Uti Kwa Wanawake: Zijue Sababu 3 Zinazopelekea Kuugua Uti, Tiba Mbadala Na Jinsi Ya Kujikinga.

Uti kwa wanawake ni maambukizi ya mfumo wa mkojo kwa wanawake ambao huhusisha figo (kidney), kibofu cha mkojo (urinary  bladder), mrija wa mkojo kutoka kwenye kibofu cha mkojo (urethra) pamoja na mrija unao unganisha figo na kibofu cha mkojo (ureter).

Maambukizi haya kwa kiasi kikubwa husababishwa na bakteria jamii ya E. coli, lakini katika mazingira machache fangasi na virusi wanaweza kuwa chanzo cha maambukizi haya.

Mfumo Wa Mkojo Wa Mwanamke:

mfumo wa mkojo kwa mwanamke / Uti Kwa Wanawake

Aina Za UTI Kwa Wanawake.

Zifuatazo ni aina mbili za u.t.i kwa wanawake ambazo ni;

1. Lower U.T.I.

Hii ni hatua ya ugonjwa kushambulia maeneo ya urethra na kibofu cha mkojo ambapo katika hatua hii, mgonjwa atakuwa na dalili zifuatazo:Maumivu wakati wa kukojoa, kujiskia kukojoa mara kwa mara lakini kutoa mkojo kidogo tu (polyuria), damu katika mkojo (hematuria), maumivu ya kiuno kwa wanawake, kukojoa mkojo wenye harufu kali.

2. Upper U.T.I.

Haya ni maambukizi ya ndani ya figo.Hii ni hatua mbaya sana endapo bakteria wataanza kuingia kwenye mfumo wa damu kutoka kwenye figo (sepsis). Sepsis huweza kusababisha msukumo wa damu kuwa mdogo sana (low blood pressure), mshituko au kifo. Katika hatua hii, mgonjwa atakuwa na dalili zifuatazo: Maumivu ya maeneo juu ya mgongo, homa, kutapika, kichefuchefu.

Chanzo Cha U.t.i Kwa Wanawake:

U.t.i husababishwa na bakteria waitwao Escherichia coli (E.coli), bakteria hawa wanapoingia mwilini huenda kuathiri mfumo wa mkojo.

Mambo yafuatayo yanaweza kumuweka mwanamke kwenye hatari ya kupata U.t.i;

  • Kinga ya mwili kutokuwa imara (immunosuppresion).
  • Kutumia vifaa au dawa za kuzuia mimba.
  • Kupungua kwa homoni ya estrogen.
  • Ugonjwa wa kisukari.
  • Kutumia choo kichafu.
  • Kufanya ngono isiyo salama (unprotected sexual intercourse).
  • Mimba (Pregnancy).

Sababu Za U.t.i Kwa Mwanamke:

Mwanamake huwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kuugua ugonjwa huu pamoja na kujirudia mara kwa mara kwa kuwa mrija wa mkojo huwa ni mfupi sana tofauti na mwanaume, pia tundu la uke huwa karibu na sehemu ya haja kubwa hivyo ni rahisi kwa bakteria kutoka kwenye choo kuingia ukeni.

Pia, matumizi ya baadhi ya njia za uzazi wa mpango, kemikali kali kusafishia via vya uzazi, kufikia umri wa ukomo wa hedhi pamoja na ujauzito ambao hubana kibofu cha mkojo na kupunguza ufanisi wake kwenye kutoa mkojo wote huwa ni baadhi ya sababu zinazoongeza uwezekano wa mwanamke kuugua ugonjwa huu kuliko mwanaume.

Dalili Za UTI kwa wanawake:

Zifuatazo ni baadhi ya dalili za u.t.i kwa wanawake ambazo ni pamoja na;

a) Kupatwa na maumivu yanayochoma wakati wa haja ndogo.

b) Kujisaidia haja ndogo mara kwa mara isiyotoa mkojo mwingi.

c) Kujisaidia mkojo mweusi au ulio na chembechembe za damu na harufu kali.

d) Maumivu ya nyonga.

e) Uchovu, Homa na kutapika.

f) Maumivu ya sehemu ya chini ya tumbo.

Soma pia hizi makala:

Dawa Za Asili Za U.t.i:

Zifuatazo ni dawa za asili 10 zinazotibu u.t.i ambazo unaweza kuzitumia uwapo katika mazingira yako ya nyumbani ambazo ni;

1) Baking Soda.

U.t.i ambayo imedumu zaidi ya siku 2 inahitaji kuripotiwa kwa daktari. U.t.i isiyotibiwa mapema inaweza kupelekea matatizo zaidi kwenye figo. Ili kuzuia u.t.i isijiimarishe zaidi jaribu kutumia baking soda.

baking soda

Jinsi ya kutumia Baking soda kutibu u.t.i;

Chukua kijiko kimoja cha chai cha baking soda weka kwenye glasi yenye maji na unywe mchanganyiko huo, hii itakusaidia kupunguza makali au kuendelea kwa maambukizi ya u.t.i.

