Yajue Mambo 7 Muhimu Kuhusu Ugonjwa Wa Bawasiri (Kuota Vinyama Sehemu Ya Haja Kubwa).

Bawasiri Ni Nini?

Bawasiri ni ugonjwa unaotokana na kuvimba kwa mishipa ya damu katika mfereji wa njia ya haja kubwa.

Ugonjwa huu umekuwa ni ugonjwa hatari sana kutokana na tabia za wagonjwa wenyewe walioathirika na tatizo hili kuficha. Hii ni kutokana na aibu ya tatizo lenyewe lilipo au kuhofia jamii kuwatazama tofauti kwa sababu jamii nyingi hasa za afrika mashariki zinaamini kuwa ugonjwa huu ni mkosi mkubwa.

Ugonjwa huu unajulikana kwa kitalaamu kama ‘Haemorrhoids.’

Ugonjwa huu unaweza kusababisha muwasho, maumivu na damu au kamasi kutoka wakati wa kujisaidia haja kubwa ingawa wakati mwingine hauna dalili.

Soma pia hii makala: Ujue Ugonjwa Wa Genital Warts (Kuota Vinyama Sehemu Za Siri) na Tiba Yake.

Picha Za Bawasiri:

Aina Za Bawasiri:

Kuna aina kuu mbili za bawasiri ambazo ni pamoja na;

1) Bawasiri ya ndani.

Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawajitambui kuwa wana tatizo hili. Aina hii hutokana na kuvimba na kuharibika kwa mshipa wa artery za ndani ya mfereji wa haja kubwa.

Aina hii ya bawasiri hujulikana kwa kitalaamu kama internal hemorrhoids.

Internal hemorrhoids

Aina hii ya bawasiri imegawanyika katika madaraja manne ambayo ni;

i) Daraja la kwanza.

Hii ni bawasiri ambayo haitoki mahali pale panapohusika.

ii) Daraja la pili.

Hii hutokea wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe ndani baada ya kujisaidia.

iii) Daraja la tatu.

Hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenyewe.

iv) Daraja la nne.

Hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi.

Four  grades of internal hemorrhoids

2) Bawasiri Ya Nje.

Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa na huambatana na maumivu makali na kuwashwa kwa ngozi katika eneo la tundu. Pia husababisha mishipa ya damu (vena) kupasuka na damu kuganda na kasababisha aina ya bawasiri iitwayo thrombosed hemorrhoids.

Aina hii ya bawasili hujulikana kwa kitaalamu kama external hemorrhoids.

external hemorrhoids

Bawasiri Husababishwa Na Nini?

Bawasiri hutokea pindi mishipa inayozunguka sehemu ya kutolea haja kubwa kwa ndani kwenye kuta zake kuumia au kukandamizwa kwa kushuka chini na kuvimba.

Mambo yanayochangia kupata Bawasiri:

Yafuatayo ni mambo yanayomuweka mtu katika hatari ya kupata bawasiri ambayo ni pamoja na;

1) Kufunga choo (Constipation).

Kutoa kinyesi kikubwa au kujikamua kwa nguvu wakati wa kujisaidia haja kubwa. Hii huongeza msukumo ndani na kuzunguka veni za kwenye tundu la haja kubwa. Hii inaonekana kuwa ni sababu kubwa ya bawasiri kutokea.

2) Mimba.

Ni kawaida kabisa bawasiri kujitokeza wakati wa uja uzito. Hii hutokea kutokana na msukumo (pressure) unaotokea juu ya rectum na anus kwa kutokana na mtoto kulalia juu ya maeneo hayo.

Pia kutokana na mabadiliko ya homoni wakati wa ujauzito ambayo huchangia mama mjamzito kupata choo kigumu (constipation).

3) Kuzeeka.

Tishu zinazozunguka ndani ya mkundu  zinaweza kupoteza nguvu zake kadri umri unavyokuwa mkubwa na hivyo kumuweka mtu katika hatari ya kupata bawasiri.

5) Kurithi.

Watu wengine wanaweza kurithi udhaifu wa kuta za veini za kwenye eneo la tundu la haja kubwa kutoka kwenye familia zao na hivyo kuwa katika hatari ya kupata bawasiri.

