Sababu Za Mwanaume Kukosa Hamu Ya Tendo La Ndoa.

Kukosa Hamu Ya Tendo La Ndoa Kwa Wanaume:

Kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa mwanaume, hali ijulikanayo kwa kitaalamu kama low libido inaweza kusababishwa na mambo mengi, kuanzia sababu za kihisia hadi za kimwili.

tendo la ndoa

Baadhi ya sababu zinazochangia mwanaume kukosa hamu ya tendo la ndoa ni pamoja na:

1) Matatizo Ya Kiafya.

Matatizo ya kiafya kama vile ugonjwa wa kisukari, shinikizo la juu la damu, magonjwa ya moyo, au unene kupita kiasi yanaweza kusababisha upungufu wa hamu ya ngono.

2) Matumizi Ya Dawa.

Baadhi ya dawa, kama vile dawa za kutibu shinikizo la juu la damu (antihypertensive drugs), dawa za kutibu mfadhaiko (antidepressants), dawa za kulevya, zinaweza kusababisha upungufu wa hamu ya ngono kwa mwanaume kama mojawapo ya athari tarajiwa (side effects) zake.

3) Matatizo Ya Kisaikolojia.

Matatizo ya kisaikolojia kama vile msongo wa mawazo, wasiwasi ambayo hayajatatuliwa yanaweza kuathiri hamu ya tendo la ndoa kwa mwanaume.

msongo wa mawazo

4) Matatizo Ya Mahusiano.

Migogoro katika mahusiano, mawasiliano duni na mwenzi wako yanaweza kusababisha upungufu wa hamu ya ngono.

migogoro katika mahusiano

5) Kupungua Kwa Kiwango Cha Testosterone.

Kupungua kwa kiwango cha homoni ya testosterone mwilini kunaweza kusababisha upungufu wa hamu ya ngono kwa mwanaume. Testosterone ni homoni ya kiume inayozalishwa kwenye korodani ambayo ina jukumu muhimu katika kudumisha hamu ya tendo la ndoa kwa mwanaume.

low testosterone level

6) Mtindo Wa Maisha.

Unywaji wa pombe kupita kiasi, uvutaji sigara, matumizi ya dawa za kulevya, mlo mbaya au lishe duni vinaweza kusababisha upungufu wa hamu ya ngono kwa mwanaume.

pombe na sigara

7) Umri.

Kwa wanaume wengine, kupungua kwa hamu ya ngono inaweza kuwa sehemu ya mchakato wa kawaida wa kuzeeka.

kuzeeka

8) Uchovu Wa Kiakili Au Kimwili.

Kuchoka kimwili au kiakili, iwe ni kwa sababu ya kazi ngumu au kutokana na usingizi mdogo, inaweza kusababisha kupungua kwa hamu ya tendo kwa mwanaume.

HITIMISHO:

Ikiwa mwanaume unasumbuliwa na tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa muda mrefu kiasi ambacho tatizo hilo linaathiri mahusiano yako, ni muhimu kushauriana na daktari ili kufanya uchunguzi wa kiafya na kisaikolojia ili kutambua sababu na kupata matibabu yanayofaa.

By the way, hivi unajua kwamba dawa ya asili iitwayo PANACEA iliyotengenezwa kutokana na mimea na matunda itakusaidia mwanaume kutatua changamoto ya kukosa hamu ya tendo la ndoa?

Ndiyo ni kweli, kupata dawa hiyo wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487.

panacea