Baking soda itapunguza hali ya uasidi (acidic medium) katika mkojo wako na kupelekea kupata nafuu haraka.

2) Maji Ya Kunywa.

Kama unasumbuliwa na u.t.i au inaonekana unapatwa na ugonjwa huu mara kwa mara (recurrent u.t.i), basi hakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku walau glasi 8 mpaka 10 kwa siku, unashauriwa kutumia maji yenye joto la kawaida yaani yale ambayo hayajawekwa kwenye friji. Mara nyingi mtu mwenye u.t.i huwa na upungufu wa maji mwilini na ikiwa mkojo wake utachunguzwa utaona ni wa rangi ya njano.

maji ya kunywa

Jinsi ya kutumia maji  kutibu UTI kwa wanawake;

Kunywa maji ya kutosha kila siku na  matokeo yake bakteria wote waliokupelekea upate u.t.i watalazimishwa kutoka nje ya mwili kupitia mkojo utakaoupata kutokana na kukojoa mara kwa mara kama matokeo ya kunywa maji mengi na utaona baada ya siku 4 mpaka 7 hata rangi ya mkojo inabadilika na kuwa mweupe kabisa.

3) Kitunguu Swaumu.

Kitunguu swaumu ni moja wapo ya tiba mbadala ya nguvu katika kutibu maambukizi kwenye njia ya mkojo. Ni dawa nzuri dhidi ya bakteria na virusi na hivyo moja kwa moja kuwa muhimu katika kutibu UTI kwa wanawake.

kitunguu saumu

Jinsi ya kutumia kitunguu swaumu kutibu u.t.i;

Chukua kitunguu saumu, menya punje 6 na kisha kikatekate (chop) vipande vidogo vidogo na kisha meza kama unavyomeza dawa na maji vikombe walau viwili kila unapoenda kulala kwa muda wa siku 7.

4) Limao/Ndimu.

Limao au ndimu  pia ni moja wapo ya tiba mbadala ya maambukizi katika njia ya mkojo ambayo unaweza kuitumia uwapo katika mazingira yako ya nyumbani.

limao/ndimu

Jinsi ya kutumia limao/ndimu kutibu u.t.i;

Weka vijiko vikubwa vitano vya juisi ya limao au juisi ya ndimu na uongeze maji ya vuguvugu ili kupata robo lita (250mls) na unywe kutwa mara 3. Pia unaweza kuongeza asali vijiko vikubwa vitatu ndani ya juisi ya limao/juisi ya ndimu ambapo mchanganyiko huo utakuondolea maumivu yatokanayo na u.t.i na hata kuzuia kutokwa na damu kwenye mkojo kama matokeo ya maambukizi katika njia ya mkojo hasa kwenye kibofu cha mkojo.

5) Vyakula Vyenye Vitamini C.

Vyakula vyenye vitamini c kwa wingi husaidia kuzuia uzalishwaji wa bakteria wabaya (pathogens) mwilini. Unashauriwa utumie mpaka mg 5,000 za vitamini C kwa siku ikiwa unasumbuliwa na maambukizi ya mara kwa mara kwenye njia ya mkojo.Ukiacha machungwa, vitamini c pia inapatikana kwa wingi katika juisi ya  ubuyu na kwenye mlonge. Hivyo hakiksha unatumia kiasi cha kutosha cha vitamini c kila siku ili kujikinga na hata kujitibu na u.t.i.

vitamin c foods

6) Nanasi.

Kula nanasi mara kwa mara ni mbinu nzuri kabisa katika kudhibiti maambukizi katika njia ya mkojo. Kwenye nanasi kuna kimeng’enya muhimu sana kijulikanacho kwa kitaalamu kama ’Bromelian’. Kula  walau vipande vitatu mpaka vitano vya nanasi kila siku kutakuweka mbali na ugonjwa huu wa u.t.i.

nanasi

7) Zabibu.

Ulaji wa zabibu mara kwa mara unasaidia kudhibiti bakteria ambapo unashauriwa  kutumia juisi ya zabibu glasi 2 mpaka 4 kwa siku mara kwa mara ili kujikinga na maambukizi katika njia ya mkojo.

zabibu

8) Unga Wa Majani Ya Mlonge.

Unga utokanao na majani ya mlonge pia ni moja wapo ya tiba mbadala  ya maambukizi katika njia ya mkojo  ambayo unaweza kuitumia uwapo katika  mazingira yako ya nyumbani.

unga wa majani ya mlonge

Jinsi ya kutumia unga wa majani ya mlonge kutibu u.t.i;

Weka kijiko kimoja cha unga wa majani ya mlonge kwenye kikombe kilichowekwa uji, au kwenye  glasi ilyowekwa juisi ya matunda uliyotengeneza mwenyewe au kwenye kikombe kilichowekwa maji ya vugu vugu, kisha kunywa mchanganyiko huo husika kutwa mara 3. Tumia walau kwa mwezi mmoja mpaka miezi mitatu, pia unashauriwa kutumia unga wa majani ya mlonge muda wote kama kinga ya mwili wako dhidi ya magonjwa.

