwa Hypospadias.

hypospadias

Tiba Ya Mwanaume Kushindwa Kutungisha Mimba:

Tatizo la mwanaume kushindwa kutungisha mimba linaweza kutibika au kushindikana kutibika kutokana na sababu iliyopelekea tatizo hilo. Tiba inaweza kuwa kubadilisha mfumo wa kuishi kutokana na maelekezo ya daktari, dawa za kutumia na lishe au upasuaji (kutegemeana na upatikanaji wa vifaa tiba na wataalamu).

HITIMISHO:

Kwa msaada wa ushauri, vipimo na tiba ya magonjwa ya afya ya uzazi kwa wanaume na wanawake wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487.

vipimo vya mfumo wa uzazi