Mambo 5 Muhimu Usiyo yajua Kuhusu Punyeto Kwa Wanaume.

Maana Ya Punyeto:

Punyeto ni kitendo cha mwanaume kutumia kiganja chake kujichua uume wake mpaka kutoa manii kwa lengo la kujistarehesha.

Mara nyingi wanaofanya kitendo hiki, hufanya kwa sababu mbalimbali lakini sababu kuu ni athari za kisaikolojia na kutokujiamini.

Kundi la vijana mabarobaro ni wahanga wakubwa katika ufanyaji wa punyeto hasa walio shule za bweni (seminary) au vyuoni na pia wanamitindo wa kiume.

Baadhi yao hata wakija kuoa huwa hawaachi kujichua na huona starehe zaidi kuliko kukutana na mkewe.

Sababu Zinazowafanya Wanaume Kupiga Punyeto:

Zipo sababu nyingi Zinazochangia wanaume kupiga punyeto baadhi ya sababu hizo ni pamoja na;

1) Kupunguza Mawazo.

Kupiga punyeto kunapelekea utoaji wa homoni mbili muhimu kwenye ubongo ambazo ni, dopamine na oxytocin.

 Dopamine hii ni kemikali inayotolewa kwenye ubongo ambayo hujiusisha na mambo kama vile furaha (pleasure), zawadi (reward).

 Oxytocin hii ni homoni ambayo hujulikana pia kama homoni ya upendo (love hormone) kwa sababu inahamasisha hisia za huruma (empathy), kuungana (bonding) na ukarimu (generosity). 

Hivyo basi kwa pamoja hizi homoni husaidia mwili kurelax na kupunguza mawazo. Hii inabaki kuwa sababu ya wanaume waliowengi kupiga punyeto.

2) Kuepuka Ndoto Nyevu.

Ikiwa mwanaume hata piga punyeto kwa muda mrefu anaishia kupata ndoto nyevu (kuota anafanya mapenzi) jambo ambalo hupelekea kujimwagia manii kwenye nguo ya ndani (boksa) ambayo huitaji kubadilishwa/kufuliwa kila asubuhi. kero ya kupata ndoto nyevu inabaki pia kuwa mojawapo ya sababu inayowafanya wanaume walio wengi kupiga punyeto.

3) Hamu Ya Juu Ya Ngono.

Wanaume wenye hamu ya juu ya ngono (high libido) hujukuta wakipiga punyeto mara kwa mara ili kukidhi haja zao. Kitendo hiki huwapelekea wanaume hao kuwa na uraibu (addiction) wa punyeto hali ambayo huwapelekea ugumu kwenye kuacha.

4) kulala Usingizi.

Kama tulivyojadili kwenye point namba1 kwamba kupiga punyeto kunahamasisha utoaji wa homoni mbili kwenye ubongo, dopamine na oxytocin, hizi homoni pia huandaa mazingira ya mwili kupata usingizi. Hivyo wanaume walio wengi hupiga punyeto ili wapate usingizi kwa urahisi.

5) Kutokujiamini mbele ya wanawake.

Wanaume wasio jiamini mbele ya wanawake (domo zege) hasa linapokuja suala la kutongoza hujikuta wakiingia katika tabia hii ya kupiga punyeto kama njia ya kujiridhisha kingono kwani wanaume haoi huwa na uoga wa kukataliwa na wanawake.

6) Athari za kisaikolojia.

Wanaume ambao hukataliwa na kudharauriwa na wanawake mara kwa mara hasa linapokuja suala la kutongoza wengi wao hupunguza kujiamini na kujiona si kitu mbele ya wanawake. Jambo hill hupelekea wanaume hao kujiingiza katika tabia ya kupiga punyeto kama njia ya kujiridhisha kingono.

Faida Za Punyeto:

Zifuatazo ni faida za kupiga punyeto ambazo ni pamoja na;

1) punyeto inapunguza mawazo (stress).

2) punyeto inasaidia kupata usingizi nzuri (sleep better).

-Inaboresha hali ya usingizi kwa haraka zaidi baada ya kupiga punyeto,

3) Inapunguza gharama.

4) Punyeto ni salama kuliko aina nyingine yoyote ya ngono. Huwezi kubebesha Mimba Isiyotarajiwa au kupata maambukizi yoyote ya zinaa kutokana na Kupiga nyeto.

5) Husaidia kuweka mfumo wa kinga yako vizuri.

-Watu walio imara katika punyeto kuchukua siku nyingi kuwa wagonjwa.

6) Inaongeza hamu ya kufanya mapenzi zaidi/ boosts libido.

7) Punyeto husaidia kuweka estrogen yako na kiwango cha Testosterone katika uwiano sahihi.

Mambo Ya Kuepuka Ufanyapo Punyeto.

Yafuatayo ni mambo ya Kuepuka pindi ufanyapo punyeto ambayo ni pamoja na;

1) Unapaswa kuepuka kubana uume Wako wakati ukitoa manii ili kuepusha Kuzuia mtiririko wa shahawa.

