Sababu Za Uke Kutoa Harufu Mbaya Wakati Wa Tendo.

Kutoa Harufu Mbaya Ukeni:

Kutokwa na harufu mbaya ukeni ni tatizo linalowasumbua wanawake wengi duniani, hususani wakati wa tendo la ndoa. Kutokwa na harufu mbaya ukeni kwa kiasi kikubwa husababishwa na fangasi wa candida albicans, japo sio kila mara ndio maana kuna umuhimu wa kutafuta chanzo cha tatizo la kunuka uke.

harufu mbaya

Harufu mbaya kutoka ukeni wakati wa tendo la ndoa inaweza kusababishwa na mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na:

1) Maambukizi Ya Bakteria.

Maambukizi ya bakteria (Bacterial Vaginosis) ni mojawapo ya sababu inayochangia harufu mbaya ukeni. Maambukizi haya hutokea wakati kuna mabadiliko katika uwiano wa bakteria ndani ya uke, ambapo bakteria wabaya (pathogens) wanakuwa wengi kuliko bakteria wazuri (normal flora). Hali hii inaweza kusababisha harufu mbaya ukeni inayofanana na shombo la samaki, hasa baada ya kufanya tendo la ndoa.

bacterial vaginosis

2) Maambukizi Ya Fangasi Ukeni.

Maambukizi ya fangasi ukeni (Yeast Infection) yanaweza kusababisha harufu mbaya ukeni pamoja na dalili nyingine kama vile kuwasha na kutokwa na uchafu mweupe ukeni unaofanana na jibini (maziwa mgando).

fangasi ukeni

3) Magonjwa Ya Zinaa.

Baadhi ya magonjwa ya zinaa (Sexually Transmitted Infections) kama trichomoniasis, gonorrhea, na chlamydia yanaweza kusababisha harufu mbaya kutoka kwenye uke.

magonjwa ya zinaa

4) Kukosekana Kwa Usafi Binafsi Wa Kutosha.

Ukosefu wa usafi binafsi kwa mwanamke unaweza kuchangia harufu mbaya ukeni. Mwanamke unashauriwa kuepuka kutumia sabuni zenye kemikali au bidhaa zenye harufu kali katika kuosha sehemu za siri kwa sababu zinaweza kuvuruga usawa wa pH ya uke.

5) Mabadiliko Ya Homoni.

Wakati wa mzunguko wa hedhi, ujauzito, au kipindi cha ukomo wa hedhi (menopause), mabadiliko ya homoni yanaweza kuathiri harufu ya uke. Mfano: Baadhi ya wanawake wanapata harufu mbaya ukeni wakati wa hedhi au baada ya hedhi kutokana na mabadiliko ya homoni na uwepo wa damu kwenye uke.

homoni

6) Matumizi Holela Ya Antibiotics Na Bidhaa Za Kemikali.

Hutumiaji kiholela wa dawa, antibiotics bila ushauri au maelekezo ya wataaalamu wa afya (daktari) ni mojawapo ya sababu ya mwanamke kutoa harufu mbaya ukeni lakini pia matumizi ya sabuni zenye harufu kali, douches, au bidhaa nyingine za kemikali kwa ajili ya kuosha uke inaweza kuvuruga usawa wa pH ya uke na kusababisha harufu mbaya ukeni.

7) Maambukizi Katika Viungo Vya Uzazi Vya Ndani Vya Mwanamke.

Maambukizi ya viungo vya uzazi vya ndani vya mwanamke (Pelvic Inflammatory Disease) kama vile mirija ya fallopian, kizazi, na ovari. PID mara nyingi husababishwa na maambukizi ya bakteria, kawaida kupitia ngono zisizo salama. Harufu mbaya kutoka ukeni inaweza kuwa moja ya dalili za PID, ingawa si dalili pekee. Dalili zingine za PID zinaweza kujumuisha maumivu ya tumbo chini ya kitovu, kutokwa na ute wenye rangi na harufu mbaya ukeni, maumivu wakati wa kujamiiana, na homa.

uchafu mweupe ukeni

Jinsi Ya Kuondoa Harufu Mbaya Ukeni:

Ili kudhibiti harufu mbaya ya uke, ni muhimu kwa mwanamke kuzingatia mambo yafuatayo:

1) Fanya usafi wa uke mara kwa mara kwa kutumia maji na sabuni isiyo na kemikali kali.

2) Vaa nguo za ndani za pamba ambazo huruhusu hewa kupita.

3) Epuka kutumia bidhaa zenye harufu kali katika maeneo ya siri.

4) Mtembelee daktari mara tu unapogundua harufu isiyo ya kawaida ili kufanyiwa uchunguzi na kupata matibabu sahihi.

HITIMISHO:

By the way hivi unajua kwamba dawa ya asili iitwayo PANACEA iliyotengenezwa kutokana na mimea na matunda itakusaidia mwanamke kutokomeza changamoto ya kutoa harufu mbaya ukeni?

Ndiyo ni kweli, kupata dawa hiyo wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487.

panacea