Fangasi Ukeni:
Fangasi ukeni ni muwasho sehemu ya ndani ya uke ambao unaweza kuambatana pia na kuvimba kwa uke. Maambukizi ya fangasi sehemu za siri imekuwa ni tatizo kubwa sana duniani, 75% ya wanawake wote duniani wanaosumbuliwa na tatizo hili wanatafuta dawa ya fangasi ukeni kila siku. Maambukizi haya ya fangasi katika sehemu za siri za mwanamke husababishwa kwa kiasi kikubwa na fangasi aina ya candida albicans na maambukizi haya pia hujulikana kama vaginal yeast infection au vaginal thrush.
Chanzo Cha Fangasi Ukeni:
Chanzo cha fangasi ukeni ni fangasi wajulikanao kwa kitaalamu kama “candida albicans,” ambao kwa kawaida huishi kwenye sehemu za siri bila kusababisha madhara, lakini wanapoongezeka kupita kiasi, husababisha maambukizi hayo. Fangasi ukeni ni maambukizi ya kawaida sana kwa wanawake na yanaweza kumuathiri mwanamke wa umri wowote.
Mahali Wanapokaa Hawa Fangasi (Candida Albicans) Katika Mwili:
Candida albicans hupatikana katika mdomo, mpira wa kupitishia chakula, kibofu cha mkojo, uume au katika uke na kwenye ngozi pia, vilevile hupatikana kwenye tumbo, kwapa.
Bakteria hawa huishi katika sehemu hizo bila kuleta madhara, isipokuwa pale mazingira ya eneo husika yanapobadilika mfano mabadiliko katika hali ya pH, tutambue pH ya mwanamke ndani ya uke ni 4-4.5 au uwiano wake na vimelea (microorganisms) wengine hivyo huharibiwa kutokana na magonjwa mbalimbali, pia kupungua kwa kinga ya mwili kutokana na magonjwa mbalimbali hupelekea kukua kwa Candida albicans, ndio maana wagonjwa wenye maradhi ya ukimwi na kansa, ama wanaopata matibabu ya mionzi huwa kwenye hatari kubwa ya kuumwa fangasi.
Maambukizi ya fangasi ukeni yanaweza isiwe ugonjwa hatari pale unapoanza lakini huleta usumbufu na harufu kali na hivyo mgonjwa kukosa amani.
Picha Za Fangasi Ukeni:
Mambo Yanayoongeza Hatari Ya Kupata Fangasi Ukeni:
Yafuatayo ni baadhi ya mambo yanayomuweka mwanamke katika hatari ya kupata fangasi ukeni;
- Ujauzito.
- Kushuka kwa kinga ya mwili kutokana na kuugua magonjwa mbalimbali kama vile kisukari, UKIMWI.
- Matumizi yaliyokithiri ya dawa hasa zile za kuua bakteria (antibiotics).
- Wanawake wenye umri wa miaka 20-30 wapo katika hatari ya kupata maambukizi haya wakati wale ambao wamekoma hedhi (menopause) na wale ambao hawajaanza kupata hedhi hawako katika hatari kutokana na mazingira au vitu wanavyotumia.
- Matumizi ya mara kwa mara ya vidonge vya majira (oral contraceptive pills).
- Msongo wa mawazo uliokithiri.
- Kujamiiana kwa njia ya kawaida mara tu baada ya kujamiiana kupitia haja kubwa (anal sex).
- Matumizi ya vilainishi wakati wa kujamiiana husababisha maambukizi pia.
- Kuwa na historia ya kupata matibabu ya homoni (hormonal replacement therapy).
- Kuwa na utapiamlo (malnutrition).
- Kuvaa nguo za ndani zisizokauka vizuri na kuvaa mavazi yanayoleta sana joto sehemu za siri.
- Matumizi makubwa ya mipira wakati wa ngono mfano condoms.
Kumbuka:
Wanawake wapo katika hatari kubwa ya kuugua fangasi za sehemu za siri ukilinganisha na wanaume, lakini pia hata wanaume huambukizwa tatizo hili.
Aina Za Fangasi Ukeni:
Maambukizi ya fangasi ukeni yamwegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni;
A) Maambukizi Yasiyo Makali (Uncomplicated Vaginal Thrush).