Kumbuka: Sababu zingine hatarishi zinazoweza kupelekea mtu kupata ugonjwa huu ni pamoja na: Kuwa mnene kupita kiasi (obesity), kutokula vyakula vyenye nyuzinyuzi (low fibres diet), kunyanyua vitu vizito mara kwa mara (regular heavy lifting), kufanya mapenzi kinyume na maumbile (anal sex intercourse), matumizi ya vyoo vya kukaa kwa muda mrefu, kuharisha kwa muda mrefu.

Dalili Za Bawasiri:

Kwa kawaida dalili za ugonjwa wa bawasiri hutegemea aina ya bawasiri;

A) Bawasiri Ya Nje.

Dalili za bawasiri ya nje ni pamoja na;

1) Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa.

2) Kupata uvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa

3) Kutokwa na kinyama baada ya kwenda haja.

4) Kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia haja kubwa.

5) Kinyesi kuwa na damu na kunuka harufu mbaya sana.

B) Bawasiri Ya Ndani.

Dalili za bawasiri ya ndani ni pamoja na;

1) Kutoa haja kubwa/kinyesi chenye damu na maumivu yasiyo makali. Unaweza kuona kiasi kidogo cha damu nyekundu kwenye haja kubwa yako.

2) Maumivu na muwasho sehemu ya haja kubwa.

Dawa Za Hospital Za Bawasiri:

Krimu za kupaka na dawa za kuingiza katika njia ya haja kubwa (suppositories) zinaweza kusaidia kupunguza kuvimba, muwasho na maumivu. Dawa hizi hupatikana katika maduka ya dawa. Kuna matibabu mengine ambapo sindano au kamba hutumika ili kupunguza ukubwa wa mishipa ya damu. Dawa ya bawasiri sugu ni upasuaji.

Hydrocortisone cream

Madhara Ya Bawasiri:

Yafuatayo ni madhara yanayoweza kutokea endapo magonjwa mwenye bawasiri atashindwa kupata matibabu mapema;

1) Upungufu wa damu mwilini.

2) Kutokwa na kinyesi bila kujitambua.

3) Kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.

4) Kupungukiwa nguvu za kiume.

5) Kupungukiwa na uwezo wa kufanya kazi kutokana na maumivu.

6) Kupata tatizo la kisaikolojia (msongo wa mawazo).

7) Kupata kansa ya utumbo (Colorectal cancer).

Jinsi Ya Kuepuka Bawasiri:

Ili kuepuka bawasili unashauriwa kufanya mambo yafuatayo;

1) Kula vyakula asilia kwa wingi. Kula matunda zaidi, mboga mboga, nafaka nzima (zisizokobolewa), kula vyakula vyenye nyuzinyuzi kwa wingi (high diet fibers). Kufanya hivyo kunalainisha kinyesi na kuongeza wingi wake hali ambayo itakusaidia kuepukana na shida inayoweza kusababisha bawasiri.

2) Epuka kufanya ngono kinyume na maumbile.

3) Kunywa maji mengi angalau glasi 6 hadi glasi 12 kila siku.

4) Nenda haja kubwa mara tu unapohisi hamu. Ikiwa unasubiri na hamu inakwenda, kinyesi chako kinaweza kukauka na kuwa kigumu wakati wa kujisaidia.

5) Fanya mazoezi mara kwa mara. Kuwa imara kunasaidia kuzuia kuvimbiwa na kupunguza shinikizo la damu kwenye mishipa ya damu, hali ambayo inaweza kutokea kutokana na kusimama au kukaa kwa muda mrefu. Mazoezi pia yanaweza kukusaidia kupoteza uzito kupita kiasi ambao unaweza kuchangia bawasiri.

HITIMISHO:

Matibabu ya bawasiri hutegemea na aina ya bawasiri, mara nyingi wagonjwa wa bawasiri hupatiwa tiba ya kukatwa vinyama hivyo na kushauriwa kuendelea na tiba ya vyakula lakini tiba hii huwa haina matokeo mazuri sana kwa sababu baada ya muda tatizo hujirudia kutokana na kutotibu chanzo cha tatizo. 

Hivyo tiba nzuri na ya uhakika ya ugonjwa huu ni kutumia virutubisho vilivyotengenezwa kutokana na mimea na matunda ambavyo ni pamoja na; Aloe vera plus, garlic, zinc, care, tre en en. Gharama ya virutubisho hivi ni TZS 295,000/=(usafiri bure).

Kupata virutubisho hivyo wasilina nasi kwa simu namba 0625 305 487.