Mvurugiko wa homoni kwa wanawake ni kitendo cha kuongezeka au kupungua kwa homoni katika mwili wa mwanamke, hivyo kufanya mabadiliko katika mwili wa mwanamke. Tatizo hili pia hujulikana kwa kitaalamu kama Hormonal imbalance.
Mvurugiko huo huathiri kila mwanamke kwa zaidi ya 80%. Asilimia kubwa ya wanawake mabadiliko huanza kati ya miaka 40 na 50, lakini kwa sasa kukosekana kwa usawa wa homoni huweza kuonekana mapema zaidi kuanzia miaka14. Mabadiliko haya asilia hutokea wakati wa balehe (kuvunja ungo), hedhi, ujauzito, kabla na baada ya ukomo wa hedhi.
Mvurugiko wa homoni kwa wanawake huweza kuchangiwa na kutokuwepo kwa usawa katika homoni zifuatazo: Estrogen, progesterone na testosterone ambapo kuzidi au kupungua kwa homoni hizi hupelekea mvurugiko wa homoni kwa wanawake.
Homoni Ya Estrogen:
Hii ni homoni ya kike muhimu zaidi ambayo hutunzwa kwenye ovari, ini na huwasaidia wanawake wajawazito, huwasaidia wasichana kwenye ukuaji, husaidia pia kwenye kipindi cha ovulasheni. Wakati wa hedhi kuisha kabisa kiwango cha estrogeni hushuka.
Kazi Za Homoni Ya Estrogen:
1) Hufanya uke wa msichana uwe umekomaa ili awe tayari kushiriki katika tendo la ndoa na pia kushika mimba.
2) Homoni hii huwafanya wasichana wapate uchu wa ngono, au ashiki ya mapenzi na kwa njia hii huonekana kama homoni ya uzazi wa wanawake.
3) Estrojeni pia husaidia mama anapokuwa mjamzito ili matiti yake yawe tayari kutoa maziwa ya kunyonyesha mtoto.
4) Homoni ya estrojeni ikishirikiana na homoni ya ukuaji (human growth hormone) husaidia katika ubalehe wa wasichana ambapo matiti yao madogo huanza kunenepa na kuwa makubwa.
Upungufu Wa Homoni Ya Estrogen:
Hii ni aina ya mvurugiko wa homoni ambao hutokea sana kwa wanawake waliofikia ukomo wa kujifungua hasa kuanzia miaka 45 na kuendelea na hasa kwa wale waliofikia ukomo wa hedhi ambapo kwa kitaalamu huitwa menopause, kwa upande wa kimo wanawake wembamba uathiriwa zaidi kuliko wanawake wanene. zifuatazo ni dalili za mvurugiko wa homoni ya estrogen;
a) Kuwepo kwa ukavu ukeni.
Hii ni dalili mojawapo inayowapata sana akina mama wenye mvurugiko au upungufu wa homoni ya estrogen, kwenye uke kunakuwepo ukavu, hali hii husababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa na kukosa ute ukeni ambako husababisha mikwaruzo kwenye uke.
b) Maumivu makali wakati wa kushiriki tendo la ndoa.
Kwa kawaida ili mwanaume aweze kushiriki na kufurahia tendo la ndoa inapaswa maandalizi kwa mwanamke yafanyike ili kupelekea uwepo wa ute kwenye uke wake ambao husaidia uboo kupita kwa urahisi, hiyo kama ute haupo ukeni kutokana na upungufu wa homoni ya estrogen lazima mwanamke atapata maumivu wakati wa kushiriki tendo la ndoa.
C) Kutokwa jasho wakati wa usiku.
Kwa sababu ya kuwepo kwa homa za vipindi kunatokana na upungufu wa homoni ya estrogen husababisha mama kutokwa na jasho wakati wa usiku, hata kama Kuna baridi kiasi gani mwanamke mwenye upungufu wa homoni ya estrogen huisi joto wakati wa usiku.
d) Matatizo ya kupoteza kumbukumbu huweza kutokea.
