Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease).

Ugonjwa Wa Pid Ni Nini?

Ugonjwa wa pid ni maambukizi katika viungo vya uzazi vya mwanamke.

Maambukizi haya kutokea ikiwa bakteria wanaoambukiza kwa njia ya kujamiiana watasambaa kutoka kwenye uke kwenda kwenye mji wa mimba (Uterus), mirija ya uzazi (Fallopian tubes) na kwenye ovari (ambapo mayai ya mwanamke hupatikana).

Ugonjwa Wa Pid Husababishwa Na Nini?

Ugonjwa wa pid husababishwa na magonjwa ya zinaa kama vile kisonono (gonorrhea) na pangusa (chlamydia). Mwili wa mwanamke unapokuwa na afya njema, mlango wa kizazi huwa na uwezo mkubwa wa kuzuia bakteria wasiweze kuingia katika viungo vya ndani vya uzazi kutoka ukeni.

Hata hivyo wakati mlango wa kizazi unapokuwa wazi na kuruhusu magonjwa ya zinaa kuingia hasa kisonono (gonorrhea) na pangusa (chlamydia), mlango wa kizazi hupata maambukizi na kisha hupoteza uwezo wake na hivyo kuruhusu maambukizi na bakteria kuingia na kufika juu kwenye viungo vya uzazi.

Soma pia hii makala: Zijue Dawa Za Asili Za Fangasi Ukeni Ambazo Hakuna Mtaalamu Wa Afya Atathubutu Kukwambia.

Jinsi Mwanamke Anavyo Ambukizwa Ugonjwa Wa Pid:

Kuna njia kadhaa ambazo mwanamke anaweza kuambukizwa ugonjwa wa pid. Njia hizo ni pamoja na:

A) Kama  Una Ugonjwa Wa Zinaa Na Hujatibiwa.

B) Kufanya Ngono Zembe Isiyosalama (Yaani Kulala Na Wanaume Tofauti Tofauti).

C) Kuwa Na Mpenzi Ambaye Ana Wanawake Wengi Nje. 

D) Kama Umeshawai Kuwa Na Historia Ya Kuugua Pid Kabla. 

E) Maambukizi Ya Nje Ya Uzazi Mara Baada Ya Kutoa Mimba Kwa Njia Zisizo Salama (Post Abortion) Au Mara Baada Ya Mimba Kutoka (Miscarriage).

F) Maambukizi Ya Nje Ya Uzazi Hasa Kipindi Mara Baada Ya Kujifungua (Postpartum Period).

G) Kutumia Vipandikizi Vya Ndani Ya Mfuko Wa Uzazi (IUCD) Kama Njia Mojawapo Ya Uzazi Wa Mpango.

H) Kuambukizwa Kupitia Damu Iliyo Na Vimelea Vya Pid. 

I) Kutuma Sana Vidole Wakati Wa Kusafisha Uke (Excess Vaginal Douching).

Dalili Za Pid Kwa Mwanamke:

 Zipo dalili kadhaa za ugonjwa wa pid kwa mwanamke, miongoni mwa dalili hizo ni pamoja na;

A) Kuhisi Maumivu Ya Tumbo Hasa Maeneo Ya Chini Ya Kitovu.

B) Kupata Maumivu Ya Mgongo.

C) Kupata Utoko Mchafu Sehemu Za Siri, Utoko Huu Huambatana Na Harufu Mbaya.

D) Kuhisi Maumivu Wakati Wa Kukojoa.

E) Kupata Maumivu/Kutokwa Na Damu Wakati Wa Tendo La Ndoa. 

F) Kutokwa Damu Bila Mpangilio Wakati Wa Hedhi.

G) Kupata Homa.

H) Wakati Fulani Kuhisi Kichefuchefu Kama Mwanamke Mjamzito Na kutapika.

doctor and patient

Matibabu Ya Pid:

Matibabu ya pid kwa kutumia dawa yataondoa mara moja maambukizi yanayosababishwa na pid lakini hakuna njia ya kukarabati makovu au uharibifu kwenye njia ya viungo vya uzazi uliotokana na pid. Matibabu ya pid yaweza kuwa:

A) Antibiotics Za Kutibu Pid.

Daktari atakuandikia dawa inayoendana na chanzo cha tatizo lako.Utasubiri siku kama tatu kuona kama dawa ulizopewa zinafanya kazi.

Dawa za Pid zinazotolewa na daktari ni pamoja na; Metronidazole tabs, doxycycline tabs na cefixime tabs

B) Kumtibu Mpenzi Wako.