 Vinginevyo hii inaweza kuharibu mishipa Nevu na mishipa ya damu kwenye uume, na pia italazimisha shahawa Kuingia kwenye kibofu cha mkojo.

2) Ikiwa unapiga punyeto katika nafasi ya uso-chini (face-down position) Unaweza kutumia Pressure zaidi kwenye uume, na unaweza kuiumiza. Ili kuepuka hili unashauriwa Kulala au kupiga nyeto ukiwa umesimama, umekaa, au umelala chali.

Madhara Ya Punyeto:

Yafuatayo ni madhara yatokanayo na punyeto ambayo ni pamoja na;

1. Mwili Kuwa Dhaifu.

Hii kutokana na mwili kupoteza protein na calcium ambayo ni muhimu kwa afya ya mifupa, hivyo hupelekea mifupa muda mwingi kuwa inamuuna na kuwaka moto. Na hata mfupa ulioko katika makalio nao huwa umelika kwa sababu ya punyeto hivyo muhusika hawezi kaa kwa kikazi kimoja kwa muda mrefu utamuona mara kakaa hivi mara vile nk.

Pia mifupa ya miguu nayo humuuma sana pamoja na ya nyayo. Vile vile mgongo na kiuno humsumbua sana.

2. Kuathiri Mfumo Wa Fahamu.

Hapa mpaka mke wake akijipara na kujikwatua yeye mwanaume hashtuki wala hapandwi na mzuka kwani mishipa ya fahamu ilisha athiriwa na hiyo punyeto. 

Hali hii mpaka sasa imo kwa baadhi ya wanaume katika jamii na inatesa wanandoa wengi kwasababu tatizo la punyeto walikuwa wakiifanya kabla hawajawa na wake zao. 

3. Upungufu Wa Nguvu Za Kiume.

Kutokana na kitendo cha kujichua kuathiri misuli na mishipa ya damu ya uume.Tatizo la kuishiwa nguvu za kiume wengi limetokana na kupiga punyeto, yawezekana walipokuwa mashuleni, au baada ya kutoka mashuleni au kutokana na kuangalia picha za ngono kupitia video, simu, nk. 

Wanaume wengi waliopitia mitindo ama mazoea ya punyeto wamekuwa wakipatwa na tatizo la kumuingia mwanamke na kujikuta wanafika kileleni dakika moja mara tu anapoingiza uume wake kwa mwanamke, na kujikuta anamwacha mwanamke njia panda. Hali hii humfanya mwanaume kushindwa kurudia tena awamu ya pili na kujikuta anapatwa na usingizi.

 Hivyo, heshima hutoweka kwani mwanamke hubaki na mawazo na manunguniko pia akihisi kama vile anaonewa na mumewe.

Soma pia hii makala: Zijue Dalili 7 Za Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Tiba Zake.

4. Kuwa Mtumwa (Teja) Wa Punyeto.

Kwa mtu aliyezoea kufanya punyeto kwake inakuwa kama kilevi (addiction) kwake, baadhi yao hawapati usingizi usiku mpaka apige nyeto au asubuhi akiamka akiwa bafuni lazima apige nyeto ndio kwake ujihisi yuko sawasawa. Au akiwa ofisini anajifungia anapiga nyeto.

Wengine hali hii huwa kubwa kwao hata wakiwa wameshaoa hisia za kufanya tendo la ndoa na mkewe huwa mbali, mpaka afanye punyeto

5. Kuwa Na Usingizi Mzito.

 Baadhi ya wanaume walio athirika na punyeto wanakuwa na hali ya kulala lala sana na upumuaji wa shida wakiwa usingizini na hali hii huwatokea zaidi mara akimaliza kutoa manii wakati wa kujichua.

7. Madhara Ya Kisaikolojia.

Kuwa na sonona (depression)  na kujihisi vibaya baada ya kumwaga manii na kukosa hali ya kujiamini

9. Kuwahi Kutoa Manii (Pre mature ejaculation).

Madhara mengine wanayoyapata ni kuwahi kumaliza wanapofanya tendo la ndoa na wake zao. Hali kama nilivyoelezea mwanzo kuwa wanaume waliokuwa na tabia ya kupiga punyeto, wanapokutana na wake zao ama wapenzi wao, huwahi kufika kileleni ndani ya dakika moja tu, na hivyo kushindwa kurudia tena. Napenda sana kuwashauri wale wote wenye mazoea haya, ni vyema kuyaacha mapema kwani ya athari kubwa mno hasa unapofikisha umri wa miaka 40 na kuendelea. Ndoa nyingi huvunjika kutokana na majanga haya.

10. Kutokuwa Na Hamu Ya Kingono Na Mwanamke (Loss of Libido).

Sababu kubwa muhusika anakuwa akisha athirika na hiyo punyeto, hukosa hamu ya tendo la ndoa, kiasi kwamba mwanamke anamwona kama katuni.

HITIMISHO:

Tahadhari: Upigaji wa punyeto kupita kiasi ni hatari kwa afya yako. Hairuhusiwi kwa watu walio na wapenzi. Piga kistaarabu.