Vyakula Vinavyofaa Kwa Mgonjwa Mwenye Kisukari.

Kisukari ni ugonjwa unaotokana na mtu kuwa na sukari nyingi kupita kiasi kwenye damu. Ugonjwa huo huvuruga utaratibu wa kuingiza sukari ndani ya chembe kutoka kwenye damu kwa kuwa chembe huhitaji sukari ili kupata nishati.

Ugonjwa wa Kisukari hujulikana kwa kitaalamu kama Diabetes Mellitus.

Kisukari ikiwa ni moja ya muuaji wa kimya kimya katika kundi  la magonjwa yasiyo ya kuambukiza. Watu milioni 285 duniani kote wameathiriwa na kisukari ambayo ni sawa na asilimia 6.6 ya idadi ya watu wote ulimwenguni pia ikishika nafasi ya 5 kwa kusababisha vifo duniani.

Soma pia hii makala: Soma Hii Kama Unataka Kutibu Ugonjwa Wa Kisukari Ndani Ya Siku 30.

Ugonjwa wa kisukari husababishwa na nini?

Ugonjwa wa Kisukari hutokea pale ambapo tezi ya kongosho inaposhindwa kutengeneza kichocheo (Homoni) aina ya insulin au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho na kusababisha kuongezeka kwa sukari (Hyperglycemia) au kushuka kwa kiwango cha sukari (Hypoglycemia). Ugonjwa wa kisukari unaweza kusababishwa na kuwa na kiwango kidogo cha insulin mwilini, mwili kutosikia kichocheo hicho au yote mawili.

Aina Za Kisukari:

Kuna aina kuu mbili za kisukari ambazo ni pamoja na;

1) Kisukari Aina Ya Kwanza.

Aina hii ya kisukari husababishwa na upungufu au ukosefu wa kichocheo kinachotengenezwa kwenye kongosho kinachoitwa insulini.

Aina hii ya kisukari hujulikana kwa kitaalamu kama Insulin Dependent Diabetes Mellitus (IDDM) au Type 1 Diabetes Mellitus.

Aina hii ya kisukari hudhibitiwa kwa kutumia sindano ya insulin kwani mwili huwa unashindwa kutengeneza kichocheo hiki, pamoja na kurekebisha ulaji. Mala nyingi aina hii ya kisukari huwapata watu wenye umri mdogo (watoto na vijana). Villevile mtu hawezi kurithi iwapo kuna historia ya kisukari katika familia.

2) Kisukari Aina Ya Pili.

Aina hii ya kisukari husababishwa na mwili kushindwa kutumia sukari. Mwili wa mtu mwenye aina hii ya sukari huweza kutengeneza insulini ya kutosha lakini haitumiki kuuwezesha mwili kutumia sukari na hivyo sukari katika damu huwa katika kiwango cha juu. 

Aina hii ya kisukari hujulikana kwa kitaalamu kama Non-Insulin Dependent Diabetes Mellitus (NIDDM) au Type 2 Diabetes Mellitus. 

Aina hii ya kisukari huweza kudhibitiwa kwa kutumia vidonge pamoja na kurekebisha ulaji; au kwa kurekebisha ulaji pekee. Mara nyingi huwapata watu wenye umri mkubwa kuanzia miaka 40 na kuendelea.

Kumbuka:

a) Ufanisi wa tiba ya aina zote za kisukari hutegemea sana ulaji unaozingatia masharti yatolewayo na mtoa huduma za afya.

b) Muonekano wa mgonjwa wa kisukari kinachotegemea insulin mara nyingi huwa ni mwembamba wakati Yule mwenye kisukari kisichotegemea insulin huwa mnene.

Aina Za Vyakula Na Kazi Zake katika Mwili:

Zifuatazo ni aina mbalimbali za vyakula na kazi zake katika mwili;

A) Vyakula Vyenye Wanga.

Vyakula hivi ni pamoja na aina zote za nafaka, viazi aina zote, mihogo, magimbi, na ndizi.

carbohydrate foods

Kazi Ya Vyakula Vyenye Wanga Mwilini.

Vyakula vyenye wanga huupa mwili nguvu.

B) Vyakula Vyenye Protini.

Aina hii ya vyakula ni pamoja na maharage, kunde, mbaazi, soya, karanga, njegere, njugu mawe, dengu, choroko, asili ya wanyama ni: nyama, mayai, samaki, dagaa, kumbikumbi, senene, maziwa na nzige.

protein foods

Kazi Ya Vyakula Vyenye Protini Mwilini.

Vyakula vyenye protini hujenga mwili.

C) Vyakula Vyenye Vitamini Na Madini.

Aina hii ya vyakula ni pamoja na matunda aina zote na mboga mboga za aina mbalimbali.

vitamin and mineral foods

Kazi Ya Vyakula Vyenye Vitamini Na Madini Mwilini.

Vyakula vyenye vitamini na madini huupa mwili kinga imara dhidi ya maradhi mbalimbali.

D) Vyakula Vyenye Mafuta Na Sukari.

Aina hii ya vyakula ni pamoja na mafuta ya kupikia, aina zote za ufuta, asali, miwa nk.

fat and sugary foods

Kazi Ya Vyakula Vyenye Mafuta Na Sukari Mwilini.

Vyakula vyenye wanga huupa mwili nguvu.