Hii pia ni mojawapo ya dalili za upungufu wa homoni ya estrogen kwa wanawake na ndio maana utawakuta akina mama wengi wenye umri wa kuingia menopause Wana shida ya kusahau sana hii ni kwa sababu ya kupoteza homoni ya estrogen.
e) Kujisikia uchovu mara kwa mara hasa wakati wa kufanya kazi.
Upungufu wa homoni ya estrogen kwa mwanamke hupelekea mwanamke kujihisi mchovu mara kwa mara hasa wakati wa kufanya kazi.
Vyakula vinavyo ongeza homoni ya estrogen:
vifuatavyo ni vyakula vinavoongeza kiwango cha homoni ya estrogen kwa wanawake ambavyo ni pamoja na;
1) Soya.
Soya na bidhaa zinazotengenezwa kutoka kwenye soya, kama vile tofu na miso, ni chanzo bora cha phytoestrogens. Fitoestrojeni ni estrojeni ya asili ambayo hufanya kazi sawa na homoni ya estrojeni kwenye mwili wa mwanamke na kusaidia kupunguza mapungufu yatokanayo na ukosefu wa homoni hii kwa mwanamke. Hivyo ulaji wa soya kwa mwanamke unasaidia kuongeza kiwango cha homoni ya estrogen mwilini.
2) Karanga.
Ulaji wa karanga kwa mwanamke husaidia kuongeza kiwango cha estrogeni mwilini.
Karanga pia ni chanzo muhimu cha phytoestrogens. Fitoestrojeni ni estrogen ya asili ambayo hufanya kazi sawa na homoni ya estrojeni kwenye mwili wa mwanamke na kusaidia kupunguza mapungufu yatokanayo na ukosefu wa homoni hii kwa mwanamke.
3) Mbegu Za Ufuta.
Mbegu za ufuta pia ni chanzo muhimu cha phytoestrogens, pamoja na kutoa kiwango kikubwa cha nyuzi (dietary fibre) na madini ya kalsiamu. Katika mbegu za ufuta pia tunapata lignans, ambayo ni metaboli za sekondari za mimea iliyo na viwango vya juu vya phytoestrogens. Hivyo ulaji wa mbegu za ufuta kwa mwanamke unasaidia kuongeza kiwango cha homoni ya estrogen mwilini.
5) Maharage.
Licha ya maharage kuwa ni chanzo cha protini mwilini, maharage pia yanasaidia kuongeza kiwango cha homoni ya estrogeni katika mwili wa mwanamke kwani yanatoa idadi kubwa ya phytoestrogens, estrojeni ya asili ambayo hufanya kazi sawa na homoni ya estrogen katika mwili wa mwanamke.
6) Mbaazi.
Ulaji wa mbaazi kwa mwanamke unasaidia kuongeza kwa haraka kiwango cha estrogen mwilini.
Mbaazi ni chanzo muhimu cha phytoestrogen, estrojeni ya asili ambayo hufanya kazi sawa na homoni ya estrogen katika mwili wa mwanamke.
7) Vyakula Vyenye Vitamini C.
Ulaji wa Vyakula vyote vyenye vitamini c kwa mwanamke kama vile machungwa, nyanya, tikiti maji, ndizi na vinginevyo unasaidia kuongeza kiwango cha homoni ya estrogen mwilini. Vyakula vyote vyenye vitamini c vinatoa idadi kubwa ya phytoestrogens, estrojeni ya asili ambayo hufanya kazi sawa na homoni ya estrogen katika mwili wa mwanamke.
Homoni Ya Progesterone:
Hii ni homoni muhimu ya uzazi wa mwanamke inayozalishwa na mfuko wa mayai (ovari).
Kazi Za Homoni Ya Progesterone:
1) Inahusika kuweka mzunguko wa hedhi katika mpangilio.
