Kiwango cha kawaida cha mbegu za kiume kinatakiwa kuwa milioni 15 mpaka milioni 200 kwa milliliter ya shahawa Kiwango chochote chini ya milioni 15 kinatambulika kwamba ni pungufu na ni ngumu kumpa mwanamke mimba.
Ili kufahamu uwezo na wingi wa mbegu zako za kiume ni muhimu uende hospitali au mabaara ya karibu kisha utapiga punyeto na kuweka mbegu kwenye kifaa, na muhudumu atafanya vipimo na kutoa ripoti yako.
Jinsi Ya Kutafsiri Uwezo Wa Mbegu Za Kiume:
Kipimo cha mbegu za kiume (semen analysis) kinapima mambo yafuatayo;
a) kiwango cha mbegu zako
b) shepu ya mbegu na
c) uwezo wa mbegu kuogoelea (sperm motility)
Kumbuka: Baada ya vipimo zungumza na daktari akupe ufafanuzi wa kina kuhusu uwezo wa mbegu zako za kiume kulingana na ripoti ya vipimo.
Umuhimu Wa Kiwango Sahihi Cha Mbegu Za Kiume:
Unapoongelea swala la kumpa mwanamke mimba, uwezo wa mbegu zako za kiume kama mwanaume ni jambo la muhimu sana. Pamoja na kwamba inahitajika mbegu moja tu kurutubisha yai, mbegu nyingi za kiume zinapokuwa na afya njema basi chansi ya mwanamke kushika mimba inaongezeka zaidi.
Hata kama bado huna mpango wa kumpa mwanamke mimba, uwezo na ubora wa mbegu zako ni kipimo cha utimamu wa afya yako pia. Utafiti mmoja uligundua kwamba wanaume wenye mbegu kidogo wana uwezekano mkubwa wa kuwa na mafuta mengi mwilini na presha kubwa ya damu ukilinganisha na wanaume wenye mbegu nyingi.
Kwa kutazama sababu hapo juu, kama daktari atagundua una mbegu kidogo, itakuwa ni muhimu sana daktari apime pia kiwango cha homoni ya testosterone, afatilie mtindo wa maisha na afya yako kwa ujumla kujua chanzo cha tatizo lako.
Jinsi Kiwango Cha Mbegu Za Kiume Kinavoathiri Uwezo Wa Kutungisha Mimba:
Chansi ya kumpa mwanamke mimba inapungua kadiri idadi ya mbegu inavopungua. Hii ni sababu mojawapo kubwa kwanini wanawake wengi hawashiki mimba.Sababu zingine kwa upande wa mwanamke ni pamoja na
a) idadi ndogo ya mayai kwa mwanamke.
b) Kuziba kwa mirija ya uzazi.
c) Kupanuka kwa kizazi.
Kushindwa kushika mimba pia yaweza kusababishwa na wapenzi kutokutana mara kwa mara. Ni kawaida kwa wapenzi wenye afya nzuri kabisa kuchukua mpaka miezi sita ama mwaka kushika mimba, hilo ni kawaida.
Kama una umri zaidi ya miaka 35 na mumekuwa mkitafuta mimba bila mafanikio zaidi ya mwaka mmoja muhimu muende hospitali mkafanyiwe vipimo kwa wote wawili.
Visababishi Vya Upungufu Wa Mbegu Za Kiume:
Vifuatavyo ni visababishi vya upungufu wa mbegu za kiume ambavyo ni;
1. Magonjwa ya uzazi na upasuaji kwenye viungo vya uzazi.
Ajali ama ugonjwa unaopelekea ufanyiwe upasuaji ni kihatarishi cha kupungua kwa uzazlishaji wa mbegu za kiume. Baada ya upasuaji mirija midogo kwenye korodani yaweza kuathiriwa na hivo mbegu zikazalishwa kidogo.
2.Tiba ya saratani.
Tiba hizi ikiwemo mionzi na chemotherapy huathiri mbegu za kiume ambapo mionzi huua mbegu za kiume moja kwa moja.
3.Kuvimba kwa mirija midogo ya damu kwenye korodani.
Kitaalamu tatizo huitwa varicocele. Mirija hii inapovimba inapunguza mzunguko wa damu kuelekea kwenye tishu za kuzalisha mbegu za kiume.
4. Maambukizi ya magonjwa ya zinaa.
Endapo mgonjwa hakupata tiba vizuri ama aliyechelewa kupata tiba ya magonjwa ya zinaa kama vile kisonono, pangusa inaweza kupelekea kuziba kwa mirija ya damu kwenye via vya uzazi.
