“Uvutaji Wa Sigara Ni Hatari Kwa Afya Yako.”

Hayo ni maneno yaliyoandikwa kwenye kila pakiti ya sigara…

Lakini…

Kutokana na ripoti ya Tanzania Cigarette Company (TCC) ya Mwaka 2021 inasema kwamba…

Sigara

“Ndani ya Miezi 12 kulikuwa na mzunguko wa zaidi ya Tshs 2.83B…hiyo ni sawa na Tshs 236.24M kwa mwezi”

Inawezekanaje?…

Kwanini licha ya kuwepo na ONYO/TAHADHARI ya kuathiri afya lakini bado watu wananunua sigara na kampuni zinatengeneza mabilioni ya fedha?…

Us billion dollars

Ndani ya sekunde 60 zijazo utaenda kuijua sababu ya kwanini…

Lakini…

Kabla ya hapo hii ndio story yangu na mzee Mbena…

Jana mida ya 12 Jioni nilikuwa nacheza bao na mzee Mbena pale stend ya kipya, Gongo la mboto-Dar es salaam.

Wakati tunaendelea Kucheza huku tukipiga story mbili tatu nikagundua katika mfuko wa kushoto wa shati la mzee Mbena kulikuwa na pakiti ya sigara…

Kwa sababu Mbena ni mtumiaji pia…

Lakini…

Baada ya kuangalia Ile pakiti kwa makini nikakutana na haya maandishi yanayosema…

“uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako”

Nikamuuliza…

Wolf inawezekanaje unavuta sigara huku umeshaambiwa kabisa ni hatari kwa afya yako?…

Inamaana hujipendi?…

Akatabasamu halafu akanishika begani Kisha akaniambia…

“Son…WE DON’T REALLY CARE” (hatujali kabisa)

(Tip: “Huwa namwita Wolf kwasababu mzee Mbena ameishi Marekani na amefanya kazi pale Wall street zaidi ya Miaka 19 kabla ya kurudi bongo, so ni mtu smart mno)

Kwanini?… (nikauliza)

Akasema…

Hatujali kwa sababu huwa tunanunua kwa HISIA (Emotions) na sio mantikiI (Logic)

Logically ni kweli sigara ni hatari…

Ila…

Emotionally tunajinunua sisi bora zaidi baada ya kuvuta sigara…(we buy a better version of ourselves)

Kwanini?…

Kwasababu kinachonunua sigara sio kichwa (penye logic), ni MOYO… (penye hisia)

Akaniambia…

Unajua Dr. Isaya Febu kisaikolojia (Psychologically) binadamu huwa anageuka ndumila kuwili (hasikii)… 

endapo atapewa vitu vya aina 3 ambavyo ni;

1) Kitu ambacho hawezi kukipata…(kilichokatazwa)

2) Kitu kinachotakiwa zaidi na wengine…(Social Proof) 

3) Kitu ambacho ni watu wachache tu ndio wana access ya 

kukipata…(Exclusivity)

Kwahiyo…

Sigara wao wamegeuka Ronaldo, Pele au Messi kwenye hyo point ya kwanza…(kitu kilichokatazwa)

Ukweli ni kwamba watu wanapofanya maamuzi ya kununua vitu huwa hawatumii kabisa akili wala vichwa kuwaza wala kufanya maamuzi… 

…Huwa wanatumia HISIA na huwaza kwa kutumia moyo sio kichwa

Inamaana wangetumia akili (Logic) Kununua sigara…basi wangekuwa Wananunua vitu hivi…

-Saratani ya mapafu, kifua Kikuu na magonjwa mengine ya mapafu.

Lakini…

Kwasababu wanatumia HISIA…basi wananunua vitu vitu hivi…

-Kuonekana wagumu, na Ma-Gangsters 

-Kuonekana wenye CONFIDENCE & Mvuto

-Masculinity traits nk 

Na hiiyo inatupeleka mpaka Kwenye MORAL LESSON (funzo) ya story ya leo ambayo ni…

1) Uuzaji wa sigara ni biashara kama biashara zingine mtaani na ni sehemu kubwa ya chanzo cha mapato katika taifa, lakini mimi nikiwa kama mtaalam afya nakushauri kuepuka uvuaji wa sigara ili kulinda aya yako na wale uwapendao kwani afya ni mtaji namba moja kwa binadamu, bila kuwa na afya njema huwezi kukamilisha malengo yako kwenye maisha

2) Tumia akili sana kuliko hisia katika kufanya maamuzi yoyote yale kwenye maisha yako kwani kuna muda hisia hukudanganya na kufanya ujutie maamuzi uliyofanya.

Natumaini umepata kitu kipya…

By the way kama ungependa kujifunza kuhusu ugonjwa wa saratani ya mapafu ikiwa ni mojawapo ya madhara ya uvutaji wa sigara BOFYA links hapa chini: