Zijue Sababu 7 Zinazochangia Mwanamke Kukosa Ute Wa Mimba.

Ute Wa Mimba:

Ute wa mimba ni ute unaovutika, ni ute muhimu sana linapokuja suala la kutungwa kwa ujauzito. Ute huu ambao huvutika mithili ya yai husaidia mbegu kuogelea na kupenya kwenye mlango kwa kizazi na kwenda kulirutubisha yai kwenye mirija ya uzazi. Baadhi ya njia za uzazi wa mpango zinapelekea kukosa ute wa mimba ili usishike mimba isiyotarajiwa.

Tatizo la kukosa ute wa mimba linachangia pia uchelewe kupata ujauzito ambapo baadhi ya wanawake watahitaji kutumia kwanza dawa za kuongeza ute ili kushika mimba. Hivyo ute ute laini unaovutika ni wa muhimu ili kuweka mazingira mazuri ya kushika ujauzito.

Siku chache kabla ya mimba kutungwa ute ute laini unaovutika huanza kuzalishwa kwa wingi kwenye mlango wa kizazi. Katika ulaini wake ute huu unaleta mazingira mazuri kwa mbegu za mwanaume kuogelea kupenya mlango wa kizazi. Changamoto yoyote kwenye uke maana yake mbegu haitapenya na mimba haitatungwa.

kukosa ute

Sababu Za Kukosa Ute Ukeni:

Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazochangia mwanamke kukosa ute wa mimba ukeni ambazo ni pamoja na;

1) Madhara Ya Matumizi Ya Baadhi Ya Dawa.

Baadhi ya dawa unazotumia kujitibia maradhi mengine zinaweza kukuletea matatizo kwenye ute wako wa uzazi. Ute kukauka au kukosa kabisa ute au ute wa uzazi kupungua wingi kunaweza kutokea kama matokeo ya dawa zingine unazotumia kujitibu magonjwa mengine.

Baadhi ya dawa zinazotumika kutibu magonjwa yafuatayo zinaweza kuathiri ubora wa ute wako wa uzazi; Dawa za kutibu mzio (aleji), dawa za kuondoa msongo wa mawazo, baadhi ya dawa zinazotibu tatizo la kukosa usingizi, dawa zinazotibu kifafa nk. Kwa kawaida dawa hizo hutumika ndani ya siku chache tu unapoumwa homa au aleji hivyo hupaswi kuziogopa sana. Lakini pia una uwezo wa kutumia dawa za asili zisizo na madhara ili kutibu maradhi mbalimbali.

Angalizo: Usiache kutumia dawa au usibadili dawa yoyote unayotumia bila ruhusa ya daktari wako wa karibu.

2) Umri.

Tafiti zinaonesha kwamba kadri mwanamke anavyozidi kuwa na umri mkubwa kuanzia miaka 35 hivi kwenda juu anaweza kuanza kuuona ute wa uzazi kwa siku chache kidogo kidogo tofauti na alivyokuwa msichana ambapo ubora na uwingi wa ute wa uzazi pia huanza kupungua kidogo kidogo. Mwanamke akiwa kwenye umri wa miaka 20 hivi mpaka miaka 28 anaweza kuwa anauona ute wake wa uzazi kwa kipindi cha mpaka siku 5 na anapata ute bora na wenye afya, lakini pia mwanamke anapofikisha miaka 30 mpaka miaka 40 na kuendelea mpaka miaka 45 anaweza kuuona ute wake wa uzazi kwa muda usiozidi siku 2 au 3. Hata hivyo hali na mabadiliko hayo hutofautiana sana toka mwanamke mmoja hadi mwingine.

3) Maambikizi Kwenye Mji Wa Uzazi.

Maambukizi ya bakteria au fangasi kwenye uke hupelekea ukavu ukeni na kukosa ute wa mimba.

Fangasi ukeni husababisha dalili za muwasho, kutokwa na uchafu mwingine mweupe na maumivu wakati wa kushiriki tendo la ndoa. Harufu mbaya ukeni ni dalili ya maambukizi ya bakteria.