Katika aina hii mgonjwa hupatwa na maambukizi mara moja hadi nne kwa mwaka. Pia dalili huwa si za kuogopesha na maambukizi haya husababishwa na fangasi aina ya candida albicans.
B) Maambukizi Makali (Complicated Vaginal Thrush).
Katika kundi hili mgonjwa hupatwa na maambukizi zaidi ya mara nne au zaidi kwa mwaka. Dalili zake huwa ni za kuogopesha kama maambukizi yatakuwa yametokea kipindi cha ujauzito, ugonjwa wa vvu, ugonjwa wa kisukari n.k
Soma pia hizi makala:
- Ujue Ugonjwa Wa PID(Pelvic Inflammatory Disease).
- Fahamu Njia 6 Zinazotumika Kuondoa Harufu Mbaya Ukeni.
- Uti Kwa Wanawake: Zijue Sababu 3 Zinazopelekea Kuugua Uti, Tiba Mbadala Na Kinga.
Dalili Za Fangasi Ukeni:
Zifuatazo ni baadhi ya dalili za fangasi ukeni ambazo ni pamoja na;
- Kuwashwa sehemu za siri.
- Kuhisi maumivu makali wakati wa kujamiiana.
- Kuhisi kuwaka moto sehemu za siri mara baada ya kutoka kufanya tendo la ndoa au kutoka kukojoa (burning sensation).
- Kuvimba na kuwa mwekundu katika mdomo wa nje ya uke (labia minora).
- Kupata vidonda ukeni (soreness).
- Kupata maumivu wakati wa kukojoa na kutokwa na uchafu wa rangi nyeupe au kijivu unaoweza kuwa mwepesi, mzito au majimaji.
- kutoa harufu mbaya ukeni.
Kumbuka: Dalili na viashiria hivi huwa mbaya zaidi mwanamke anapokuwa mwezini (hedhi).
Matibabu Ya Fangasi Ukeni:
Matibabu ya ugonjwa huu wa fangasi hupatikana hospitali na kutolewa kupitia vipimo vya uchunguzi na majibu yalivyotoka. Pamoja na hayo matibabu ya ugonjwa huu hospitali sio ya uhakika kwa sababu dawa za hospitali hazitibu chanzo cha tatizo, hivyo ndio maana tatizo hili huwa linajirudia baada ya muda, pia ugonjwa huu unaweza kujikinga nao kwa kuepuka mambo mbalimbali na kuzingatia kanuni ya afya na usafi.
Dawa Ya Fangasi Ukeni Ya Vidonge:
Klotrimazole (clotrimazole) ni dawa ya vidonge ya kuua fangasi ukeni (antifungal). Dawa hii ina majina mengi ya kibiashara ikiwemo Cruex, Desenex, Fungoid, Lotrimin, Mycelex, Clotrimazole, Canesten, Clotrimaderm, Myclo, FungiCURE na Candistat. Hupatikana pia kama dawa ya vidonge vya kuweka ukeni (vaginal pessaries).
Jinsi Ya Kutumia Klotrimazole (Vaginal Pessaries) Kutibu Fangasi Ukeni;
Tumia dawa hii wakati unaenda kulala. Hakikisha mikono yako ipo safi, kisha lala chali, panua magoti ukiwa umeyainua. Ingiza dawa ukeni kwa kutumia kifaa chake maalum. Kama haina kifaa maalum, baada ya kuitoa kwenye gamba lake, ingiza kidonge hicho kwenye uke na kisha kisukumize kwa kidole cha kati mpaka kifike mwisho. Baada ya hapo nawa mikono yako. Tumia kwa muda uliolekezwa na daktari.
Madhara Ya Fangasi Ukeni:
Madhara yafuatayo yanaweza kutokea ikiwa mgonjwa mwenye fangasi ukeni atashindwa kupata tiba mapema;
1. Mimba Kuharibika.
Hii hutokea kwa mama mjamzito ambaye hakupata tiba ya maambukizi ya fangasi ukeni mapema ambapo maambukizi hayo huenea sehemu mbalimbali za via vya uzazi na kuharibu mji wa mimba (uterus), sehemu ambapo mimba hujishikiza (fetal implantation) na kupelekea mimba kuharibika kabla ya wakati wake.
