PID Ni Nini?

Pid ni maambukizi katika viungo vya uzazi vya mwanamke. Maambukizi haya kutokea ikiwa bakteria wanaoambukiza kwa njia ya kujamiiana watasambaa kutoka kwenye uke kwenda kwenye mji wa mimba (uterus), mirija ya uzazi (fallopian tubes) na kwenye ovary (ambapo mayai ya mwanamke hupatikana).

Sababu Za Pid:

Zifuatazo ni sababu zinazochangia mwanamke kupata ugonjwa wa pid ambazo ni pamoja na:

1) Magonjwa Ya Zinaa.

Magonjwa ya zinaa kama vile kisonono (gonorrhea) na pangusa (chlamydia) yanaweza kuchangia mwanamke kupata ugonjwa huu wa pid. Mwili wa mwanamke unapokuwa na afya njema, mlango wa kizazi (cervix) huwa na uwezo mkubwa wa kuzuia bakteria wasiweze kuingia katika viungo vya ndani vya uzazi kutoka ukeni.

Hata hivyo wakati mlango wa kizazi unapokuwa wazi na kuruhusu magonjwa ya zinaa kuingia hasa kisonono (gonorrhea) na pangusa (chlamydia), mlango wa kizazi hupata maambukizi na kisha hupoteza uwezo wake na hivyo kuruhusu maambukizi na bakteria kuingia na kufika juu kwenye viungo vya uzazi.

magonjwa ya zinaa

2) Historia Ya Kuugua Ugonjwa Wa Pid.

Hii pia ni mojawapo ya sababu zinazoweza kuchangia mwanamke kupata ugonjwa wa pid, ambapo mwanamke ambaye umeshawahi kuugua pid kabla anaweza kuugua tena ugonjwa huo, hii ni kutokana na ugonjwa huo kutotibiwa vizuri hapo awali.

3) Matumizi Ya Vipandikizi Vya Ndani Ya Mfuko Wa Uzazi.

Matumizi ya vipandikizi (kitanzi) vya ndani ya mfuko wa uzazi vijulikanavyo kwa kitaalamu kama intrauterine contraceptive device (IUCD) kama njia mojawapo ya uzazi wa mpango yanaweza kuchangia mwanamke kupata maambukizi ya ugonjwa wa pid kwani wakati mwingine kitanzi huweza kuwahifadhi bakteria wanaotokana na magonjwa ya zinaa kwa urahisi.

kitanzi

4) Kujisafisha Uke Kupita Kiasi (Excessive Vaginal Douching).

Kujisafisha uke kupita kiasi kunaharibu mpangilio wa kawaida wa bakteria wazuri kwenye uke wajulikanao kama normal flora. Baadhi ya wanawake wanadhani kujisafisha sana uke husaidia kuondoa mambukizi, lakini ukweli ni kwamba uke umeumbwa na uwezo wa kujisafisha wenyewe (vagina is self cleansing). Kwa hiyo mwanamke anapotumia kemikali na spray kujisafisha uke unaua bakteria wazuri na kuongeza hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa pid.

vaginal douching

5) Kufanya Ngono Bila Kutumia Kinga.

Kufanya ngono bila kutumia kinga (kondomu) kunaongeza uwezekano wa mwanamke kupata magonjwa ya zinaa kama vile kisonono, kaswende, pangusa n.k. Bakteria wanaotokana na magonjwa hayo ya zinaa  husambaa kutoka kwenye Uke kwenda kwenye mji wa mimba (uterus), mirija ya uzazi (fallopian tubes) na kwenye ovary (sehemu ambapo mayai ya mwanamke hupatikana) na hivyo kusababisha ugonjwa wa pid.

6) Mwanamke Kuwa Na Wapenzi Wengi (Multiple Sexual Partners).

