Yajue Mambo 7 Muhimu Kuhusu Ugonjwa Wa Siko Seli.

Ugonjwa wa siko seli ni aina ya ugonjwa wa kurithi ambao huathiri seli nyekundu za damu na vibeba oxygen kwenye damu vinavyoitwa haemoglobin, haemoglobin ni kiambata cha protein kilichopo kwenye seli nyekundu za damu, kazi yake ni kubeba hewa safi ya oxygen kuisafirisha sehemu mbalimbali za mwili kupitia kwenye damu. Ugonjwa huu hujulikana kwa kitaalamu kama sickle cell disease (SCD), japo wengine hupenda kuita seli mundu.

Ugonjwa wa sikoseli ni kundi la maradhi ya kurithi ya seli nyekundu za damu ambapo hutokea pale mtu anaporithi jeni ya beta-globin zilizoathirika kutoka kwa mzazi wake, jeni hizi zinaathiri moja kwa moja ufanyaji kazi wa seli nyekundu za damu. Kwa kawaida seli nyekundu za damu zenye afya huwa za mviringo, huishi kwa wastani wa siku 120, husafiri ndani ya mishipa ya damu kusambaza hewa safi ya oksijeni kwenda sehemu mbalimbali za mwili.

Ndani ya mwili wa mtu mwenye ugonjwa wa siko seli, seli nyekundu za damu hugeuka kuwa na umbo la C, ama umbo la mwezi nusu, umbo linalofanana na kifaa cha shambani kiitwacho “sickle” (mundu).

Seli hizi hufa mapema, hali ambayo husababisha mtu awe na upungufu wa damu kila wakati. Pia seli hizi za damu zenye umbo la mundu zinapata ugumu kusafiri kwenye mishipa ya damu kutokana na umbo lake, jambo ambalo hupelekea seli hizi kuvunjika na kukwama njiani kwenye mishipa ya damu na kuzuia damu kusafiri. Hivyo kupunguza usafirishaji wa hewa safi ya oxygeni kwenda sehemu mbalimbali za mwili.

Siko Seli Hupatikanaje?

Siko seli hupatikana baada ya mtoto kurithi baadhi ya jeni (Vinasaba) zilizoathirika kutokana na ugonjwa wa siko seli. Kwa hiyo kama mzazi mmoja ana vinasaba hivyo basi mtoto atarithi jeni hizo lakini ugonjwa na dalili hazitajionesha mpaka pale huyu mtoto atakapopata mzazi mwenzake ambaye na yeye alibeba jeni zilizoathirika basi mtoto atakayezaliwa atakuwa na siko seli anemia na dalili zake zitakuwa zinajionesha. Kwa hiyo kabla wazazi hawajapata mtoto wanaweza kufanya vipimo ili kujua kama wamebeba jeni za siko seli.

Soma pia hii makala: Vijue Vyakula Vinavyo ongeza Kiwango Cha Damu Mwilini Kwa Haraka.

Aina Za Ugonjwa Wa Siko Seli:

Aina za ugonjwa wa siko seli ambazo huonekana mara nyingi ni pamoja na;

1) HbSS.

Watu wenye aina hii ya ugonjwa wa siko seli wanarithi jeni “S” mbili (jeni: sehemu ya DNA inayorithisha tabia au umbile fulani), moja toka kwa kila mzazi. Hii mara nyingi huitwa sickle cell anemia na ndiyo aina ya ugonjwa huu inayosumbua zaidi.

2) HbSC.

Watu wenye aina hii ya ugonjwa wa siko seli wanarithi jeni “S” moja toka kwa mzazi mmoja na hemoglobin isiyo ya kawaida iitwayo “C”. Hemoglobini ni protini inayowezesha seli nyekundu za damu kusafirisha oksijeni kuelekea sehemu mbalimbali za mwili. 

3) Hbs Beta Thalassemia.

Watu wenye aina hii ya ugonjwa wa siko seli wanarithi jeni moja ya sickle cell “S” kutoka kwa mzazi mmoja na jeni moja ya beta thalassemia, aina nyingine ya anemia kutoka kwa mzazi wa pili. Kuna aina mbili za beta thalassemia ambazo ni pamoja na HbS beta 0 thalassemia na HbS beta + thalassemia  ambapo wale wenye HbS beta O thalassemia huwa na hali mbaya zaidi ya ugonjwa wa siko seli lakini Watu wenye HbS + beta thalassemia huonyesha nafuu kidogo ya ugonjwa wa siko seli.

Kumbuka:

Watu wenye sickle cell trait hurithi jeni moja ya sickle cell “S” kutoka kwa mzazi mmoja na jeni “A” moja ya kawaida kutoka kwa mzazi wa mwingine. Hali hii huitwa sickle cell trait (SCT). Watu hawa hawaonyeshi dalili zo zote za ugonjwa na huishi maisha ya kawaida, lakini huweza kuwarithisha ugonjwa watoto wao.

Dalili Za Siko Seli:

Dalili za ugonjwa wa siko seli anemia huanza kuonekana mtoto akiwa na umri wa miezi mitano. Dalili huwa tofauti kwa watu tofauti na hubadilika na wakati. Dalili zinaweza kuwa ni pamoja na;

1) Upungufu Wa Damu (Anaemia).