2. Kupata Homa Na Kizunguzungu.
Hali hii hutokea kwa sababu ya kubadilika kwa hali ya kawaida ya mwili na kuharibika kwa sehemu mbalimbali za mwili kutokana na maambukizi ya fangasi hali ambayo husababisha kubadilika kwa joto la mwili pia.
3. Kuongezeka Kwa Miwasho Sehemu Za Siri.
Madhara ya fangasi ukeni husababisha kuwepo kwa miwasho kwenye sehemu za siri ambapo mwathirika hujikuna kila wakati, hali hii huongeza uwezekano mkubwa wa kuenea kwa ugonjwa wa fangasi ukeni kwa sababu mwenye maambukizi kama anajikuna na anawagusa wengine wanaomzunguka basi anaweza kusambaza maambukizi hayo kwa wanaomzunguka kwa urahisi.
4. Maumivu Makali Wakati Wa Kukojoa.
Hali hii hutokea kwa mgonjwa Mwenye tatizo la fangasi ukeni, pale ambapo maambukizi yameenea sehemu mbalimbali za via vya uzazi na kusababisha michubuko. Hivyo wakati wa haja ndogo, mgonjwa akikojoa na mkojo ukagusa sehemu ya michubuko maumivu makali hutokea na kusababisha kukosa raha.
Jinsi Ya Kujikinga Na Fangasi Ukeni:
Yafuatayo ni mambo ya muhimu ambayo mwanamke anapaswa kuzingatia ili kujikinga na fangasi ukeni;
- Vaa nguo za ndani ambazo hazibani na zilizotengenezwa kwa pamba au hariri.
- Epuka kufanya mapenzi na mpenzi wako mwenye maambukizi haya mpaka pale atakapotibiwa na kupona kabisa.
- Osha sehemu zako za siri kwa kutumia maji safi na jikaushe kwa kutumia taulo au kitambaa safi.
- Epuka kuoga maji ya moto sana (hot baths), tumia maji ya vuguvugu.
- Kula mlo wenye virutubisho kama vile mboga za majani, matunda.
- Kunywa maziwa aina ya mtindi yenye live culture mara kwa mara yatakusaidia.
- Epuka matumizi ya vifaa vya kupanga uzazi na vifaa vya kufanyia mapenzi (sex toys, diaphragm, cervical caps) husababisha maambukizi ya fangasi ukeni.
- Epuka kutumia sabuni za kemikali au dawa kuoshea uke.
- Usivae nguo zenye unyevunyevu, hakikisha unavaa nguo zilizokauka vizuri.
- Epuka kutumia kiholela dawa za Antibiotics, kama huna ulazima wa kutumia antibiotics, acha kutumia.
Dawa Za Asili Za Fangasi Ukeni:
Zifuatazo ni baadhi ya dawa za asili za fangasi ukeni ambazo unaweza kutumia uwapo katika mazigira yako ya nyumbani kabla ya kumuona mtaalamu wa afya (daktari);
- Lemonade.
Hii ni mojawapo ya dawa ya asili ya fangasi ukeni ambayo unaweza kuiandaa na kuitumia uwapo katika mazingira yako ya nyumbani.
Jinsi Ya Kuandaa Lemonade Kutibu Fangasi Ukeni;
Lemonade inaandaliwa kwa kutumia limao, asali na unga wa mdalasini kidogo.
chukua limao kubwa 12 zikatekate kila moja, tumbukiza ndani ya sufuria na weka maji lita 3, chemsha mchanganyiko huo mpaka limao ziive (zisiive sana).
Ipua na utoe zile nyama nyama za ndani za limao moja baada ya nyingine, tupa maganda ya hayo malimao, baada ya hapo chuja mchanganyiko huo kupata juisi ambayo itakuwa na wastani wa ujazo wa lita 2 na nusu hivi. Chukua sufuria nyingine changanya asali nusu lita na hiyo juisi ya limao lita 2 na nusu, ongeza maji safi ya kawaida lita 2, vijiko vikubwa vitatu vya unga wa mdalasini ndani ya juisi ili kupata lemonade ya ujazo wa lita 5 kisha kunywa robo lita kutwa mara 2 kwa siku kwa muda wa siku 10.
