Mambo 6 Muhimu Usiyo yajua Kuhusu Kuziba Kwa Mirija Ya Uzazi Kwa Wanawake.

Kuziba kwa mirija ya uzazi ni hali ya kujaa maji kwenye mirija ya uzazi (fallopian tubes) ambako kunazuia yai kusafiri kutoka kwenye mifuko ya mayai (ovaries) kwenda kwenye mji wa mimba (uterus), maji haya kwenye mirija ya uzazi hulizuia yai lisiweze kupata mbegu za kiume za kulirutubisha na hivyo kumfanya mwanamke asipate ujauzito. Kuziba kwa mirija ya uzazi hujulikana kwa kitaalamu kama “Hydrosalpinx”.

Asilimia 20% mpaka 30% ya kesi za ugumba kwa wanawake (infertility cases)  zinahusiana na mirija ya uzazi (tubal factor infertility). Tatizo la kuziba kwa mirija ya uzazi linachangia asilimia 10% mpaka 20% kwenye changamoto za ugumba kwa wanawake.

hydrosalpinx

Sababu Za Mirija Ya Uzazi Kuziba:

Kisababishi kikubwa cha kuziba kwa mirija ya uzazi ni tatizo la maambukizi kwenye via vya uzazi ambalo hujulikana kwa kitaalamu kama Pelvic inflammatory Disease (PID). PID mara nyingi husababishwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama vile kisonono (gonorrhea) na pangusa (chlamydia).

Sababu zingine zinazoweza kupelekea kuziba kwa mirija ya uzazi ni pamoja na; Magonjwa ya zinaa kama vile pangusa (chlamydia), kisonono (gonorrhea), michubuko au majeraha kwenye mirija ya uzazi kutokana na upasuaji, mimba kutunga nje ya kizazi (ectopic pregnancy) na kusababisha upasuaji hali ambayo hupelekea michubuko, hali ya kukua kwa uvimbe aina ya fibroid ambayo hupelekea kuziba nafasi ya mirija ya uzazi, mkusanyiko wa usaha au uchafu kutokana na maambukizi ya magonjwa kwenye mirija ya uzazi.

Soma pia hizi makala:

Dalili Za Kuziba Kwa Mirija Ya Uzazi:

Kuziba kwa mirija ya uzazi ni hali ambayo huonyesha dalili zake kwa nadra sana. Wanawake wengi hushindwa hata kutambua kuwa wana tatizo la kuziba kwa mirija ya uzazi mpaka pale wanapokuwa wakijaribu kutafuta ujauzito bila mafanikio. Hata hivyo kwa baadhi ya wanawake hali hii inaweza kuonyesha dalili zifuatazo;

1) Maumivu makali wakati wa hedhi.

2) Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa.

3) Maumivu wakati wa kukojoa.

4) Kutokwa na uchafu ukeni.

5) Mirija ya uzazi kuvimba na kujaa maji.

6) Maumivu makali chini ya kitovu.

7) Maumivu ya nyonga.

Kumbuka: Hali ya kuziba kwa mirija ya uzazi kwa kawaida huwa haiathiri vipindi vya hedhi wala mzunguko wa hedhi zaidi ya kujitokeza baadhi ya maumivu au kukosa furaha.  Hata kama mirija yote miwili ikiwa imeziba haiwezi kuathiri vipindi vya hedhi. Hata hivyo, magonjwa ambayo husababisha mirija ya uzazi kuziba yanaweza kuathiri vifuko vya mayai pamoja na ukuta wa mfuko wa kizazi, na kwa hali hii, vipindi vya hedhi lazima vibadirike badirike au kutokwa na damu nyingi sana wakati wa hedhi.

Uchunguzi Na Vipimo Vya Kuziba Kwa Mirija Ya Uzazi:

Ikiwa unasumbuliwa na tatizo la kuziba kwa mirija ya uzazi unashauriwa uende hospitali ambako utafanyiwa uchunguzi na vipimo vifuatavyo;

1) Ultrasound.

Ikiwa mirija ya uzazi imevimba kutokana na kujaa maji, kipimo hiki  kitaonyesha  ukubwa wa mirija ya uzazi kuliko kawaida na  kuna muda mwingine mirija ya uzazi itaonekana kufanana na umbo la soseji (shaped like sausage) ambapo mtaalam wa afya itambidi afanye vipimo vingine ili kubaini kisababishi cha kujaa maji kwenye mirija ya uzazi.