Seli za mgonjwa wa siko seli huvunjika haraka na kufa na kumwacha mgonjwa akiwa na idadi chache ya seli nyekundu. Kwa kawaida seli nyekundu huishi kwa muda wa siku 120 kabla ya kuhitaji kubadilishwa. Lakini seli za mgonjwa wa siko seli huishi kwa muda wa siku 10 hadi 20, na kuacha pengo la seli nyekundu (anemia). Bila ya kuwa na kiwango kizuri cha seli nyekundu, mwili haupati oksijeni ya kutosha hali ambayo husababisha uchovu wa mwili.

2) Vipindi Vya Maumivu.

Vipindi vya maumivu vya kujirudia (pain crisis), ndiyo dalili kuu ya siko seli anemia. Maumivu hutokea wakati seli nyekundu za damu zenye umbo la sickle (mundu) zinapoziba mtiririko wa damu kwenye mishipa midogo ndani ya kifua, tumbo na joints. Maumivu huweza kutokea vile vile ndani ya mifupa, mwanaume hupata maumivu uume unaposimama (painful erection).

Maumivu huwa ya uzito tofauti na huweza kudumu kwa saa chache hadi siku chache. Watu wengine hupata vipindi vya maumivu vichache katika mwaka. Wengine huwa na maumivu mara nyingi zaidi.  Maumivu ya kupindukia huhitaji uangalizi hospitalini.

Vijana wengine wa umri wa balehe na watu wazima wenye siko seli anemia hupata maumivu sugu ambayo yanaweza kutokana na kuharibika kwa mifupa na joints na sababu nyingine.

3) Kuvimba Mikono Na Miguu.

Kuvimba mikono na miguu kunatokana na seli zenye umbo la sickle (mundu) kuziba damu isifike kwenye mikono na miguu.

4) Maambukizi Ya Kila Wakati.

Siko seli zinaweza kuliharibu bandama na kukuacha kwenye hali ya kuweza kupata mambukizi ya haraka. Madaktari huwapa watoto wadogo wenye siko seli anemia sindano au antibiotics kuzuia maambukizi hatari kwa maisha yao, kama vile nimonia.

5) Matatizo Ya Kuona.

Vijishipa vidogo vya damu ndani ya macho vinaweza kuzibwa na sikoseli. Hali hii inaweza kuharibu retina, sehemu ya jicho inayoratibu uonaji na kusababisha matatizo ya kuona.

 6) Kuchelewa Kukua Na Balehe.

Seli nyekundu za damu husaidia katika usafirishaji wa oksijeni na virutubisho muhimu kwa ajili ya ukuaji wa mwili kupitia haemoglobin. Upungufu wa seli hizo huweza kusababisha ukuaji wa taratibu kwa watoto wadogo na kuchelewesha balehe kwa vijana.

Tiba Ya Ugonjwa Wa Siko Seli:

Tiba ya siko seli hulenga kupunguza vipindi vya maumivu, kuzipunguza dalili na kuzuia madhara yatokanayo na ugonjwa huu. Tiba inaweza kuwa ni dawa na kuongezewa damu. Kwa baadhi ya watoto na vijana, tiba ya stem cell transplant inaweza kuuponya ugonjwa.

Dawa Ya Siko Seli:

Watoto wenye siko seli anemia wanaweza kupewa penicillin wakiwa na umri kama wa miezi 2 hadi miaka 5 kuzuia maambukizi ambayo yanaweza kuwahatarishia maisha yao, kama vile nimonia.

Watu wazima wenye siko seli anemia wanaweza kulazimika kutumia penicillin maisha yao yote , kama walikwisha pata nimonia au kufanyiwa upasuaji wa kuondoa bandama.

penicillin

Bone Marrow Na Stem Cell Transplant:

Bone marrow au stem cell transplant ndiyo njia pekee ya uponyaji kwa mgonjwa wa s. Bone marrow, kwa kiswahili uboho, ni tishu laini ya mafuta iliyo katikati ya mifupa ambako seli za damu zinatengenezwa. Bone marrow au stem cell transplant ni utaratibu wa kuchukua seli za kutengeneza damu zenye afya kutoka kwa mtu (donor) na kuziweka kwa mtu ambaye uboho wake haufanyi kazi vizuri.

Bone marrow na stem cell transplant ni taratibu za kubahatisha, na zinaweza kuleta matokeo mabaya, ikiwa ni pamoja na kifo. Ili utaratibu huu ufanikiwe, uboho wa watu hawa wawili inatakiwe ulingane. Kwa kawaida, mtoaji mzuri ni kaka au dada. Bone marrow na stem cell transplant hufanywa kwa watoto wadogo.

Madhara Ya Siko Seli:

Yafuatayo ni baadhi ya madhara yanayoweza kutokea kwa mgonjwa mwenye siko seli endapo atashindwa kupata tiba mapema;

1) Kushindwa kushiriki ngono ipasavyo mfano wanaume hupata maumivu uume unaposimama.

2) Moyo kutanuka kutokana na kuongezeka kwa presha kusukuma seli za damu zilizokwama kwenye mishipa ya damu.

3) Uharibifu kwenye viungo mbalimbali vya mwili kama vile figo, ubongo, mifupa, bandama na vingine kutokana na kupungua kwa usambaaji wa damu katika viungo hivyo.

4) Maumivu ya kifua, kukohoa, homa (Acute chest syndrome).

5) Osteoporosis (low bone density).

HITIMISHO:

Kwa uhitaji wa ushauri, vipimo na tiba ya magonjwa ya afya ya uzazi wasiliana nasi  kwa simu namba 0625 305 487.

vipimo