Uti Kwa Wanaume: Zijue Sababu Zinazopelekea Kuugua Uti, Dalili, Tiba, Madhara Na Jinsi Ya Kujikinga.

Uti kwa wanaume  maambukizi ya mfumo wa mkojo kwa wanaume ambao huhusisha figo (kidney), kibofu cha mkojo (urinary  bladder), mrija wa mkojo kutoka kwenye kibofu cha mkojo (urethra) pamoja na mrija unao unganisha figo na kibofu cha mkojo (ureter).

Maambukizi haya kwa kiasi kikubwa husababishwa na bakteria jamii ya E. coli, lakini katika mazingira machache fangasi na virusi wanaweza kuwa chanzo cha maambukizi haya.

uti kwa wanaume

Sababu Za Uti Kwa Mwanaume:

UTI kwa mwanaume yaweza kusababishwa na vijidudu vya namna nyingi. Mathalani ni vimelea (bakteria) japo pia na jamii nyingine ya vijidudu vinaweza kusababisha UTI. Bakteria aina ya Escherichia coli kwa kiasi kikubwa ndio inayosababisha UTI japo pia bakteria wengine wapo. Vijidudu hivi vyaweza kuingia katika njia ya mkojo kutokea nje ya mwili au hata kwa kupitia damu ya mhusika.

Kwa wanaume mara nyingi kutokana na maumbile yao na mfumo mzima wa mkojo na viungo vyake, huwa siyo waathirika wakubwa wa UTI ukilinganisha na wanawake.

escherichia coli

Soma pia hii makala: Uti Kwa Wanawake: Zijue Sababu 3 Zinazopelekea Kuugua Uti, Tiba Mbadala Na Jinsi Ya Kujikinga.

Dalili Za Uti Wa Mwanaume:

Zifuatazo ni dalili za uti kwa mwanaume ambazo ni pamoja na:

1) kusikia maumivu wakati wa kukojoa.

2) Homa na maumivu katika viungo vya mkojo.

3) kuhisi kuhitaji kukojoa mara kwa mara na pia mkojo kuwa na hali ya kuunguza wakati wa kukojoa.

4) Maumivu ya tumbo chini ya kitovu na au mgongo kwa chini. 

5) Mkojo wenyewe unaweza kuonekana una ukungu, damu au usaha.

Tiba Ya Uti Kwa Wanaume:

Tiba ya uti kwa wanaume inahusisha matumizi ya dawa za kuua bakteria katika njia ya mkojo ziitwazo antibiotics ambazo hutolewa na daktari baada ya mgonjwa kufanyiwa vipimo, hasa kipimo cha mkojo.

urinalysis

Dawa Za Uti Kwa Wanaume.

Baadhi ya dawa zinazoweza kutolewa na daktari kwa mgonjwa mwenye ugonjwa wa uti isiyo sugu ni pamoja na:

1) Ciprofloxacin.

2) Erythromycin.

3) Amoxicillin.

4) Nitrofurantoin.

5) Amoxyclav.

Kumbuka

Dawa zilizoorodheshwa hapo juu zinatibu maambukizi ya bakteria katika njia ya mkojo na dozi yake inapaswa kutumika kuanzia siku 3 hadi 7.

Uchaguzi wa mgonjwa mwenye uti atumie dawa ipi kati ya hizo zilizoorodheshwa hapo juu hutegemea mambo kadhaa kama vile, aina ya bakteria aliye sababisha ugonjwa, aina ya uti na hali ya mgonjwa.

Dawa Ya Uti Sugu Kwa Mwanaume.

By the way, hivi unajua kwamba virutubisho vifuatavyo: Garlic allium complex, Tre en en, Chelated zinc na Care vitakusaidia kutibu uti sugu?. Ndio ni kweli kupata virutubisho hivi bonyeza hapa 0625 305 487.

Madhara Ya Uti Kwa Mwanaume:

Ugonjwa huu usipotibiwa vizuri unaweza kusababisha madhara yafuatayo kwa mwanaume:

a) Figo kushindwa kufanya kazi (kidney failure), hii ni hatari sana  na hutokana na bakteria kushambulia figo.

b) Magonjwa ya kibofu cha mkojo kama vile kibofu cha mkojo kuziba, kushindwa kukojoa hali ambayo hupelekea mgonjwa kukojoa kwa mrija (urinary catheterization).

c) Maumivu ya mgongo, kiuno na nyonga.

d) Kupoteza hamu ya tendo la ndoa.

e) Uti sugu.

Jinsi Ya Kujikinga Na Uti Kwa Wanaume:

Kuna baadhi ya njia zinazoweza kutumika kujikinga na tatizo la UTI ya kujirudia kwa wanaume. Mfano wa njia hizo ni pamoja na:

1) Kunywa maji na vinywaji kwa wingi kila siku. Hii itakusaidia ukojoe mara kwa mara na kutoruhusu bakteria kujenga makazi kwenye njia ya mkojo. Kojoa kila ujisikiapo mkojo na usiubane kwa muda mrefu.

2) Epuka ngono zembe kwa kutumia kondomu wakati wa kujamiiana nayo ni kinga nzuri dhidi ya uti.

3) Kuacha tabia ya kutunza mkojo kwa muda mrefu baada ya kuhisi haja ndogo. Mkojo ukikaa sana kwenye kibofu unaweza kuzalisha bakteria.

4) Kwenda haja ndogo (kukojoa) mara tu umalizapo tendo la kujamiiana. Hii itasaidia kutoruhusu bakteria kuingia na kujenga makazi kwenye njia ya mkojo.

5) Kuacha mazoea ya kuvaa nguo za ndani mbichi.

HITIMISHO:

Kwa msaada wa ushauri, vipimo na tiba ya magonjwa ya afya ya uzazi kwa wanaume na wanawake wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487.

vipimo