Lakini pia magonjwa ya zinaa kama vile kisonono, kaswende, pangusa yanaweza kupelekea mwanamke akose ute wa mimba ukeni pamoja na kuziba kwa mirija ya uzazi kama hatatibiwa mapema.

Soma pia hii makala: Mambo 6 Muhimu Usiyo yajua Kuhusu Kuziba Kwa Mirija Ya Uzazi Kwa Wanawake.

4) Mvurugiko Wa Homoni.

Ikiwa homoni za uzazi kwa mwanamke hazipo sawa na zimevurugika basi hiyo ni mojawapo ya sababu zinazoweza kupelekea changamoto ya kukosa ute ukeni. Hivyo basi kama mwanamke huoni ute wako wa uzazi au unaona ute wa uzazi usioeleweka kuna uwezekano mkubwa ikawa ni matokeo ya kuvurugika kwa homoni zako za uzazi.

Hormones imbalance

Soma pia hii makala: Mambo 4 Usiyo yajua Kuhusu Mvurugiko Wa Homoni Kwa Wanawake.

5) Kusafisha Uke Kupita Kiasi (Vaginal Douching).

Kuosha uke mara kwa mara hupelekea kuondoa bakteria wazuri (normal flora) wa ukeni na hivyo kuongeza hatari hatari ya kupata maambukizi ukeni kama vile fangasi na kupungua kwa ute ukeni. Mwanamke unashauriwa kuacha kuosha sehemu ya ndani ya uke kwa kutumia manukato na sabuni zenye kemikali, kwani sehemu ya ndani uke hujisafisha yenyewe (vagina is self cleansing) badala yake osha sehemu ya nje ya uke tu.

vaginal douching

Soma pia hii makala: Fahamu Siri 7 Za Utunzaji Wa Uke Ambazo Hakuna Mtaalamu Wa Afya Atathubutu Kukwambia.

6) Matumizi Ya Dawa Za Kupevusha Mayai Ziitwazo Clomifene.

Siyo kila mwanamke anayemeza dawa hizi anakosa ute. Kwa wanawake wanaotumia dawa hizi kwa muda mrefu wanapata changamoto ya kukosa ute ute wa mimba. Endapo utagundua uke wako ni mkavu ama unakosa ute wa mimba baada ya kumeza clomifene, mjulishe daktari wako mapema. Daktari ataweza kukupa dawa zingine kuondoa madhara haya.

clomifene

7) Uzito Mdogo Kupita Kiasi.

Homoni ya estrogen ndio kichocheo kinachopelekea mwili kuzalisha ute wa mimba. Wanawake wenye uzito mdogo sana, na wanaofanya mazoezi makali huwa na kiwango kidogo cha homoni ya estrogen. Kupata lishe nzuri, kupunguza mazoezi na kuongeza uzito yaweza kusaidia kama hichi ndio chanzo cha tatizo lako.

HITIMISHO:

Dawa Ya Kuongeza Ute Kwenye Uke.

Ikiwa unasumbuliwa na changamoto ya kukosa ute wa mimba ukeni unashauriwa kutumia Chelated zinc kama suluhisho lako bora, hivi ni virutubisho vilivyotengenezwa kutokana na matunda na mimea.

Kwa uhitaji wa virutubisho hivyo kwa ajili ya kutatua changamoto yako ya kukosa ute wa mimba ukeni bonyeza hapa: Chelated zinc.

Vyakula Vya kuongeza Ute Kwenye Uke:

Jipatie kitabu (soft copy) kinachoelezea vyakula vinavyosaidia kuongeza ute wa mimba kwa wanawake wenye changamoto ya kukosa ute wa mimba kwa gharama ya Tshs 10,000/= tu. Kupata kitabu hicho bonyeza hapa: KITABU.

ute wa mimba
vipimo vya mfumo wa uzazi