Kuzuia maambukizi yafaa mpenzi wako afanyiwe uchunguzi na atibiwe.

C) Kuacha Kushiriki Ngono Kwa Muda.

Acha kushiriki ngono hadi utakapomaliza tiba na kuona kuwa umepona.

Madhara Ya Pid:

PID ambayo haikupata tiba inaweza kusababisha makovu na vifuko vyenye maji yenye wadudu kwenye mkondo wa njia ya uzazi ya mwanamke, vitu hivi vinaweza kusababisha madhara ya kudumu kwenye viungo vya uzazi. Madhara yanayoweza kutokea ni pamoja na;

A) Mimba Nje Ya Mirija Ya Uzazi (Ectopic Pregnancy).

PID ndiyo sababu ya mimba kutunga nje ya kizazi, mimba huweza kutunga nje ya kizazi endapo PID imesababisha makovu ndani ya mirija ya uzazi. Makovu haya husababisha yai lililopevushwa kushindwa kusafiri ndani ya mirija ya uzazi kuelekea kwenye nyumba ya mirija ya uzazi. Mimba nje ya uzazi husababisha utokaji wa damu usiowakawaida unaoweza kukatisha maisha ya mwanamke.

B) Ugumba.

Uharibifu wa viungo vya uzazi huweza kusababisha ugumba, kushindwa kupata ujauzito. Kadri unavyozidi kupata PID mara nyingi zaidi ndivyo hatari ya ugumba inavyozidi, kuchelewa kupata tiba ya PID kuongeza hatari ya ugumba.

C) Maumivu Sugu Ya Nyonga.

PID inaweza kusababisha maumivu ya nyonga yanayoweza kudumu miaka mingi. Makovu ndani ya mirija ya uzazi na viungo vingine vya uzazi huweza kuleta maumivu wakati wa kujamiiana na wakati yai hudondoshwa (ovulation).

D) Tubo Ovarian Abscess.

PID huweza kusababisha kutunga kwa usaha na kufanya majipu ndani ya mirija ya uzazi na ovari, ingawa huweza kuota ndani ya nyumba ya uzazi na shingo ya kizazi kama tiba haitatolewa, unaweza kupata maambukizi hatarishi kwa maisha.

Madhara Ya Pid Kwa Mjamzito:

Yafuatayo ni madhara yanayoweza kutokea kwa mama mjamzito endapo atashindwa kupata tiba ya pid mapema;

1) Kujifungua kabla ya wakati au ujauzito kuharibika.

2) Kujifungua mtoto mwenye maambukizi na wakati mwingine hufariki muda mchache baada ya Kujifungua au kujifungua mtoto mfu.

3) Kuziba kwa mirija ya uzazi.

Jinsi Ya Kuzuia Ugonjwa Wa Pid:

Kuna njia kadhaa za kuzuia ugonjwa wa pid.Njia hizi ni pamoja na;

A) Kuwai Kuwaona Wataalamu Wa Afya Mara Dalili Za Ugonjwa Zinapoanza Kujitokeza Au Pindi Tu Unapogundua Kuwa Mpenzi Wako Ana Dalili Za Magonjwa Ya Zinaa Au Anatembea Na Wanawake Wengi.

B) Kufanya Vipimo Mara Kwa Mara Hasa Vipimo Vya Uzazi, Pamoja Na Vipimo Vya Maambukizi Ya Magonjwa Yanayosambazwa Ka Njia Ya Ngono (STI) Hususani Kwa Mgonjwa Wa Chlamydia, Ufanye Vipimo Kila Mwaka Mara Moja.

C) Kutofanya Ngono Mara Baada Ya Kujifungua, Mimba Kutoka Au Mara Baada Ya Kutoa Mimba Ili Kuhakikisha Njia Ya Shingo Ya Uzazi Imefunga Vyema.

D) Njia Hakiki Ya Kujizuia Na Maambukizi Haya Ni Kuacha Ngono Zembe Na Kufanya Ngono Salama.

Dawa Za Asili Za Pid:

Zifuatazo ni dawa za asili ambazo unaweza kuzitumia kutibu ugonjwa wa pid unapokuwa katika mazingira yako ya nyumbani;

A) Kitunguu Saumu.