2) Inahusika pia kuweka mimba katika hali salama kwani katika kipindi cha mimba inasaidia kuboresha mzunguko wa damu kwenye mji wa mimba.
Baada ya yai la mwanamke kutolewa na ovari (ovulation) homoni hii huzalishwa kwa wingi ili kuimarisha kuta za mji wa mimba kuandaa kupokea yai lililorutubishwa tayari kwa ajili ya kutengeneza mtoto.
Endapo hakuna yai lililorutubishwa basi homoni hii huachwa kuzalishwa kwa wingi hali inayopelekea mwanamke kupata hedhi.
Vyanzo Vya Mvurugiko Wa Homoni Kwa Wanawake:
Mvurugiko wa homoni ni tatizo linalowakumba wanawake wengi kwa sasa, hii ni kutokana na mfumo wa maisha wanayoishi (lifestyle), elimu finyu waliyonayo juu ya afya zao na kutokula kulingana na makundi ya damu. Vyanzo vya kuvurugika kwa homoni ni kama vile.
a) Uwepo wa sumu mwilini.
b) Mfumo mbovu wa maisha (Unbalanced lifestyle).
c) umri.
d) Kukoma kwa hedhi.
e) Kutofanya mazoezi.
f) Uzito mkubwa.
g) Mabadiliko ya mazingira au hali ya hewa.
h) Msongo wa mawazo.
i) Kula vyakula visivyo endana na blood group.
j) Upungufu wa lishe mwilini.
k) Matumizi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango.
l) Utoaji wa mimba.
m) Family history (upungufu au ongezeko la homoni ya progesterone na estrogen).
0) Ethnicity, wanawake wa kiafrika wengi wana hili tatizo la ongezeko la homoni ya estrogen.
Dalili Za Mvurugiko Wa Homoni Kwa Wanawake:
Baadhi ya dalili zinazoweza kuonekana kwa mwanamke mwenye changamoto ya mvurugiko wa homoni ni kama vile;
a) Ukavu ukeni.
b) Maumivu wakati wa tendo la ndoa.
c) Uchovu wa mara kwa mara.
d) Maumivu chini ya kitovu wakati wa hedhi.
e) Upungufu wa hamu ya tendo la ndoa.
f) Mabadiliko ya siku za hedhi na kupata hedhi kwa muda mrefu unaozidi siku7 (heavy menstrual bleeding).
g) Kukosa hedhi kwa muda mrefu, na kutoa damu yenye mabonge mabonge wakati wa hedhi.
h) Kukosa usingizi.
i) Homa za usiku na kizunguzungu cha mara kwa mara.
j) Mzio wa vyakula (allergy), kuchagua chagua vyakula.
k) Ongezeko la tumbo na nyama uzembe.
l) Kuharibika kwa ngozi (chunusi, vipele).
m) Maumivu ya viungo.
n) Upungufu wa nywele kichwani.
o) Kupata hedhi wakati wa ujauzito (progesterone ikiwa imezidi).
p) Mwili kutokukua, kuonekana kama binti mdogo na kutokukua kwa via vya Uzazi.
Madhara Ya Mvurugiko Wa Homoni Kwa Wanawake:
Yafuatayo ni baadhi ya madhara ya mvurugiko wa homoni kwa wanawake;
a) Kutoshika ujauzito kwa muda mrefu.
b) Mimba kuharibika mara kwa mara.
c) Kukosa mtoto au ugumba.
d) UTI (Urinary Tract Infections).
Soma pia hii makala: Uti Kwa Wanawake: Zijue Sababu 3 Zinazopelekea Kuugua Uti, Tiba Mbadala Na Kinga.
e) Maumivu wakati wa tendo la ndoa.
f) Kuzeeka mapema.
g) Kuziba kwa mirija ya uzazi.
h) Uvimbe (uterine fibroids na ovarian cysts).