2) Hysterosalpingogram (HSG).

Hiki ndio kipimo kinachotumika kubaini (diagnose) tatizo la kuziba kwa mirija ya uzazi ambacho hutumia dai ya mionzi (x-ray dye) ambapo mtaalam wa afya ataingiza dai kwenye mji wako wa mimba (uterus) na kuangalia mzunguko wa dai kupitia mionzi (x-rays). Kama dai itatoka nje ya mirija yako ya uzazi na kuingia kwenye uwazi wa pelivisi (pelvic cavity) ni dhahiri kuwa mirija yako ya uzazi iko wazi, lakini kama dai itaacha kuzunguka basi ni dhahiri kuwa mirija yako ya uzazi imeziba.

Hysterosalpingogram

3) Laparoscopy.

Huu ni upasuaji mdogo unaomruhusu mtaalam wa afya kuangalia ndani ya uwazi wako wa tumbo (abdominal cavity) ambapo mtaalam wa afya hukata kidogo tumbo (tiny cuts) na kuingiza kifaa kiitwacho laparoscope ndani ya tumbo na kuangalia kwa karibu mirija yako ya uzazi. Muda mwingine mtaalam wa afya huingiza catheter kwenye uke (vagina) na shingo ya kizazi (cervix) ili kusukuma dai kuelekea kwenye mji wako wa mimba (uterus) na mirija yako ya uzazi (fallopian tube) kwa lengo la kubaini tatizo la kuziba kwa mirija ya uzazi. Mara nyingi  hiki kipimo ndio hutumika kuthibitisha (confirm) matokeo ya kipimo cha Hysterosalpingogram.

laparoscopy

Tiba Ya Kuziba Kwa Mirija Ya Uzazi:

Kutibu tatizo la kuziba kwa mirija ya uzazi kunaongeza uwezekano wa mwanamke kushika ujauzito. Matibabu hayo yatategemea vitu kama umri wako (age) na kiwango cha uharibifu uliotokea kwenye mirija ya uzazi (severity of blockage). Pia kama una maambukizi kwenye mirija yako ya uzazi daktari atakuandikia dawa za kutumia (antibiotics) kutibu maambukizi hayo.

Matibabu mengine yanayofanyika kwa mgonjwa mwenye tatizo la kuziba kwa mirija ya uzazi ni pamoja na;

 1) Salpingectomy.

Matibabu haya yanahusisha uondoaji wa mrija mmoja wa uzazi ulioathirika (unilateral salpingectomy) au uondoaji wa mirija yote miwili iliyoathirika (bilateral salpingectomy).

2) Salpingostomy.

Matibabu haya yanahusisha urekebishaji wa  mirija ya uzazi iliyoathirika (repair the blockage in your tubes).

Vyakula Vinavyosafisha Mirija Ya Uzazi:

Kumbuka: Japo watu wengi wanasifia njia hizi kuwasaidia kuzibua mirija ya uzazi kwa kupunguza uvimbe kwenye mirija, bado hakuna utafiti wa kisayansi unaohakiki uwezo wa tiba hizi asili. Lakini usiogope kujaribu, bahati inaweza kuwa upande wako ukashika mimba mwaka huu.

1.Vitamin C.

Vitamin C ni kiondoa sumu ambacho kinapunguza mpambano (inflammation) ndani ya mwili na pia kinaimarisha kinga yako. Kwa sababu hizi pekee, vitamin C inasemekana kuwa na uwezo wa kutibu makovu na hivo kusaidia mirija yako kuzibuka.

Vitamin C inapatikana kwa wingi kwenye matunda yenye uchachu kama limau na machungwa. Lakini pia waweza kupata kwenye matunda mengine kama kiwi papai na mboga ya broccoli.

Shirika la afya duniani linapendekeza upate vitamin C kutoka kwenye vyakula zaidi, japo kuna virutubishi pia waweza kutumia vilivyo katika mfumo wa vidonge. Kumbuka kuwa mwili hauwezi kuhifadhi vitamin C, hivo watakiwa kuipata kutoka kwenye chakula au virutubishi kila siku.

vitamin C foods

2.Binzari Ya Manjano (Tumeric).

