Mambo 9 Muhimu Usiyo yajua Kuhusu Saratani.

Saratani Ni Nini?

Saratani ni uvimbe unaojitokeza mahali popote katika mwili wa binadamu kutokana na seli za mwili kuanza kujigawa yaani kukua bila utaratibu na bila mwisho. Saratani hujulikana kwa kitaalamu kama Cancer.

Kwa kawaida miili yetu ina chembechembe hai nyingi ambazo huzaliana, hukua, na kufa kwa mpangalio maalumu. Chembechembe hizi zinapobadilika na kuanza kuzaliana na kukua katika utaratibu ambao sio wa kawaida ndio zinasababisha saratani.

Chembe chembe za saratani hufuata mfumo huo usio wa kawaida – zinazaliana haraka zaidi bila mpangilio na kukua kwa haraka zaidi na wakati mwingine kuwa na umbile kubwa zaidi.
Chembechembe hizi za saratani zisipodhibitiwa/zisipotibiwa mapema  zina uwezo wa kusambaa na kuota sehemu nyingine ya mwili wa mhusika.

Kumbuka:

Aina Za Saratani:

Saratani zipo za aina nyingi sana na majina yake hutegemea kiungo kilichougua na aina ya chembechembe hai zilizoshambuliwa. Kiungo chochote kinaweza kushambuliwa mfano:

1) Shingo ya mfuko wa kizazi

2)  Matiti

3) Ngozi

4) Koo na njia ya chakula, tumbo, utumbo, kongosho, ini

5) Kibofu cha mkojo na tezi dume

6) Mapafu, ubongo, macho, mifupa, misuli

7) Matezi hasa kwa watoto

8) Damu nk.

Soma pia hizi makala:

Nini Kinasababisha Saratani?

Hakuna sababu moja pekee ambayo husababisa saratani, bali ni mchanganyiko wa vitu vingi vinavyotuzunguka ikiwemo viumbe hai, kemikali, na aina ya maisha tunayoishi kila siku. Saratani tofauti zina vyanzo vyake tofauti.

Mambo yanayochangia kupata saratani:

Yafuatayo ni mambo yanayomuweka mtu katika hatari ya kupata saratani ambayo ni pamoja na:

  1. Jinsia
  2. Umri
  3. Kurithi
  4. Matumizi ya kemikali  au Mionzi
  5. Uvutaji wa sigara
  6. Maambukizi ya baadhi ya vimelea: Virusi, bakteria, fangasi
  7. Matumizi Makubwa ya  pombe
  8. Matumizi ya kemikali na mionzi
  9. Ulaji mbovu: Mafuta mengi, nyama nyekundu kwa wingi  n.k
  10.  Kutofanya mazoezi
  11.  Unene uliokithiri
  12.  Madawa, sumu ya kuulia wadudu
  13.  Wasichana kuanza ngono katika umri mdogo

Dalili Za Saratani:

Zifuatazo ni baadhi ya dalili za awali za saratani ambazo ni pamoja na:

1) Kila Saratani huwa na dalili zake kutokana na ilipoanzia

2) Mara nyingi saratani haina maumivu mwanzoni na ni ngumu kugundua hasa kamma iko kwa ndani

3) Uvimbe sehemu yoyote ya mwili

4) Mafindofindo

5) Mabadiliko ya haja kubwa au ndogo

6) Kidonda ambacho hakiponi

7) Damu kutoka bila mpangilio au uchafu usio wa kawaida kutoka sehemu za siri (uke)

8) Shida ya kumeza au kupumua

9) Sauti inayokwama kwama

10) Kuvimba mdomo kwa watoto

11) Kuvimba tumbo kwa watoto

Uhakiki Wa Saratani:

Saratani inahakikiwa kwa njia ya kutoa kinyama (biopsy) au ute wa chembechembe husika na kupimwa katika maabara maalum (PATHOLOGY LABORATORY).

Vipimo vingi vya maabara au Radiologia vinaonyesha tu mabadiliko yenye kuashiria uwezekano na siyo uhakiki.

Tiba Ya Saratani Kwa Ujumla:

Tiba za kitaalamu zilizohakikishwa ni pamoja na:

1) Upasuaji

2) Dawa za mshipa/dripu, vidonge

3) Mionzi (Radiotherapy)

4) Tiba ya vichochezi (Hormonal Replacement Therapy)

5) Tiba hizi hutumika kwa mchanganyiko kwa kutegemea aina ya saratani, hatua ya ugonjwa na hali ya kiafya ya mgonjwa

6) Tiba mpya: Targeted & Gene therapy

Madhara Ya Saratani:

Yafuatayo ni madhara yanayoweza kutokea endapo mgonjwa mwenye saratani atashindwa kupata tiba mapema ambayo ni pamoja na:

1) Mgonjwa asipotibiwa mapema saratani huwa kubwa zaidi, na kufanya kidonda

2) Maumivu makali

3) Kusambaa katika viungo vingine vya mwili hasa:

  • Mapafu – Kukohoa na Maumivu
  • Maini – Kujaa tumbo, macho kuwa ya njano na maumivu
  • Mifupa – Maumivu / Kuvunjika ovyo
  • Kupoteza kiungo/Viungo vya mwili

Jinsi Ya Kujikinga Na Saratani:

Ili kujikinga na saratani mtu anashauriwa kufanya mambo yafuatayo:

1) Epuka Viashiria hatarishi  vinavyozuilika (66% ya saratani zinazuilika)

2) Jiepushe na uvutaji wa sigara

3) Epuka unene uliopitiliza

4) Fanya mazoezi mara kwa mara

5) Ulaji bora: Epuka matumizi ya mafuta mengi na nyama nyekundu kwa wingi, tumia matunda na mbogamboga kwa wingi

6) Epuka matumizi ya pombe kwa wingi

7) Jikinge na mionzi ya jua, hasa  watu wenye ualbino

8) Jenga mazoea ya kupima afya mara kwa mara

9) Chanjo kwa saratani zenye chanjo mfano, chanjo ya homa ya ini (HBV) na mlango wa kizazi (HPV)

HITIMISHO:

Kwa ushauri, vipimo na tiba ya magonjwa ya afya ya uzazi wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487.

vipimo vy afya ya uzazi