Kisukari: Ujue Ugonjwa Wa Kisukari Na Jinsi Ya Kujikinga.

Ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa unaotokana na mtu kuwa na kiwango cha sukari nyingi kupita kiasi kwenye damu kwa muda mrefu. Ugonjwa huu huvuruga utaratibu wa kuingiza sukari ndani ya chembechembe hai kutoka kwenye damu kwa kuwa chembechembe hai uhitaji sukari ili kutengeneza nishati mwilini.

Ugonjwa wa Kisukari hujulikana kwa kitaalamu kama Diabetes Mellitus.

Kisukari ikiwa ni moja ya muuaji wa kimya kimya katika kundi la magonjwa yasiyo ya kuambukiza. Watu milioni 285 duniani kote wameathiriwa na kisukari ambayo ni sawa na asilimia 6.6 ya idadi ya watu wote ulimwenguni pia ikishika nafasi ya 5 kwa kusababisha vifo duniani.

Ugonjwa wa kisukari husababishwa na nini?

Ugonjwa wa Kisukari hutokea pale ambapo tezi ya kongosho inaposhindwa kutengeneza kichocheo (Homoni) aina ya insulin au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho na kusababisha kuongezeka kwa sukari (Hyperglycemia) au kushuka kwa kiwango cha sukari (Hypoglycemia). Ugonjwa wa kisukari unaweza kusababishwa na kuwa na kiwango kidogo cha insulin mwilini, mwili kutosikia kichocheo hicho au yote mawili.

Aina Za Ugonjwa Wa Kisukari:

Kuna aina kuu mbili za ugonjwa wa kisukari ambazo ni pamoja na;

1) Kisukari Kinachotegemea Insulini/Kisukari Aina Ya Kwanza.

Aina hii ya kisukari husababishwa na upungufu au ukosefu wa kichocheo kinachotengenezwa kwenye kongosho kinachoitwa insulini.

Aina hii ya kisukari hujulikana kwa kitaalamu kama Insulin Dependent Diabetes Mellitus (IDDM) au Type 1 Diabetes Mellitus.

Aina hii ya kisukari hudhibitiwa kwa kutumia sindano ya insulin kwani mwili huwa unashindwa kutengeneza kichocheo hiki, pamoja na kurekebisha ulaji. Mara nyingi aina hii ya kisukari huwapata watu wenye umri mdogo (watoto na vijana). Vilevile mtu hawezi kurithi iwapo kuna historia ya kisukari katika familia.

2) Kisukari Kisichotegemea Insulini/Kisukari Aina Ya Pili.

Aina hii ya kisukari husababishwa na mwili kushindwa kutumia sukari. Mwili wa mtu mwenye aina hii ya sukari huweza kutengeneza insulini ya kutosha lakini haitumiki kuuwezesha mwili kutumia sukari na hivyo sukari katika damu huwa katika kiwango cha juu. 

Aina hii ya kisukari hujulikana kwa kitaalamu kama Non-Insulin Dependent Diabetes Mellitus (NIDDM) au Type 2 Diabetes Mellitus. 

Aina hii ya kisukari huweza kudhibitiwa kwa kutumia vidonge pamoja na kurekebisha ulaji; au kwa kurekebisha ulaji pekee. Mara nyingi huwapata watu wenye umri mkubwa kuanzia miaka 40 na kuendelea.

Kumbuka:

a) Ufanisi wa tiba ya aina zote za kisukari hutegemea sana ulaji unaozingatia masharti yatolewayo na mtoa huduma za afya.

b) Muonekano wa mgonjwa wa kisukari kinachotegemea insulin mara nyingi huwa ni mwembamba wakati Yule mwenye kisukari kisichotegemea insulin huwa mnene.

Mambo Yanayoongeza Uwezekano Wa Kupata Ugonjwa Wa Kisukari:

Yafuatayo ni mambo yanayomuweka mtu katika hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari ambayo ni pamoja na;

1) Uzito uliozidi (overweight) au unene uliokithiri (obesity).