5. Mazingira.
Hali ya joto sana inaathiri na kuua mbegu. Hii ndiomaana wakati wa joto utaona mapumbu yakininginia nje kuepka joto kali la mwili. Hivo vitu chochote chenye joto sana siyo salaa kuwekwa karibu na viungo vya uzazi, mfano kompyuta mpakato, simu nk.
Mazingira mengine hatarishiri ni eneo lenye mionzi hasa kwenye viwanda.
6. Mtindo wa maisha.
Aina fulani ya maisha ina mchango mkubwa kwenye ubora na wingi wa mbegu zako. Matumizi ya pombe, sigara na madawa ya kulevya hupunguza uzalishaji wa mbegu. Kufanya kazi masaa mengi ukiwa umekaa, uzito mkubwa, msongo wa mawazo pia hupelekea kupungua uzalishaji wa mbegu za kiume.
Vipi kuhusu kupiga punyeto, je inapunguza mbegu?
Tafiti zinasema kwamba hata kama ukimwaga mbegu kila siku aidha kwa kupiga punyeto ama kukutana na mwanamke bado mbegu zitawepo za kutosha. Madhara ya punyeto ni kushindwa kumridhisha mwanamke na kwa kushindwa kurudia tendo na pia kuwahi kufika kileleni.
Tiba ya Kuongeza Mbegu za Kiume:
Habari njema ni kwamba tiba inapatikana hospitali na kwenye tiba asili pia, ili kuboresha idadi na uwezo wa mbegu zako. Kwa kulingana na chanzo cha tatizo, daktari anaweza kupendekeza tiba zifuatazo;
a) Kufanyiwa upasuaji.
Hii hufanyika endapo kama mishipa midogo ya damu kwenye korodani imevimba (varicocele).
b) Antibiotics.
Dawa hizi hutolewa endapo Kama kuna maambukizi ya bakteria yanyosababisha mbegu za kiume kufa.
C) Dawa Za Kuchochea Uzalishaji Wa Mbegu Za Kiume.
Dawa za kuchochea uzalishaji wa mbegu za kiume hutolewa pamoja na ushauri ikiwa una tatizo la kuwahi kumwaga na kutosimamisha uume.
Ushauri wa Kufuata ili Kuboresha Mbegu za kiume:
Yafuatayo ni baadhi ya mambo muhimu ambayo mwanaume anapaswa kuzingatia ili kuboresha mbegu zake za kiume;
a) Punguza uzito na kitambi.
uzito mkubwa na kitambi yaweza kusababisha kupungua kwa uzalishaji wa mbegu za kiume. Rekebisha mtindo wa maisha ili upunguze uzito kuwa kawaida.
b) Tumia vyakula vyenye madini ya zinki kwa wingi.
Ulaji wa vyakula vyenye madini ya zinki kwa wingi husaidia katika kuongeza mbegu za kiume.Unashauriwa kutumia vyakula hivi katika mlo wako wa kila siku ili kuepukana na changamoto ya kuwa na kiwango kidogo cha mbegu za kiume.Mfano wa vyakula vyenye madini ya zinki kwa wingi ni pamoja na mbegu za maboga.
c) Punguza matumizi ya pombe na sigara.
Uvutaji wa sigara na matumizi ya pombe yaliyokithiri ni moja wapo ya sababu ya kupungua kwa uzalishaji wa mbegu za kiume, hivyo unashauriwa kuepukana na matumizi ya sigara na pombe yaliyokithiri ikiwa ni sehemu ya kusaidia katika uzalishaji wa mbegu za kiume zenye afya bora.
d) Vaa boksa za cotton.
Boksa zilizotengenezwa kwa material ya pamba (cotton) zinakinga pumbu dhidi ya joto kali ambalo huua mbegu za kiume.Pia unashauriwa kuepuka kuvaa boksa zinazobana sana.
Soma pia hii makala: Fahamu aina 7 za vyakula vinavyo ongeza kiwango cha mbegu za kiume.
HITIMISHO:
Ikiwa una changamoto ya kuwa na kiwango kidogo cha mbegu za kiume unashauriwa kutumia virutubisho vilivyotokana na mimea na matunda vyenye madini ya zinki kwa wingi, virutubisho hivi vitakusaidia kuongeza kiwango cha mbegu za kiume kwa haraka. Thamani ya virutubisho hivi mara zote ni TZS 120,000/= full dose lakini sasa hivi unavipata kwa gharama ya TZS 90,000/= full dose (okoa 30,000/= nzima), dozi ya mwezi mmoja na wiki mbili. Ili kupata virutubisho hivyo bonyeza hapa chini.
Kwa msaada wa ushauri, vipimo na tiba ya magonjwa ya afya ya uzazi wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487
Good work Mzee✌️
Karibu sana mkuu