Binzari ya manjano inafanana sana na tangawizi. Ni moja ya chakula kikubwa katika kupunguza mpambano na kuvimba ndani ya mwili (anti-inflammatory). Kiambata hai cha Curmin ndani ya binzari ya manjano ndicho hufanya kazi ya kuzuia mpambano huo.

Hakuna madhara yoyote ya kutumia binzari ya manjano. Japo unashauriwa kutumia kujiko kimoja tu cha binzari ya manjano kwa siku, kwa kutengeneza kama chai na kuweka na viungo vingine.

Pamoja na faida nyingi za binzari ya manjano kiafya, lakini bado hakuna tafiti za kina juu ya uwezo wake katika kuzibua mirija ya uzazi.

tumeric

3.Tangawizi.

Kiambata hai cha gingerol kilichopo wenye tangawizi kinasaidia kupunguza mpambano na kuvimba kwenye mwili. Pamoja na faida hii hakuna utafiti wa moja kwa moja juu ya uwezo wake katika kuzibua mirija ya uzazi.

tangawizi

4.Kitunguu Swaumu.

Kitunguu swaumu kinafahamika kwa kuimarisha kinga ya mwili, kuzibua mirija ya uzazi na kutibu maambukizi ya bakteria na fangasi. Menza punye tano za kitunguu swaumu kila siku kufurahia uponyaji wake.

kitunguu saumu

5.Dong Quai (Female Ginseng).

Ni mmea unaopatikana zaidi barani Asia. Unafahamika kwenye kutibu changamoto mbalimbali za uzazi ikiwemo kuzibua mirija ya uzazi. Ni moja ya tiba maarufu sana kwenye tiba asili za watu wa China.

ginseng

6.Maca.

Maca ni mmea unaopatikana hasa Marekani ya kusini. Mmea huu unasemakana kuwa tiba ya uzazi wa mwanamke kwa kuimarisha uwezo wa kushika mimba. Tafiti zinasema mmea wa maca pia unasaidia kuongeza uzalishaji wa mbegu za kiume. Bado hakuna utafiti wa kisayansi kuhusu uwezo wa maca kuzibua mirija.

maca plant

Madhara Ya Kuziba Kwa Mirija Ya Uzazi:

Ikiwa tatizo la kuziba kwa mirija ya kuzazi halitafanyiwa matibabu haraka basi litapunguza uwezekano wa mwanamke kushika ujauzito.

Kushindwa kutibu tatizo la kuziba kwa mirija ya uzazi pia kunaongeza hatari ya mimba kutoka (miscarriage) na mimba kutunga nje ya kizazi (ectopic pregnancy).

Jinsi Ya Kuzuia Kuziba Kwa Mirija Ya Uzazi:

Njia ya kuepuka kuziba kwa mirija ya uzazi ni kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya zinaa (STI’s) ambayo ndio huchangia kwa kiasi kikubwa tatizo la kuziba kwa mrija ya uzazi. Kufanya ngono ilyosalama (practising safe sex) kunapunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya zinaa ambayo huchangia kwa kiasi kikubwa kuleta uharibifu kwenye viungo vya uzazi (reproductive organs).

HITIMISHO:

Mirija ya uzazi inapoziba huzuia mwanamke asipate ujauzito kwa kuwa huzizuia mbegu za mwanaume zisiweze kulifikia yai la mwanamke, na vile vile hulizuia yai lililorutubishwa lisiweze kufika kwenye mji wa mimba. Upasuaji unaweza ukafanyika ili kuondoa hali ya kuziba, lakini njia hii ya tiba sio ya maana sana kwakuwa inaweza ikasababisha mimba kutunga nje ya kizazi (ectopic pregnancy). Yafaa sana ukapata virutubisho vilivyotokana na mimea na matunda ili kuondoa kabisa vyanzo au visababishi vya kuziba kwa mirija ya uzazi na kukuwezesha kupata ujauzito. Ikiwa unasumbuliwa na tatizo hili, tafadhali wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487 kupata virutubisho vyenye uwezo wa kuondoa vyanzo vya tatizo hili kwa gharama nafuu, navyo ni pamoja na; FEMININE HERBAL, CRUCIFEROUS, GARLIC ALLIUM COMPLEX, CHELATED ZINC, TRE EN EN, na VITAMIN E.

vipimo vya mfumo wa uzazi