SULUHISHO:
A) Suluhisho Linalopendwa.
wanawake wengi baada ya kujifahamu kuwa homoni zao haziko sawa hutumiwa madawa (bioidentical or synthetic hormones) na wengine hufanyiwa hormone replacement therapy. Tiba hii huandaliwa kwa ajili ya kuzifanya homoni zifanye kazi zake kama kawaida. Lakini hupelekea baadhi ya madhara kama;
a) Kuongezeka uwezekano wa shinikizo la damu.
b) Osteoporosis (low bone density).
c) Madhara katika mfumo wa uzazi.
d) Saratani.
B) Suluhisho La Kudumu.
Mvurugiko wa homoni unasababishwa na upungufu wa lishe, msongo wa mawazo, na uwepo wa sumu mwilini na hivi vyote ni vitu unavyoweza kurekebisha. Kwa wanawake wenye changamoto hii tumewaandalia programu ya virutubisho lishe ambavyo vimetokana na mimea asili ambavyo vinasaidia kuweka sawa homoni za mwanamke, kurekebisha mfumo mzima wa uzazi, uleta heshima ya ndoa mana uke utarudi katika hali yake ya asili (mnato na ute ute ukeni wenye kuleta msisimko wakati wa tendo la ndoa), na kupunguza kasi ya uzee kwani sumu zikizidi mwilini mwanamke huzeeka kabla ya wakati na kupatwa na changamoto mbalimbali za kiafya ikiwemo;
a) Vimbe zinazojipachika kwenye uzazi wa mwanamke.
b) Vidonda vya tumbo.
Hivyo programu hii itakusaidia katika kuboresha afya yako na kukuondolea hizo changamoto zote.
Kwa mwanamke yeyote atakayehitaji hii programu kwa ajili ya kutatua changamoto yake ya mvurugiko wa homoni bonyeza hapa: “Hili Ndilo Suluhisho Bora Ukiwa Unataka Kutibu Tatizo La Kutokuona Hedhi/Hedhi Kutokukata.”
Ni mimi mwenye kujali afya yako Dr. ISAYA FEBU.
Mnayo Whatsapp group
Hapana hatuna
Inakuwaje kwa mwanamke mwenye ndevu
Mnapatikana wap kwa dar
Tunaweza wasiliana
Ndio…wasiliana nami kwa simu namba 0625305487
Gharama za kupima mirija ya uzazi maana mke hajapata uja uzito mpaka Sasa
Gharama yake ni 20,000/=
Nko na umri wa miaka 22 nimekuwa nikipata changamoto ya kukosa hedhi kuanzia miezi 3 au zaidi na pia wakati mwingine napata hedhi Kwa siku nyingi zaidi yaani “overbleeding” mpaka ata mwezi mzima.
Shida hiyo imekuwa ikinisumbua tangu nilipovunja ungo nikiwa na umri wa miaka 13
pole sana…matibabu yapo nichek 0625305487
Mimi Nina changamoto ya ukavu uken napata maumivu makali wakat wa tendo pia siku za piriod Kwan mwezi huu nimepata mara mbili alaf natokwa na jasho wakat wa usku
Tiba ipo…nichek kwa namba 0625305487
Nauliza Kwa MTU amabae ana shida ya kutoka na damu nying wakatii wa hedhi inatibiwa Kwa Dawa Gani
I have read some excellent stuff here Definitely value bookmarking for revisiting I wonder how much effort you put to make the sort of excellent informative website
This is my first time pay a quick visit at here and i am really happy to read everthing at one place
Mimi nina kaa sku 50 ndio napata hedhi nina miezi 7 tangu nijifungue je hii ni Sawa
Kwahiyo daktari nawez kufatiliza vyakula tajwa hapo juu ili kurekebisha tatizo langu la hormone?
yes, unaweza pia
Tunapatikana majumba sita kama unaelekea banana
Ni vyakula gani hivyo doctor eti
Tunatakiwa tule ili tatizo liiishe