Zijue Dawa 7 Hatari Kwa Mama Mjamzito.

Kwa kawaida mama mjamzito haruhusiwi kutumia dawa ya aina yoyote kiholela bila utaratibu kutoka kwa wataalamu wa afya.

Leo katika makala yetu tuta zungumzia dawa, antibiotics ambazo mama mjamzito hatakiwi kutumia kutokana na aidha madhara yake kwa mama mwenyewe au mtoto aliye tumboni.

Dawa hizi ni pamoja na;

G – Griseofulvin.

C – Chloramphenicol.

R – Rifampicin.

A – Aminoglycosides (Gentamicin).

F – Fluoroquinolones (Ciprofloxacin).

T – Tetracycline

S – Sulfonamides (Flagyl).

Tumia neno ‘G Crafts’ ili kukumbuka dawa hizo kirahisi.

antibiotics

Dawa Hatari Kwa Mama Mjamzito:

Hivyo ungana nami katika kuchambua dawa hizo moja baada ya nyingine;

1) Dawa Ya Mseto.

Hii ni dawa inayotibu malaria. Dawa hii ni hatari sana inapotumika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito (first trimester). Dawa hii huingilia ukuaji wa maumbile ya kwanza ya mtoto na kusababisha mwanamke mjamzito kuwa kwenye hatari ya kujifungua mtoto ambaye hajakamilika.

ALU

2) Misoprostol.

Hii ni dawa ambayo ipo kwenye kundi la prostaglandins analogue, ambazo hutumika kuongeza njia ya mlango wa uzazi kipindi cha kujifungua. Pia hutumika kutibu vidonda vya tumbo. Hii ni hatari kwa mama mjamzito kwa sababu husababisha mimba kutoka (miscarriage).

misoprostol

3) Aspirin. 

Hii ni dawa ambayo hutumika kupunguza maumivu (pain killer). Dawa hii ni hatari kwa mama mjamzito kwa sababu husababisha kuvuja kwa damu nyingi hasa kama mama akipata matatizo ya uzazi kama vile placenta previa. Hivyo dawa hii haitakiwi kabisa kutumika kipindi chote cha ujauzito.

Aspirin

4) Praziquantel.

Hii ni dawa inayotumika kutibu minyoo inayopatikana sehemu za maji yaliyotuama. Dawa hii ni hatari kwa wajawazito kwani huingilia mfumo wa ukuaji wa mtoto.

5) Furosemide.

Hii ni dawa inayotumika kurekebisha kiwango cha maji mwilini kwa kushusha ongezeko la maji nje ya mfumo husika wa damu au kufidia maji yanayopotea kupitia mkojo au jasho. Pia hutibu shinikizo la damu (presha). Dawa hii haitakiwi kutumiwa na mama mjamzito.

furosemide

6) Albendazole.

Dawa hii hutumika kutibu minyoo lakini ikitumiwa na mama mjamzito kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito (first trimester), husababisha mimba kutoka. Madaktari hushauri kutumika kwa dawa nyingine mbadala kutibu minyoo mfano mebendazole lakini siyo Albendazole.

7) Fluoroquinolones.

Dawa hizi pia zinaweza kuongeza uwezekano wa kuharibika kwa mimba kulingana na utafiti wa mwaka 2017 kama zitatumiwa na mama mjamzito.

fluoroquinolones

Soma pia hii makala: Mama Mjamzito: Vijue Vyakula Anavyopaswa Kula Na Vyakula Hatarishi Kwa Afya Yake Na Mtoto Aliye tumboni.

HITIMISHO:

Msisitizo: Mama mjamzito hushauriwi kutumia dawa ya aina yoyote kiholela bila utaratibu kutoka kwa wataalamu wa afya.

Kwa msaada wa ushauri, vipimo na tiba ya magonjwa ya afya ya uzazi kwa wanawake wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487.

vipimo