Mwanamke kuwa na mpenzi (mwanaume) ambaye ana wanawake wengi nje kunaongeza uwezekano wa mwanamke uyo kupata ugonjwa wa pid, hii ni kutokana na hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama vile kisonono, kaswende, pangusa kutokana na uwepo wa ngono zembe baina ya wapenzi hao.

multiple sexual partners

Dalili Za Pid Kwa Mwanamke:

Zipo dalili kadhaa za ugonjwa wa pid kwa mwanamke, miongoni mwa dalili hizo ni pamoja na:

1) Kuhisi maumivu ya tumbo hasa maeneo ya chini ya kitovu

2) Kupata maumivu ya mgongo

3) Kupata utoko mchafu sehemu za siri, utoko huu huambatana na harufu mbaya

4) Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa

5) Kupata maumivu/kutokwa na damu wakati wa tendo la ndoa 

6) Kutokwa damu bila mpangilio wakati wa hedhi

7) Kupata homa

8) Wakati fulani kuhisi kichefuchefu kama mwanamke mjamzito na kutapika

Dawa Ya Pid Ya Hospital:

Matibabu ya pid kwa kutumia dawa yataondoa mara moja maambukizi yanayosababishwa na pid lakini hakuna njia ya kukarabati makovu au uharibifu kwenye njia ya viungo vya uzazi uliotokana na pid.

Dawa za Pid zinazoweza kutolewa na daktari ni pamoja na: Metronidazole tabs 400mg TDS (3x), doxycycline tabs 100mg BID (2x)  na IV ceftriaxone 1g stat (sindano) kwa muda wa wiki2.

Dawa Ya Pid Ya Kienyeji:

Dawa ya pid ya kienyeji (asili) ni pamoja na PANACEA natural product, hii ni dawa ya asili iliyotengenezwa kutokana na mimea na matunda.

panacea

Kwa pid ya muda mfupi (Acute pid) mgonjwa atahitajika kutumia panacea, dozi ya wiki2 lakini kwa pid ya muda mrefu (chronic pid) mgonjwa atahitajika kutumia panacea, dozi ya wiki4.

Matumizi ya panacea yanaambatana na mchanganyiko wa vitu vingine vya asili ambayo ni pamoja na karafuu, mdalasini, tangawizi mbichi na asali mbichi.

By the way kupata dawa hii bonyeza link hapa: “Jinsi Ya Kutokomeza P.I.D Bila Ya Kuchoma Sindano…

HITIMISHO:

Ni muhimu kuonana na daktari ili kufanya vipimo na kutambua matibabu sahihi ikiwa una wasiwasi wowote kuhusu PID au maambukizi ya muda mrefu ya mfumo wa uzazi.

Matibabu sahihi ni muhimu ili kuzuia madhara zaidi kwa afya yako ya uzazi.

Mtu Mwenye Pid Anaweza Kupata Mimba?

Ndiyo, mtu mwenye PID (Pelvic Inflammatory Disease) anaweza kupata mimba, lakini hali hii inaweza kuongeza hatari za matatizo ya ujauzito kama vile mimba kutunga ya nje ya uzazi (ectopic pregnancy) au hatari za kuharibika kwa mimba.
PID ni maambukizi katika sehemu za ndani za uzazi, kama vile mirija ya uzazi (fallopian tubes), kizazi (uterus), na ovari (ovary).
Maambukizi haya yanaweza kusababisha uharibifu kwenye mirija ya uzazi na tishu zingine za uzazi, na hivyo kusababisha matatizo ya uzazi kwa baadhi ya wanawake.
Hata hivyo, si kila mwanamke mwenye PID atakosa kupata mimba. Uwezekano wa kupata mimba unaweza kutofautiana kutoka kwa mwanamke mmoja hadi mwingine kulingana na ukali wa PID na kiasi cha uharibifu uliotokea.
Baadhi ya wanawake wenye PID wanaweza kupata mimba bila shida yoyote, wakati wengine wanaweza kukabili matatizo ya uzazi au kuhitaji matibabu ya uzazi ili kupata mimba.