Ugonjwa wa kaswende ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na viini vya bakteria vijulikanavyo kama Treponema pallidum. Ugonjwa huu hujulikana kwa kitalaamu kama Syphilis.
Ugonjwa wa kaswende pia inaweza kuambukizwa kutoka kwa mama hadi kwa mtoto wakati wa ujauzito, wakati wa kujamiiana, na kwa kushirikiana sindano na vifaa vya kujidunga. Kushiriki chakula, kukumbatiana, au kutumia bafu moja na mtu aliye na kaswende hakuenezi ugonjwa huo.
Ugonjwa wa kaswende ambao haujatibiwa kwa muda mrefu unaweza kuathiri viungo muhimu kama vile moyo na ubongo. Vile vile ugonjwa wa kaswende ambao haujatibiwa unaweza kusababisha maswala ya kiafya ya muda mrefu kama vile ulemavu, uharibifu wa mfumo wa neva na hata kifo.
Picha Za Ugonjwa Wa Kaswende:
Picha Ya Vipele Vya Kaswende:
Kisababishi Za Ugonjwa Wa Kaswende:
Ugonjwa wa kaswende unasababishwa na maambukizi ya bakteria waitwao Treponema pallidum. Bakteria hawa huingia mwilini kupitia mikwaruzo midogo sana au michubuko kwenye ngozi au utando wa mucous, mara nyingi wakati wa ngono. Ugonjwa huo unaweza kuambukizwa katika hatua zake zote za msingi na sekondari, wakati upele unaweza kutokea kwenye torso, viganja vya mikono, nyayo na sehemu nyingine za mwili.
Soma pia hizi makala:
- Haya Ndiyo Mambo 7 Muhimu Usiyo yajua Kuhusu Ugonjwa Wa Kisonono.
- Mambo 7 Muhimu Usiyo yajua Kuhusu Ugonjwa Wa Pangusa.
Sababu Hatarishi Zinazoweza Kupelekea Kupata Ugonjwa Wa Kaswende:
Yafuatayo ni baadhi ya mambo yanayomuweka mtu katika hatari ya kupata ugonjwa wa kaswende;
1) Kufanya ngono isiyo salama na mtu mwenye maambukizi ya ugonjwa huu hasa kupitia mdomo (oral sex), mkundu (anal sex).
2) Kuzaliwa na mama ambaye alikuwa na kaswende ya kuambukiza wakati wa ujauzito.
3) Kufanya ngono na mtu kutoka nchi au eneo ambalo kaswende ni kawaida.
4) Kupewa damu isiyo salama yenye maambukizi ya bakteria wanaosababisha ugonjwa huu.
Dalili Za Ugonjwa Wa Kaswende:
Kuna hatua nne za ugonjwa huu wa kaswende. Ni dalili gani utaziona, inategemea na ugonjwa upo katika hatua ipi kati ya hizo nne. Hatua hizo zinaweza kuingiliana na dalili si lazima zitokee kwa mtiririko ule ule. Unaweza pia ukawa na kaswende na usione dalili zo zote kwa miaka kadhaa. Zifuatazo ni dalili za ugonjwa wa kaswende ambazo ni pamoja na;
A) Dalili Za Ugonjwa Wa Kaswende Kwa Mwanaume.
1) Kidonda kwenye sehemu za siri (uume), mdomo au makalio. Kidonda hiki hujulikana kama chancre.
2) Vipele kwenye viganja vya mikono na nyayo za miguu ambavyo ni vyekundu au vyekundu-kahawia.
3) Maumivu ya kichwa na mwili (misuli).
4) Uchovu.
5) Homa.
6) Kupoteza nywele (Alopecia).
B) Dalili Za Ugonjwa Wa Kaswende Kwa Mwanamke.
1) Kidonda kwenye sehemu za siri (uke), mdomo au makalio. Kidonda hiki hujulikana kama chancre.
2) Vipele kwenye viganja vya mikono na nyayo za miguu ambavyo ni vyekundu au vyekundu-kahawia.
3) Maumivu ya kichwa na mwili.
4) Uchovu.
5) Homa.