2) Kutofanya mazoezi.

3) Ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi.

4) Kuwa na shinikizo kubwa la damu.

5) Matumizi ya sigara na bidhaa nyingine za tumbaku.

6) Kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40.

7) Historia ya kuwa na kisukari katika familia.

Dalili Za Ugonjwa Wa Kisukari:

Zifuatazo ni dalili za ugonjwa wa kisukari ambazo ni pamoja na;

1) Kukojoa mara kwa mara.

2) Kusikia kiu sana.

3) Kusikia njaa sana.

4) Kuchoka sana na kukosa nguvu bila kufanya kazi.

5) Kupungua uzito bila kukusudia.

6) Kusikia kizunguzungu.

7) Kutoona sawa.

8) Kuwa na maambukizi ya ngozi na vidonda visivyopona upesi.

9) Baadhi ya viungo vya mwili kama vile vidole vya miguu na mikono kufa ganzi.

Soma pia hii makala: Uti Kwa Wanawake: Zijue Sababu 3 Zinazopelekea Kuugua Uti, Tiba Mbadala Na Kinga.

Utambuzi wa Ugonjwa wa kisukari:

Utambuzi wa ugonjwa wa kisukari hufanywa kulingana na dalili na kupima kiwango cha sukari kwenye damu. Ikiwa bado haitambuliki kama mtu ana ugonjwa wa kisukari, utambuzi unaweza kuthibitishwa kwa kipimo cha ustahimilivu wa glukosi (glucose tolerance test). Katika kipimo hiki, mtu humeza kiasi fulani cha glukosi. Halafu kiwango cha sukari kwenye damu hupimwa baada ya muda ili kuona ikiwa mwili unatumia glukosi namna ipasavyo.

Dawa Ya Ugonjwa Wa Kisukari:

Matibabu ya kisukari kisichotegemea insulini hulenga kuwa na kiwango cha sukari katika damu ambacho ni salama kiafya. Hii hulenga kuboresha athari ya insulini kwenye mwili na kuzuia madhara ya ugonjwa wa kisukari.

Hatua za kwanza za matibabu hujumuisha kuongeza kufanya mazoezi na kuboresha lishe. Kuwa na uzito mzuri kiafya ni muhimu. Hata hivyo, baada ya muda, dawa huweza kuhitajika kupunguza kiwango cha sukari kwenye damu.

Kadiri ugonjwa unavyoendelea, mtu aliyeathirika anaweza kuhitaji kufundishwa jinsi ya kufanya baadhi ya mambo kama vile kuchunguza wenyewe viwango vyao vya sukari. Wataalamu wa afya huweza kutoa maelezo na kusaidia katika hatua zote za matibabu.

Ufuatiliaji wa mara kwa mara ni muhimu. Ufuatiliaji unaweza kusaidia kutambua na kutibu madhara yanayosababishwa na kisukari.

Madhara Ya Ugonjwa Wa Kisukari:

Ugonjwa wa kiskari usipodhibitiwa huleta madhara mbalimbali mwilini. Madhara haya huwa makubwa zaidi hasa pale mgonjwa anapokua hazingatii masharti ya matibabu na ulaji bora.

Kuna madhara ya muda mfupi na muda mrefu.

Kushuka kwa kiwango cha sukari katika damu.

Hali hii hutokea pale ambapo sukari hushuka kuliko kawaida. Hii inaweza kutokana na kutumia dawa kuzidi kipimo, kunywa pombe, kufanya mazoezi bila kula na kutokula kwa muda mrefu.

Dalili za kushuka kwa kiwango cha sukari katika damu ni pamoja na;

1) Moyo kwenda mbio.

2) Mwili kutetemeka.

3) Kusikia njaa.

4) Kusikia kizunguzungu.

