Mambo 7 Muhimu Usiyo yajua Kuhusu Ugonjwa Wa Pangusa.

Ugonjwa wa pangusa ni ugonjwa wa zinaa unaoambukizwa kwa njia ya ngono. Ugonjwa huu unajulikana kwa kitaalamu kama ‘chancroid’.

Ugonjwa huu huleta vidonda vikubwa sana kwenye sehemu za siri na kusababisha kulika kwa sehemu hizo, huweza kuzimaliza kabisa sehemu za siri kama matibabu yasipopatikana.

Ugonjwa huu hupatikana kwenye sehemu za joto na wagonjwa wengi ni wanawake wanaojiuza hasa sehemu za mijini. Ugonjwa huu hurahisisha zaidi maambukizi ya virusi kwa ukimwi kwa waathirika wa ugonjwa huu.

Maambukizi ya ugonjwa wa pangusa huenea zaidi kwa vijana wenye umri wa miaka 16-25.

Baada ya kuambukizwa ugonjwa wa pangusa mgonjwa huchukua siku 3 mpaka 14 kuanza kuonyesha dalili.

Picha za ugonjwa wa pangusa:

ugonjwa wa pangusa kwenye uume
ugonjwa wa pangusa kwenye uke

Ugonjwa Wa Pangusa Unasababishwa Na Nini?

Ugonjwa wa pangusa unasababishwa na bakteria wanaojulikana kwa kitaalamu kama ‘Haemophilus ducreyi’. 

Bacteria hawa huweza kupita kwenye ngozi laini kama ya uke kirahisi bila hata kuwepo kwa michubuko. Wanawake huweza kuhifadhi bakteria hawa bila kuonyesha dalili yeyote na kuwaambukiza wanaume wengi zaidi kupitia ngono zembe.

Soma pia hizi makala:

Tabia Hatarishi Zinazochangia Kupata Ugonjwa Wa Pangusa:

Zifuatazo ni tabia hatarishi zinazomuweka mtu (mwanaume/mwanamke) katika hatari ya kupata ugonjwa wa pangusa ambazo ni pamoja na:

1) Kufanya ngono isiyosalama na mgonjwa mwenye pangusa.

2) Kufanya ngono isiyo salama na wanawake wanaojiuza hasa sehemu za mijini (sex workers).

3) Kuwa na wapenzi wengi au kujamiiana na mtu mwenye wapenzi wengi (multiple sexual partners).

4) Upungufu wa kinga mwilini (immunosuppresion).

5)  kuishi kwenye maeneo ambayo kuna idadi kubwa ya wagonjwa wa pangusa.

Dalili Za Ugonjwa Wa Pangusa:

Zifuatazo ni dalili za ugonjwa wa pangusa ambazo ni pamoja na:

A) Dalili Za Pangusa Kwa Mwanaume.

Dalili za ugonjwa huu kwa mwanaume ni pamoja na:

1) Kutokwa uchafu mweupe, au wenye ukijivu au majimaji kwenye uume.

2) Kuhisi maumivu, kutojisikia raha au kuhisi kuwaka moto kwenye uume hasa wakati wa kukojoa.

3) Uvimbe sehemu za korodani na kuhisi maumivu sehemu hizo.

chancroid in males

B) Dalili Za Pangusa Kwa Mwanamke.

Dalili za ugonjwa huu kwa mwanamke ni pamoja na:

1) Kutokwa uchafu usio wa kawaida kwenye uke.

2) Majeraha au kuwaka moto wakati wa kukojoa.

3)  Maumivu wakati wa kujamiiana (dyspareunia).

chancroid in female

Uchunguzi Na Vipimo Vya Ugonjwa Wa Pangusa:

Daktari mzoefu anaweza akagundua ugonjwa huu bila vipimo vyovyote lakini kwa uhakika zaidi majimaji yanayotoka sehemu za siri huchukuliwa na kupimwa maabara.

Dawa Ya Pangusa:

Dawa zinazotumika kutibu ugonjwa wa pangusa ni pamoja na:

1) Azithromycin – 1 g Vidonge (PO) kama dozi au

2) Ceftriaxone – 250 mg kwa njia ya Sindano (IM) Kama dozi au

3) Erythromycin base – 500 mg (PO) Kila baada ya Masaa 8 kwa muda wa siku 7 au

4) Ciprofloxacin – 500 mg (PO) Mara mbili kwa siku au Kila baada ya Masaa 12 kwa muda wa siku 3

Kumbuka: Azithromycin na ceftriaxone zimeonyesha mafanikio katika matibabu ya pangusa.

Ceftriaxone ni chaguo la matibabu kwa mama mjamzito, ingawa ciprofloxacin imeonyesha kutoa madhara machache kwa mtoto akiwa tumboni kwa mama na mama anayenyonyesha.

Wapenzi wenye maambukizi ya Pangusa wachunguzwe, kupimwa na kutibiwa kulingana na dalili ambazo huanza kujitokeza ndani ya siku 3 mpaka siku 14.

Madhara Ya Ugonjwa Wa Pangusa:

Yafuatayo ni madhara yanayoweza kutokea endapo mgonjwa mwenye pangusa atashindwa kupata matibabu haraka, ambayo ni pamoja na:

1) Vidonda vikubwa sana kwenye sehemu za siri na kusababisha kulika kwa sehemu hizo.

2) Ugonjwa huu hurahisisha zaidi maambukizi ya virusi kwa ukimwi kwa waathirika wa ugonjwa huu.

Jinsi Ya Kujikinga Na Ugonjwa Wa Pangusa:

Kujikinga na ugonjwa wa pangusa unashauriwa kufanya mambo yafuatayo;

1) Kutumia kondomu kila mara unapojamiiana.

2) Kuwa na mwenzi mmoja mwaminifu.

3) Kuachana na tabia ya kununua malaya na kufanya nao ngono zembe.

HITIMISHO:

Kwa ushauri na tiba ya magonjwa ya afya ya uzazi wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487.

Ulikuwa nami daktari wako Dr. Isaya Febu.