Fahamu Siri 7 Za Utunzaji Wa Uke Ambazo Hakuna Mtaalamu Wa Afya Atathubutu Kukwambia.

Utunzaji wa uke ni jambo la muhimu sana kwa mwanamke. Uke wenye afya bora ni fahari ya mwanamke na furaha kwa mpenzi wake ( mwanaume). Uke wenye afya bora utakufanya mwanamke ujithamini na kujiamini. Kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya kwenye uke ni kiashiria kwamba unaumwa na hauko sawa kiafya.

 Ni kawaida kwa mwanamke kupata harufu ukeni kutokana na hali ya uke kujisafisha wenyewe ili kutoa vimelea wabaya. Lakini pale harufu inapokuwa kali sana mfano wa harufu ya shombo la samaki basi ujue kuna tatizo kubwa kiafya.

 Kutokwa na harufu mbaya ukeni kunaweza kusababishwa na aidha ukuaji wa bakteria (Bacterial vaginosis), trichomoniasis, mabadiliko ya homoni, kutozingatia usafi na kutokwa sana na jasho, au kuvaa pedi masaa mengi.

Soma pia hii makala: Fahamu Njia 7 Zinazotumika Kuondoa Harufu Mbaya Ukeni.

 Leo katika mada yetu ya blogu hii tuta zungumzia mambo 7 ambayo mwanamke anapaswa kutekeleza ili kuweka uke katika hali ya usafi na afya bora.

uke

Mambo 7 Ya Kuzingatia Ili Kuweka Uke Katika Hali Ya Usafi Na Afya Bora:

Yafuatayo ni mambo 7 ambayo mwanamke anapaswa kutekeleza ili kuweka uke katika hali ya usafi na afya bora (utunzaji wa uke);

1) Epuka Kuflash Uke Kila Mara(Vaginal Douching).

Kusafisha uke kila mara hasa kwa kutumia kemikali na sabuni inaharibu mazingira ya bakteria wazuri ukeni (Normal flora). Bakteria hawa ni walinzi kwenye uke, na hivyo kuacha nafasi kwa uke kushambuliwa na bakteria wabaya (pathogens) pamoja na fangasi wa candida. Badala yake unashauriwa kutumia sabuni ya maji iitwayo care isiyokuwa na kemikali yoyote hatarishi kwenye mwili katika utunzaji wa uke.

2) Badili Nguo Zako  Kila Baada Ya Kufanya Mazoezi.

Badilisha nguo zako zenye unyevu unyevu kila baada ya kufanya mazoezi au nguo za spoti baada ya michezo bila kukawia kwani nguo zenye unyevu unyevu ni mbolea nzuri kwa ukuaji wa bakteria wabaya. Tabia hii itakusaidia katika utunzaji wa uke wako.

3) Punguza Uzito Kama Inawezekana.

Uzito mkubwa na kitambi vinakufanya utokwe na jasho kwa wingi Zaidi hasa kwenye uke ambapo jasho na unyevu nyevu vinaleta fangasi na bakteria wabaya. Hivyo chagua kula lishe nzuri na kufanya mazoezi ili kurekebisha mwili wako.

4) Epuka Kutumia Spray Na Marashi Ukeni.

Ukweli ni kwamba ngozi ya uke ni laini sana kwa hiyo inanyonya kwa urahisi kemikali zilizopo kwenye spray  na kuingia kwenye damu.Uke wenye afya bora hauhitaji marashi au manukato. Hivyo katika utunzaji wa uke hutakiwi kutumia vitu tajwa hapo juu (marashi na spray) kwenye sehemu za siri.

5) Vaa Nguo Za Ndani Za Pamba, Zisizo Bana Sana.

Nguo zinazobana zinazuia kupita kwa hewa safi kuelekea ukeni hivyo kusababisha unyevu unyevu ambao ni mbolea kwa bakteria  na fangasi wabaya (pathogens) wanaoleta harufu mbaya kwenye uke. Hivyo hakikisha unabadilisha chupi kila baada ya masaa 12 kwani inasaidia kuzuia ukuaji wa fangasi na bakteria wabaya kwenye uke.

6) Jitawaze  Kutoka Mbele Kwenda Nyuma Baada Ya Haja Ndogo Au Kubwa.

Hakikisha unajipangusa kila baada ya haja ndogo na kubwa kwa kutumia maji safi. Pangusa kutoka mbele ukienda nyuma (front to back wiping) ili usieneze bakteria kwenye uke na hivyo kujiletea maambukizi. Kitendo hiki kitasaidia katika utunzaji wa uke wako.

7) Epuka Baadhi Ya Vyakula Ambavyo Ni Adui Wa Afya Yako.

 Kuna aina nyingi za vyakula ambavyo vinaweza kumuathiri mwanamke kwenye suala la uzazi.Vyakula hivi vinaharibu mazingira ya uke, kuua bakteria wazuri (normal flora) na kubadili pH.Baadhi ya vyakula hivyo ni pamoja na; Pombe, vyakula vyenye sukari, ngano, na vyakula vilivyosindikwa huchochea ukuaji wa fangasi wa candida.

HITIMISHO:

Dumisha Usafi Wakati Wa Hedhi.

Ni kawaida sana mwanamke kutoa uvundo wakati wa hedhi iwapo hatadumisha usafi wa uke wake, hivyo jitahidi kuoga mara kwa  mara walau mara mbili kwa siku, osha uke wako kwa maji safi peke yake, usitumie sabuni zenye kemikali, vaa pedi yako lakini hakikisha unaibadilisha mara kwa mara na haifai kulowa kupita kiasi kwani uvundo wa damu utaanza kujitokeza na vilevile kuna hatari ya kujiletea maambukizi kwenye uke

Baadhi ya maadui kwenye uke ni pamoja na kuingiziwa au kujiingiza vidole/vitu vigeni ukeni bila kunawa mikono yako vizuri, kufanya mapenzi kinyume na maumbile, ulaji mbovu n.k

Uke wenye afya bora hautoi harufu mbaya, hauna fangasi na bakteria wabaya, majimaji kiasi.

Jinsi Ya Kujisafisha Uke:

Toni, kidonge cha maajabu