6) Kupoteza nywele (Alopecia).
Kumbuka: Hatua za baadaye za ugonjwa wa kaswende huendelea polepole ndani ya miaka, na huathiri moyo, ubongo na sehemu nyingine za mwili. Hii inaweza kusababisha dalili tofauti, kama vile: Kuishiwa pumzi, kuchanganyikiwa, kusahau, kupoteza uratibu, uharibifu wa neva na vinginevyo.
Jinsi Ya Kupima Kaswende:
Vipimo vya ugonjwa wa kaswende hufanywa kulingana na dalili, hii inahusisha uchunguzi wa kimwili na vipimo vya damu kwa uwepo wa protini dhidi ya kaswende. Utambulizi wa ugonjwa wa kaswende mara nyingi hufanywa wakati wa uchunguzi wa kawaida, kwa sababu kaswende inaweza isisababishe dalili zozote, au dalili zisizo za kawaida.
Kama kuna kidonda, sampuli ya majimaji kutoka kwenye kidonda huweza pia kuchunguzwa kwa uwepo wa bakteria. Hamna kipimo kimoja cha kutambua magonjwa yote ya zinaa. Tafadhali ongea na mtaalamu wa afya kwa taarifa zaidi.
Dawa Ya Kaswende:
Kaswende hutibiwa kwa antibiotiki, Penisilini ya Benzathine (Benzathine penicillin) ndiyo chaguo la kwanza la tiba kwa hatua zote za kaswende. Machaguo mengine, haswa ikiwa mtu aliyeathirika ana mzio (Allergy) wa penisilini, ni doxycycline na ceftriaxone. Penisilini ya Benzathine kwa kawaida ni sindano inayochomwa kwenye misuli (Intramuscularly), wakati doxycycline na ceftriaxone kwa kawaida huchomwa kwenye mishipa ya damu (Intravenously) au misuli (Intramuscularly). Dawa zote tatu hutolewa kwa dozi kubwa, kwa siku moja au siku kadhaa mfululizo. Penisilini ya Benzathine inaweza kutolewa katika dozi tofauti, kulingana na hatua iliyofikia kaswende inayotibiwa.
Madhara Ya Kaswende:
Yafuatayo ni madhara yanayoweza kutokea ikiwa mgonjwa mwenye kaswende hatopata matibabu haraka;
A) Madhara Ya Kaswende Kwa Mwanaume.
1) Matatizo ya kuona, upofu (Visual problems, blindness).
2) Kupoteza kusikia (Hearing loss).
3) Uharibifu wa neva (Nerves damage).
4) Dementia.
5) Kupoteza uwezo wa kusimamisha uume (Sexual dysfunction).
6) Matatizo ya moyo na mishipa (Heart problems).
7) Kiharusi (stroke).
8) Kuumwa kichwa (Headache).
9) Kupoteza maumivu na hisia za joto (loss of pain and temperature sensation).
B) Madhara Ya Kaswende Kwa Mwanamke.
1) Matatizo ya kuona, upofu (visual problems, blindness).
2) Kupoteza kusikia (Hearing loss).
3) Uharibifu wa neva (Nerves damage).
4) Dementia.
5) Kupoteza maumivu na hisia za joto (loss of pain and temperature sensation).
6) Matatizo ya moyo na mishipa (Heart problems).
7) Kiharusi (stroke).
8) Kuumwa kichwa (Headache).
Kumbuka: Kaswende inaweza kusababisha madhara kwa mwili ikiwa haitatibiwa. Kaswende huongeza uwezekano wa kuambukizwa VVU na inaweza kuleta matatizo wakati wa ujauzito. Matibabu inaweza kusaidia kuzuia madhara ya baadaye, lakini haiwezi kuponya au kubadilisha uharibifu uliopo.
HITIMISHO:
Kwa msaada wa ushauri, vipimo na tiba ya magonjwa ya afya ya uzazi wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487.
Lakini pia, kwa uhitaji wa updates, vitabu (e-books) bure kuhusu afya jisajili (subscribe) kupitia email yangu kwa kubonyeza hii link: https://isayafebu.beehiiv.com/subscribe
2 Comments