- Maziwa Ya Mtindi.
Maziwa ya mtindi au bidhaa zitokanazo na maziwa ya mtindi, ni dawa ya kuaminika ya fangasi ukeni ambapo unaweza kutumia njia yoyote ile kuweka maziwa mtindi kwenye uke kwa kiasi kidogo, labda kwa ujazo wa kijiko kidogo cha chai, ukeni wakati wa kulala na asubuhi unajisafisha kama kawaida. Pia unashauriwa kula maziwa ya mtindi kiasi cha kutosha kila siku.
Uke una uwezo wa kujisafisha wenyewe na kuondoa mabaki yote ya mtindi na kubakisha kiwango kikubwa cha bakteria wazuri (Lactobacilli) pamoja na hali ya tindikali yenye uwezo wa kuzuia kujitokeza na kukua kwa fangasi. Mara zote bakteria hawa wanaopatikana kwenye maziwa ya mtindi kama bidhaa ijulikanayo kwa kitaalamu kama”Supplements of Acidophiles”.
- Kitunguu Saumu.
Kitunguu saumu kina sifa na uwezo wa kuua bakteria na hata virusi mwilini. Hii pia ni mojawapo ya dawa ya asili ya fangasi ukeni ambayo unaweza kuitumia uwapo katika mazingira yako ya nyumbani.
Jinsi Ya Kutumia Kitunguu Saumu Kutibu Fangasi Ukeni;
Chukua kitunguu saumu kimoja kisha kigawanyishe katika punje punje, chukua punje 6 menya punje noja baada ya nyingine, kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo sana kwa kisu. Meza hivyo vipande vidogo vidogo vya kitunguu saumu na maji nusu lita kila asubuhi uamkapo na unapoenda kulala kwa muda wa wiki 2 hadi 3.
Pia unaweza kuweka hivyo vpande vidogo vidogo vya kitunguu saumu ndani ya kikombe chenye maziwa ya mtindi kisha koroga vizuri na unywe, hii itakusaidia kupunguza harufu mbaya ya kitunguu saumu mdomoni huku ukipata faida nyingine muhimu zilizomo kwenye maziwa ya mtindi.
Tahadhari: Mama mjamzito chini ya miezi 4 hashauriwi kutumia kitunguu saumu.
- Mafuta Ya Nazi.
Kama fangasi hao wa ukeni watajitokeza hadi sehemu kidogo ya nje ya uke na ukapata muwasho pia, hakikisha unapaka sehemu ya nje ya uke mafuta ya asili ya nazi yaliyotengenezwa nyumbani. Hii ni dawa tosha kwa fangasi wowote wanaoshambulia sehemu ya nje ya uke.
HITIMISHO:
Suluhisho La Kudumu La Fangasi Ukeni:
Dawa za asili zilizotajwa hapo juu zitakusaidia kuleta nafuu hivyo tunakushauri kutumia virutubisho (nutritional supplements), hizi ni dawa za asili kabisa ambazo zinaenda kupambana na bakteria wabaya peke yake.
Pia kuna sabuni ya maji (Care) ambayo imethibitishwa na zaidi ya nchi 160 duniani, iko vizuri kwa ajili ya kuoshea sehemu za siri ambayo ina pH sawa na joto la ukeni. Inasaidia sana kwa watu ambao tayari wameshapata hii changamoto na ambao hawataki kukutana na hii changamoto.
Kujua virutubisho hivyo pamoja na sabuni ya maji (Care) bonyeza hapa: “Je Umehangaika Kwa Muda Mrefu Kutibu Fangasi Ukeni Bila Mafanikio…?