5) Kuchanganyikiwa.

6) Kutokwa jasho kwa wingi.

7) Kuchoka sana.

Hali hii ikizidi mgonjwa huweza kupoteza fahamu na hatimaye kupoteza maisha kama hatapata matibabu mapema.

mapema.Kama mgonjwa akipatwa na hali hii asipewe kitu chenye sukari, ikiwemo glukosi, soda au juisi.

Kumbuka:

a) Mgonjwa aliyepoteza fahamu asipewe kinywaji au chakula.

b) Anaweza kuwekewa glukosi kidogo kati ya shavu na fizi.

c) Awahishwe katika kituo cha huduma za afya haraka iwezekanavyo.

Kupanda kwa kiwango cha sukari katika damu.

Hali hii hutokea pale kiwango cha sukari kinapokuwa juu kuliko kawaida. Hii inaweza kutokea wakati mgonjwa anapoacha kutumia dawa, asipotunza dawa vizuri, asipotumia dawa kwa usahihi, anapoacha kufuata masharti ya ulaji unaotakiwa, anapopata maambukizi au maradhi mfano malaria, flu, nimonia nk.

Dalili za kupanda kwa kiwango cha sukari katika damu ni pamoja na;

1) Kupumua kwa haraka.

2) Kukojoa mara kwa mara hasa wakati wa siku.

3) Kutoona vizuri.

4) Kuongezeka mapigo ya moyo au moyo kwenda mbio.

5) Kuchanganyikiwa.

6) Kupungukiwa na maji mwilini. 

7) Kupoteza fahamu na hatimaye kupoteza maisha kama mgonjwa hatapata matibabu mapema.

8) Kizunguzungu. 

9) Kuwa na kiu au kukauka koo.

Kumbuka: Mgonjwa aliyepoteza fahamu asipewe chochote bali awahishwe katika kituo cha kutoa huduma za afya haraka sana.

Madhara ya muda mrefu ya ugonjwa wa kisukari. 

Madhara ya muda mrefu yatokanayo na ugonjwa wa kisukari ni pamoja na;

1) Upofu.

2) Maradhi ya moyo.

3) Maradhi ya figo.

4) Vidonda kutopona upesi na hatari ya kukatwa mguu.

5) Kufa ganzi na kupoteza hisia za mikono na miguu.

6) Kiharusi (stroke).

Jinsi Ya Kuepuka Ugonjwa Wa Kisukari:

Yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia ili kujikinga na ugonjwa wa kisukari;

1) Kula mlo kamili angalau mara tatu kwa siku.

2) Epuka kula chakula kingi kupita kiasi.

3) Epuka kula chakula chenye mafuta mengi au sukari nyingi.

4) Fanya mazoezi ya mwili mara kwa mara.

5) Pima sukari katika damu mara kwa mara, angalau mara moja kwa mwaka.

6) Epuka matumizi ya pombe za aina zote.

7) Epuka matumizi ya sigara , bidhaa nyingine za tumbaku na madawa ya kulevya.

Jinsi Ya Kuishi Na Ugonjwa Wa Kisukari:

Ili kuishi na ugonjwa wa kisukari, mgonjwa anashauriwa kufanya mambo yafuatayo;

a) Dhibiti Ulaji Wako.

1) Kula mlo kamili uliotayarishwa kutokana na angalau chakula kimoja kutoka katika kila kundi la vyakula.

2) Kula vyakula vya nafaka kama ulezi, mtama, uwele, ma nafaka zisizokoboewa kwa mfano dona, ngano, au shairi.

3) Kula mboga mboga kwa wingi kwa mfano mchicha, matembele, karoti, majani ya maboga, kisamvu, mlenda nk.

4) Kula kiasi kidogo cha vyakula vya nafaka, mizizi na ndizi katika mlo.

5) Kula vyakula vya jamii ya kunde kama mboga (sehemu ya mlo) kwa mfano maharagwe, njegere, mbaazi, kunde, choroko, nk.

