Madhara Ya Fangasi Kwa Mwanaume.

Fangasi sehemu za siri kwa mwanaume, ingawa inaweza kutibika kirahisi, inaweza kusababisha madhara ikiwa haitatibiwa au ikiwa maambukizi yamekuwa sugu.

Picha Za Fangasi Kwenye Uume:

Yafuatayo ni baadhi ya madhara yanayoweza kusababishwa na fangasi sehemu za siri kwa mwanaume ambayo ni pamoja na:

1) Maambukizi Makali Na Ya Muda Mrefu.

Maambukizi ya fangasi sehemu za siri kwa mwanaume yasipotibiwa yanaweza kuwa makali zaidi na kusababisha maumivu na usumbufu mkubwa kama vile kupata miwasho na kujikuna mara kwa mara sehemu za siri. Maambukizi haya yanaweza kuwa sugu na kujirudiarudia.

2) Phimosis Na Paraphimosis.

Maambukizi ya fangasi sehemu za siri kwa mwanaume yanaweza kusababisha govi kuwa na uvimbe na kuuma, hali inayojulikana kama phimosis (govi kushindwa kurudi nyuma kabisa kutoka kwenye kichwa cha uume) au paraphimosis (govi kushindwa kurudi mbele baada ya kurudi nyuma). Mara nyingi madhara haya ya fangasi huwapata wanaume ambao hawajapata tohara.

Phimosis Na Paraphimosis.

3) Kudhoofisha Mfumo Wa Kinga Ya Mwili.

Maambukizi sugu ya fangasi sehemu za siri kwa mwanaume yanaweza kuashiria au kuchangia kudhoofisha mfumo wa kinga ya mwili, hali ambayo inaweza kuwa hatari zaidi kwa watu wenye magonjwa kama vile kisukari au HIV.

4) Uwezekano Wa Kueneza Maambukizi Kwa Wenza.

Fangasi sehemu za siri kwa mwanaume inaweza kuenezwa kwa wenza wake anaoshiriki nao ngono, na hivyo kusababisha maambukizi kwa wenza na hata kujirudiarudia kwa maambukizi kati ya wenza wake.

5) Madhara Ya Kisaikolojia Na Kiakili.

Maumivu, muwasho sehemu za siri, na usumbufu wa kujikuna mara kwa mara vinaweza kuathiri maisha ya kila siku ya mwanaume, kuleta aibu, kujitenga kijamii, na matatizo ya kiakili kama vile wasiwasi na msongo wa mawazo (sonona).

6) Maumivu Na Usumbufu Wa Kupata Miwasho Wakati Wa Kujamiana.

Miwasho na maumivu yatokanayo na maambukizi ya fangasi sehemu za siri kwa mwanaume wakati wa kujamiiana yanaweza kusababisha matatizo katika mahusiano ya kimapenzi kama vile migogoro na kupunguza hamu ya ngono.

Hatua Za Kujikinga Na Kutibu Fangasi Sehemu Za Siri:

Ikiwa mwanaume umeathiriwa na fangasi sehemu za siri ni muhimu kuzingatia mambo yafuatayo:

1) Matumizi Ya Dawa Za Antifungal.

Dawa za kupaka na vidonge vya antifungal vinaweza kutibu maambukizi ya fangasi. Ni muhimu kutumia dawa kama inavyoelekezwa na daktari.

Soma pia hii makala: Dawa Za Fangasi Sehemu Za Siri Kwa Mwanaume.

2) Usafi Wa Sehemu Za Siri.

Kudumisha usafi na ukavu wa sehemu za siri ni muhimu. Osha na kausha vizuri eneo hilo kila siku.

3) Kuepuka Sabuni Zenye Kemikali Kali.

Tumia sabuni laini zisizo na harufu kali ili kuepuka kuwasha na mzio (allergy).

4) Kuvaa Nguo Za Ndani Zilizotengenezwa Kwa Pamba.

Vaa nguo za ndani (boksa) zilizotengenezwa kwa pamba ambazo huruhusu hewa kupita na kuzuia unyevu.

5) Matumizi Ya Kinga Wakati Wa Ngono.

Tumia kinga kama vile kondomu wakati wa ngono ili kupunguza hatari ya kuambukizana fangasi na magonjwa mengine ya zinaa.

HITIMISHO:

Ikiwa dalili za maambukizi ya fangasi sehemu za siri hazipotei baada ya kutumia dawa za kawaida za antifungal au kama maambukizi ya fangasi sehemu za siri yanajirudia mara kwa mara, ni muhimu kumwona daktari kwa uchunguzi zaidi na matibabu sahihi.