Kwa uhitaji wa updates, vitabu (e-books) bure kuhusua afya jisajili (subscribe) kupitia email yangu kwa kubonyeza hii link: https://isayafebu.beehiiv.com/subscribe
Nahitaji tiba nitabataje ivo viruthubisho na mafuta
Nicheki 0625305487
Nipo njombe napataje tiba
Nateseka sana, nawashwa sana sehemu za Siri mpaka nakosa amani, Furaha nakuwa mtu wa mawazo muda wote na Niko mjamzito Mimi. Nataman sana kupata tiba muda mwingi nikivaa nguo ya ndani zinalowa muda wote na kupelekea kuwashwa Kila wakati na nikijikuna ndo nahic nafuu. Nifanye Nini, nimejikuta mpka nalia kabisa
tiba ipo…wasiliana nasi kwa simu namba 0625305487
Nahitaji kujua kama kuna vipimo maana nikisoma dalili za hormonal imbalance na fangasi dalili zao zinafanana…..sasa hapa nakuwa sielewi nichukue dawa ya aina gani
vipimo pia tunafanya…karibu sana katika ofisi zetu zilizopo mikoa yote nchini Tanzania
Nipo Moshi nahitaji tiba naomba nielekeze huduma Moshi nitapata sehemu gani
Moshi mjini, jengo la kilimani plaza
Thanks
Ivo vidonge vinapatikana pharmacy
Hapana…vinapatikana ofisini kwetu sinza madukani, DSM
Hapana…vinapatikana ofisini kwetu sinza madukani, DSM
Thanks much
Thanks for the information..mm nawashwa ukeni..Sio Sana Ila huwa nawashwa naona Nina fangasi
Mimi nawashwa ukeni..Sio Sana Ila nimejua nina fangasi maana dalili hiyo Niko nayo..thanks for the information
Karibu tena…
Habari, hiyo lemonade kwa mjamzito anaruhusiwa kutumia?
Anatumia
Mimi ninashida ya kutokwa maji yenye harufu na baadhi ya muda napata maumivu makali ukeni na kiuno pia kinaniuma mno nina miezi miwili toka nimejifungua. Baada ya kukata damu ndio hali hyo imajitokeza naomba ushauri sijui shida ninini
Unapatikana wapi?
Mimi plz natokwa na uchafi kama vile umeganda mwingi mpaka naogopa na unakua na shombo, ni dawa gan itanisaidia plz msaada
Unapatikana wapi?
Mm kuta za uke zimeliwa zote had najiskia vbaya yan
Nipo mkwajuni songwe nimepima meambiwa ninafangasi kwenye kibofu napataje Tina yake
Nicheki 0625305487 kwa msaada wa tiba
Mm kuta za uke zimeliwa zote had najiskia vbaya yan
Ugonjwa unasumbua sana. Na harufu inatoka mpaka aibu
Naitwa Getrud Niko.kilimanjaro……napata shida yakutokwa na haruf mbaya uken pia nimeenda hospital wanasema mpaka uapasuajii ndio nitapona pia kuna mda nikikutana na mwenza wangu naumia…yeye mwenyew amechoka na halii hii doctor nisaidie nimechoka jamaniii
Tiba ipo…nichek 0625305487
Hello
Naomba kuuliza, nimetengeneza lemon Sasa kadri siku zinavyoenda inatengeneza povu kama kuchacha ndivyo ilivyo ? Kama ndivyo haina madhara ? Na pia nikinywa kuanzia kiunoni kwenda chini kama nakuwa mzito miguu inawaka moto , naomba ushauri
Mbeya mnapatikana wap??
Soweto karibu na hotel ya mkulu
Dodoma mnapatikana wap na gharama zenu ni zipi
Tunapatikana dodoma mjini, makulu
Gharama ya dawa-TZS 70,000/=
Nameliwa kuta za uke nipo Moshi ila ni mwanachuo natumia bima inaruhusiwa
Hapana hatupokei bima
mm fangasi zime nifanya uke kua mkavu nifanyaj ili niwe sawaa msaaada jmn
Kwa msaada wa tiba piga 0625305487
Habar doctor Mimi ni mjamzito lakin kuna tatizo la kuwashwa ukeni na kutoka na uchafu na harufu na sijui nitumie dawa gani.
wasiliana nasi 0625305487 kwa msaada wa tiba
Habar doctor Mimi ni mjamzito nasumbuliwa na tatizo la kuwashwa ukeni na kutoka na uchafu na pia harufu mbaya naomba msaada wako