Kitunguu Saumu Ni Mojawapo Ya Tiba Mbadala Ya Nguvu Katika Kutibu Ugonjwa wa Pid. Ni Dawa Nzuri Dhidi Ya Bakteria Wanao Sababisha Ugonjwa Wa Pid Na Hivyo Moja Kwa Moja Kuwa Muhimu Katika Kutibu Ugonjwa Wa Pid. 

Jinsi ya kutumia kitunguu saumu kutibu pid.

Chukua Kitunguu Saumu Kimoja Na Ukigawe Mara2, Menya Nusu Yake (Punje 10 Au 15), Menya Punje 1 Baada Ya Nyingine Na Kisha Kikatekate (Chop) Vipande Vidogo Vidogo Na Kisu Kisha Meza Kama Unavyomeza Dawa Na Maji Vikombe Viwili Kila Unapoenda Kulala Na Uamkapo Asubuhi Kwa Siku7, Baada Ya Hapo Hakutakuwa Na Maambukizi Ya Pid.

Kumbuka: Matumizi ya kitunguu saumu pamoja na dawa za kushusha presha (anti hypertensive drugs) yanaweza kusababisha presha kushuka zaidi. Hivyo ikiwa unatumia dawa za kushusha presha hashauriwi kutumia kitunguu saumu.

B) Binzari Ya Manjano.

Binzari Ya Manjano Pia Ni Mojawapo Ya Dawa Ya Asili Ambayo Hutumika Kutibu Ugonjwa Wa Pid.

Jinsi Ya Kutumia Binzari Ya Manjano Kutibu Pid.

Chukua Kijiko Kimoja Cha Binzari Ya Manjano Iliyosagwa, Kisha Koroga Kwenye Glass Iliyobeba Asali Mbichi Vijiko Viwili Na Maji, Baada Ya Hapo Kunywa Mchanganyiko Huo Wa Asali Mbichi, Binzari Na Maji, Asubuhi Na Jioni Kwa Muda Wa Siku 7.

C) Baking Soda. 

Kama Ukikosa Kitunguu Swaumu Au Binzari Ya Manjano Unaweza Kutumia Baking Soda Kama Dawa Ya Kutibu Ugonjwa Wa Pid.

Jinsi Ya Kutumia Baking Soda Kutibu Pid.

Chukua Nusu Kijiko Au Kijiko Kimoja Cha Baking Soda, Kisha Koroga Kwenye Glass Iliyobeba Maji Ya Vuguvugu, Baada Ya Hapo Kunywa Mchanganyiko Huo Wa Baking Soda Na Maji Ya Vuguvugu Asubuhi Jioni Kwa Muda Wa Wiki Mbili.

D) Mbegu Za Mlonge.

Vitamini, Madini, Na Homoni Muhimu Zilizomo Kwenye Mbegu Hizi Huufanya Mwili Wako Kuwa Na Usawa Unaohitajika Kiafya Na Hivyo Kukupa Kinga Dhidi Ya Magonjwa Mengi Bila Idadi Ikiwemo Pid (Pelvic Inflammatory Disease). Ikiwa Utakosa Kitunguu Saumu, Binzari Ya Manjano au Baking Soda Katika Mazingira Yako Ya Nyumbani Basi Unaweza Kutumia Mbegu Za Mlonge Kutibu Maambukizi Ya pid.

mbegu za mlonge

Jinsi ya kutibu pid kwa kutumia mlonge.

Chukua Punje 3 Za Mlonge Na Uzimenye Ganda Lake La Juu Kila Moja, Kisha Tafuna Zile Mbegu Zake Za Ndani, Ukimaliza Kuzitafuna Kunywa Maji Ya Kawaida Glass 2 (Nusu Lita), (Epuka Kunywa Maji Ya Baridi yaliyotoka Kwenye Friji), Fanya Hivi Kutwa Mara Tatu.

HITIMISHO:

Ikiwa utahitaji kutokomeza kabisa changamoto ya ugonjwa wa pid baada ya kutumia mojawapo ya tiba asili zilizotajwa hapo, tunakushauri utumie PANACEA natural product, dawa ya asili iliyotengenezwa kutokana na mimea na matunda. Kupata dawa hiyo bonyeza hapa: “Jinsi Ya Kutokomeza P.I.D Bila Ya Kuchoma Sindano…

Lakini pia, kwa uhitaji wa updates, vitabu (e-books) bure kuhusu afya jisajili (subscribe) kupitia email yangu kwa kubonyeza hii link: https://isayafebu.beehiiv.com/subscribe

Ni mimi mwenye kujali afya yako Dr. ISAYA FEBU.

vipimo vya mfumo wa uzazi