Yajue Mambo 8 Muhimu Kuhusu Kansa Ya Shingo Ya Kizazi.

Shingo Ya Kizazi:

Shingo ya kizazi ni sehemu ya kizazi kati ya uke (vagina) na mji wa mimba (uterus). Sehemu hii ya kizazi hujulikana kwa kitaalamu kama cervix.

Picha Ya Shingo Ya Kizazi:

Shingo ya kizazi ina kazi nyingi ikiwemo; 

1) Kupitisha mbegu za kiume kuelekea katika mji wa uzazi na hatimaye mirija ya uzazi (fallopian tubes) ili kupevusha yai (ovum).

2) kupitisha damu ya hedhi, mlango anaopitia mtoto wakati wa kuzaliwa.

Kansa Ya Shingo Ya Kizazi:

Hii ni aina ya kansa inayoshambulia seli zilizoko ndani ya ngozi laini inayozunguka shingo ya kizazi.

Soma pia hizi makala:

Kansa Ya Shingo Ya Kizazi Husababishwa Na Nini?

Kansa ya shingo ya kizazi husababishwa na aina ya kirusi kinachoitwa ‘Human Papilloma Virus’ HPV, kirusi hiki huambukizwa kwa njia ya kujamiiana na mtu mwenye maambukizi.

Sababu Za Kansa Ya Shingo Ya Kizazi:

Zifuatazo ni sababu zinazomuweka mwanamke katika hatari ya kupata kansa ya shingo ya kizazi ambazo ni pamoja na;

1) Kuanza ngono katika umri mdogo (chini ya miaka 18).

2) Uvutaji wa sigara.

3) Kuwa na wapenzi wengi au kujamiiana na mtu mwenye wapenzi wengi.

4) Matumizi ya mafuta mengi kwenye chakula au kula vyakula vyenye mafuta kwa wingi.

5) Kutokula mboga za majani na matunda.

6) Upungufu wa kinga mwilini.

Dalili Za Kansa Ya Shingo Ya Kizazi:

Kansa ya shingo ya kizazi huanza na kuendelea kwa muda mrefu bila kuonesha dalili zozote. Dalili ambazo zinaweza kujitokeza wakati ugonjwa upo katika hatua za mwisho ni pamoja na;

1) Kutokwa na damu isiyo ya hedhi.

2) Kutokwa na damu ukeni baada ya kujamiiana.

3) Kutokwa na damu ukeni kwa wanawake waliokwisha kukoma hedhi.

4) Damu iliyochanganyikana na majimaji ya uke.

5) Matone ya damu au damu kutoka kipindi kisicho cha hedhi.

6) Kutokwa na majimaji au uchafu ukeni wenye harufu mbaya wakati mwingine ukiwa umechanganyika na damu.

7) Maumivu wakati wa kujamiiana (dyspareunia).

8) Maumivu chini ya tumbo, nyonga na kiunoni.

9) Kukojoa mkojo wenye damu (hematuria).

10) Upungufu wa damu (anaemia).

Matibabu Ya Saratani Ya Shingo Ya Kizazi:

Matibabu ya saratani ya shingo ya kizazi hutolewa kulingana na hatua ya ugonjwa.

Ugojwa ukiwa katika hatua za mwanzo huweza kutibika kabisa (ingawa kuna uwezekano wa kujirudia).

Hatua za mwisho za ugonjwa huu huwa haziwezi kupona kabisa. Kinachofanyika mara nyingi ni kutoa matibabu yatayotuliza dalili na maumivu na kumuwezesha mgonjwa kuishi vizuri.

Huduma za matibabu hutolewa kwa njia zifuatazo:

1) Upasuaji katika hatua za mwanzo za ugonjwa.

2) mionzi.

3) Dawa za saratani.

4) Mionzi pamoja na dawa za saratani.

Jinsi Ya Kupima Saratani Ya Shingo Ya Kizazi:

Mara nyingi saratani ya shingo ya kizazi huchukua muda mrefu mpaka kuonesha dalili.

Vipimo vya uchunguzi vinavyofanyika ni pamoja na;

1) Pap Smear.

Kipimo hiki ni rahisi na hakina madhara yoyote. Inashauriwa kufanya kipimo hiki mara moja kwa mwaka.

PAP SMEAR

2) Colposcopy.

Hiki ni kipimo kinachotumia darubini (colposcope) kuangalia seli zilizondani ya ngozi inayozunguka shingo ya kizazi.

COLPOSCOPY

HITIMISHO:

Kwa msaada wa ushauri, vipimo na tiba ya magonjwa ya afya ya uzazi wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487.

VIPIMO