6) Kula matunda kwa kiasi mfano ndizi au chungwa moja au kipande cha papai au embe kubwa katika kila mlo.

7) Kunywa maji kwa wingi.

8) Epuka ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi kama jamu, asali, chokoleti, pipi, bazooka, aiskrimu, na juisi bandia.

9) Epuka ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi.

10) Epuka unywaji wa pombe.

b) Fanya Mazoezi Mara Kwa Mara Angalau Nusu Saa Kwa Siku.

c) Tunza Miguu Yako Kwa Makini.

1) Epuka kuvaa viatu au soksi zinazo bana.

2) Epuka kuvaa viatu vyenye kisigino kirefu ambacho huweza kusababisha kuanguka na kuumia.

3) Osha miguu yako kwa maji safi na kausha vizuri hususan katikati ya vidole.

4) Usitembee bila kuvaa viatu.

5) Vaa viatu vya wazi na vyenye kisigino kifupi.

6) Epuka kijiumiza, na unapokua na kidonda tibu mapema.

d) Epuka Msongo Wa Mawazo.

1) Zingatia afya ya kinywa kwa kupiga mswaki angalau mara mbili kwa siku.

2) Usafi wa mwili.

3) Taarifa na elimu kuhusu kisukari.

4) Masharti ya dawa na ulaji.

5) Kuhudhulia kliniki kama inavyoshauriwa.

6) Kumuona daktari mapema mara unapopata tatizo lolote la kiafya.

HITIMISHO:

Kisukari kinachotegemea insulini hakiwezi kupona. Hata hivyo, kwa usaidizi na elimu, watu wengi hujifunza kumudu viwango vyao vya sukari kwenye damu. Watu wasiodhibiti viwango vyao vya sukari huweza kupata madhara zaidi. Madhara haya hujumuisha kupoteza uwezo wa kuona, uharibifu wa neva kwenye mikono na miguu pamoja na ugonjwa wa moyo.

By the way, hivi unajua kwamba virutubisho vifuatavyo: Provitality, Neolife shake, na Botanical Balance vitakusaidia kudhibiti kiwango kikubwa cha sukari mwilini?. Ndio ni kweli kupata virutubisho hivi tuma ujumbe sasa hivi kwenda 0625 305 487.

Kwanini mtu mwenye kisukari, kidonda chake hakiponi haraka?

Kuna sababu kuu mbili za kisukari kuchelewesha kupona kwa vidonda:
KWANZA: Viwango vya juu vya sukari kwenye damu.
Viwango vya sukari kwenye damu vikiwa juu, vinaweza kuharibu mishipa ya damu na neva mwilini. Hii inaweza kusababisha mzunguko wa damu kuwa mbovu kwenye viungo, hasa kwenye miguu na vidole. Mzunguko mbovu wa damu unamaanisha kuwa majeraha hayatapata oksijeni na virutubisho vinavyohitajika kupona vizuri.

Vilevile, viwango vya juu vya sukari kwenye damu vinaweza pia kudhoofisha mfumo wa kinga, na hivyo kufanya iwe vigumu kwa mwili kupambana na maambukizi.

PILI: Mfumo dhaifu wa kinga ya mwili.

Kisukari kinaweza kudhoofisha mfumo wa kinga ya mwili, na hivyo kufanya iwe vigumu zaidi kupambana na bakteria ambao husababisha maambukizi kwenye majeraha.

Udhaifu wa kinga unatokana na mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na viwango vya juu vya sukari kwenye damu huweza kuathiri utendaji wa seli nyeupe za damu.

HIVYO: Ukiwa na kisukari, ni muhimu kuwa mwangalifu zaidi kuhusu kuangalia miguu yako. Chunguza kama una michubuko, au vidonda. Hata jeraha ndogo linaweza kuwa tatizo kubwa.