Vyakula Vya Kuepuka Kwa Mgonjwa Mwenye Kisukari:

Maakuli na ulaji unaofaa husaidia mwili kuwa na kiwango cha sukari na mafuta vinavyostahili katika damu, hupunguza unene uliopita kiasi, hutosheleza mahitaji ya mwili ya nishati, madini, vitamini nakadharika, ili kuuwezesha mwili kuwa na kiwango cha kawaida cha sukari kwenye damu, uzito unaostahili na kufanya kazi ipasavyo, unashauriwa yafuatayo;

A) Epuka Kula Vyakula Vilivyowekwa Sukari.

Vyakula unavyopaswa kuviepuka ni pamoja na; Sukari, glukosi, asali, jamu, keki, pipi, ice cream, chocolate, soda.

Badala yake unashauriwa kutumia chai, kahawa, maziwa na uji vyote bila sukari au kwa kuongeza ladha kwa kutumia vidonge vinavyopatikana katika maduka ya dawa (saccharin au sweetex). Club soda na madafu pia vinaruhusiwa.

B) Punguza Kiasi Cha Mafuta.

1) Epuka kula mafuta yenye asili ya wanyama.

2) Punguza utumiaji wa mafuta ya maji yenye asili ya mimea kwa mfano mafuta ya alizeti, mafuta ya karanga, mafuta ya korosho, mafuta ya tui la nazi nk.

3) Kuwa na mazoea ya kula vyakula vilivyochomwa au kubanikwa kuliko vile vilivyokaangwa katika mafuta mengi kama chips, sambusa, maandazi.

4) Usipendelee kula nyama nono (nyama ya ng’ombe, mbuzi nk), mayai, figo, au maini kila siku kwani husababisha kupanda mno kwa kiwango cha aina ya mafuta mabaya (high cholesterol level) yanayosababisha damu kuganda kwenye mishipa ya damu na kuleta magonjwa ya moyo.

5) Unashauriwa kuchagua kula zaidi maharage, samaki, au kuku aliyetolewa ngozi.

C) Epuka Unywaji Wa Pombe Kupita Kiasi.

1) Unashauriwa kuacha kunywa pombe.

2) Ukishindwa kuacha unashauriwa usinywe zaidi ya chupa mbili za bia au glass mbili za mvinyo au toti nne za vinywaji vikali kila siku.

D) Usikae Bila Kula Kwa Muda Mrefu.

1) Inashauriwa mtu mwenye kisukari asikae na njaa muda mrefu.

2) Ni vizuri kula mara tatu au zaidi kwa siku na ikiwezekana vitafunio vidogo vidogo katikati ya milo mikubwa.

3) Usipendelee kula mlo mmoja mkubwa mchana au jioni.

4) Mfano wa milo kwa siku: Kula chakula cha asubuhi saa 1, kula kidogo saa 4, kula chakula cha mchana saa 7, kula kidogo saa 10, kula chakula cha jioni saa 1.

5) Ukifunga ramadhani, ni lazima kubadilisha muda wako wa kutumia dawa na hata kiasi cha dawa.

Vyakula Anavyopaswa Kula Mgonjwa Mwenye Kisukari Bila Masharti:

Vyakula unavyoweza kula bila masharti ni kama ifuatavyo;

1) Mboga za majani (mchicha, spinach).

2) Nyanya, matango, bamia, karoti, vitunguu, pilipili hoho, pilipili, viungo vyote vya vyakula (bila chumvi nyingi), maji ya kunywa, chai na kahawa.

 Kumbuka:

1) Unashauriwa kula vyenye wanga hasa nafaka zisizokobelewa kwa mfano dona kwani huupatia mwili ‘fibres’ vitamini na madini.

2) Kuwa na uzito wa kawaida.

a) Ikiwa una uzito uliozidi, unashauriwa kuupunguza.

b) Punguza kiasi cha kila aina ya chakula na epuka mafuta mengi.

3) Pamoja na ushauri wa chakula, usiache matibabu ya kisukari.

4) Mambo ya kukumbuka hata kama hauna ugonjwa wa kisukari.

a) Usivute sigara.

b) Jitahidi kupunguza uzito kama una uzito ulozidi.

c) Epuka kunywa pombe kupita kiasi.

d) Fanya mazoezi ya viungo mara kwa mara.

5) Hakuna haja ya kupikiwa chakula maalumu badala yake unashauriwa kula vyakula vinavyoliwa na familia yako isipokuwa vile vilvyowekwa au vyenye sukari.

6) Unaweza kula matunda aina zote.

a) Tunda utakalokula kama ni embe au papai au tunda lolote kiwe ni kipande cha kadiri tu.

b) Unaweza kula zaidi ya mara moja kwa siku.

c)  Mfano mzuri wa namna ya kula matunda. Chungwa moja asubuhi, ndizi moja mchana, kipande cha papai au embe jioni.

7)Kula mboga za majani au kachumbari kila siku kwa wingi ambapo inashauriwa nusu ya kila mlo wako unaokula iwe ni mboga mboga.

HITIMISHO:

By the way, hivi unajua kwamba virutubisho vifuatavyo: Provitality, Neolife shake, na Botanical vitakusaidia kudhibiti kiwango kikubwa cha sukari mwilini? Ndio ni kweli kupata virutubisho hivi tuma ujumbe sasa hivi kwenda 0625 305 487.