9) Mshubiri (Aloe-Vera).

Mshubiri au aloevera pia ni moja wapo ya tiba mbadala ya maambukizi katika njia ya mkojo ambayo unaweza kuitumia uwapo katika mazingira yako ya nyumbani.

Aloevera

Jinsi ya kutumia mshubiri (Aloe-vera) kutibu u.t.i;

Chukua jeli ya mshubiri (Aloevera) vijiko vikubwa vinne changanya na maji ya kawaida ili kupata walau kikombe kimoja (250mls) au robo lita, changanya vizuri mchanganyiko huo na unywe mara kutwa mara 2 kwa siku 3 kwa muda wa wiki 2 au hadi utakapopona. Pia unaweza kuongeza asali ndani yake vijiko  vikubwa vitatu ili kupunguza ukali wa dawa hii.

10) Mchaichai.

Mchaichai pia unafaa sana kutibu maambukizi katika njia ya mkojo, tumia mchaichai uwapo katika mazingira yako ya nyumbani ikiwa unasumbuliwa na changamoto ya ugojwa wa u.t.i.

majani ya mchaichai

Jinsi ya kutumia mchaichai kutibu u.t.i;

Chukua majani ya mchaichai, yakate kate vipande vidogo vidogo halafu hivyo vipande viweke kwenye chupa ya chai. Chukua kipande cha tangawizi kiponde ponde halafu chemsha kwenye maji kiasi cha glasi moja au mbili. Maji hayo ya tangawizi yakishachemka yachuje.

Weka maji ya tangawizi yaliyochujwa kwenye chupa ambayo kuna mchaichai na funika kwa muda wa dakika 30.Dakika 30 zikishapita kunywa kikombe kimoja asubuhi na jioni kwa muda wa siku 5 mpaka siku 7. Hapo utakuwa umetibu tatizo la u.t.i.

Dawa Ya Uti Sugu Kwa Mwanamke:

By the way, hivi unajua kwamba virutubisho vifuatavyo: Garlic allium complex, Tre en en, na Chelated zinc vitakusaidia kutibu uti sugu?. Ndio ni kweli kupata virutubisho hivi bonyeza hapa 0625 305 487.

Madhara Ya UTI kwa wanawake:

Ugonjwa huu usipotibiwa vizuri unaweza kusababisha madhara yafuatayo;

a) Figo kushindwa kufanya kazi (kidney failure), hii ni hatari sana  na hutokana na bakteria kushambulia figo.

b) Magonjwa ya kibofu cha mkojo kama vile kibofu cha mkojo kuziba, kushindwa kukojoa hali ambayo hupelekea mgonjwa kukojoa kwa mrija (urinary catheterization).

c) Maumivu ya mgongo, kiuno na nyonga.

d) Kupoteza hamu ya tendo la ndoa.

e) Mimba kuharibika.

f) Kushindwa kubeba mimba.

Jinsi Ya Kujikinga Na UTI kwa wanawake:

Kuna baadhi ya njia zinazoweza kutumika kujikinga na tatizo la UTI ya kujirudia. Mfano wa njia hizo ni pamoja na;

a) Kunywa maji na vinywaji kwa wingi kila siku. Hii itakusaidia ukojoe mara kwa mara na kutoruhusu bakteria kujenga makazi kwenye njia ya mkojo.

b) Kutokuvaa nguo za ndani zinazobana sana. Badili pedi mara kwa mara uwapo hedhini.

c) Kuacha mazoea ya kuvaa nguo za ndani mbichi.

d) Kusafisha via vya uzazi kutoka mbele kwenda nyuma (frontal to back wiping) baada ya haja kubwa na wakati wa kuoga ili kuzuia bakteria wasiingie kwenye uke kutoka sehemu ya haja kubwa.

e) Kwenda haja ndogo (kukojoa) mara tu umalizapo tendo la kujamiiana. Hii itasaidia kutoruhusu bakteria kuingia na kujenga makazi kwenye njia ya mkojo.

f) Kuacha tabia ya kutunza mkojo kwa muda mrefu baada ya kuhisi haja ndogo. Mkojo ukikaa sana kwenye kibofu unaweza kuzalisha bakteria.

g) Epuka kujisafisha ukeni kupita kiasi (excessive vaginal douching), pia epuka kupulizia marashi ukeni, ama kutumia pedi zenye kemikali ya kukata harufu.

HITIMISHO:

Katika hizo dawa zote zilizotajwa hapo juu, unashauriwa utumie zote kwa pamoja ili kupata matokeo mazuri na kupona  kwa haraka nazo ni pamoja na; Maji ya kunywa, kitunguu saumu, limao, unga wa majani ya mlonge, mshubiri na mchai chai.

vipimo vya mfumo wa uzazi