Vijue Vyakula 12 Vya Kuongeza Nyege Kwa Mwanamke.

Tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa (nyege) kwa wanawake ni miongoni mwa changamoto zinazoendelea kuwathiri wanawake wengi na hata kupelekea migogoro katika mahusiano au ndoa zao huku tatizo la kukosa la kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa wanaume likizidi kushika nafasi ya kwanza.

Zipo sababu nyingi zinazochangia tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake, baadhi ya sababu hizo ni pamoja na uzalishwaji mdogo wa homoni ya estrojeni katika mwili, matumizi ya dawa za kulevya, msongo wa mawazo (sonona), unywaji wa pombe.

Kwa kawaida wanawake wengi wanaokaribia ukomo wa hedhi au waliokoma hedhi tayari (menopause) hukosa hamu ya tendo la ndoa.

Soma pia hii makala: Ukomo Wa Hedhi Kwa Wanawake Na Tiba Yake.

Wataalamu wa afya wameshauri vyakula vinavyoweza kuwapa wanawake hamu  ya tendo la ndoa. Mtaalamu wa saikolojia wa Uingereza, Cassie Bjork, anasema badala ya kutumia dawa (Viagra) ya kuongeza hamu ya tendo la ndoa kuna vyakula maalum.

sex

Hivyo basi leo katika makala yetu tutazungumzia vyakula vinavyosaidia kuongeza hamu ya tendo la ndoa (nyege) kwa wanawake.

Vyakula Vya Kuongeza Hamu Ya Tendo La Ndoa Kwa Wanawake:

Vifuatavyo ni baadhi ya vyakula vinavyosaidia kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake ambavyo ni pamoja na;

1) Mafuta Ya Samaki.

Zipo aina nyingi za mafuta ya samaki. Lakini mafuta ya samaki yenye asidi ya Omega-3 yana virutubisho ambavyo huongeza kiwango cha ‘dopamine’ kwenye ubongo.

 Dopamine ni kemikali inayotolewa kwenye ubongo ambayo humfanya mtu kujiksia faraja na hisia.  Kama kiwango cha dopamine kitolewacho na ubongo kitaongezeka basi hamu ya tendo la ndoa kwa mwanamke itaongezeka pia.

mafuta ya samaki

2) Spinachi.

Wataalamu wa afya  wanasema mboga ya majani aina ya spinachi ina wingi wa madini ya magnesium ambayo husaidia kusambaza damu kwenye mishipa ya damu inayozunguka viungo vya uzazi, uke. Damu inaposambaa vyema mwilini hasa kwenye viungo vya uzazi, uke hata hamu ya tendo la ndoa huongezeka.

spinachi

3) Chai Ya Kijani (Green Tea).

Chai ya kijani ina kompaundi iitwayo catechins. Kompaundi hii inasaidia kuyeyusha mafuta mwilini. Lakini pia inalisaidia ini  kuchuja sumu na kuisaidia mishipa ya damu kufanya kazi vizuri. Hivyo unywaji wa chai ya kijani husaidia kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake kwani chai ya kijani husaidia kuongeza mzunguko wa damu mwilini hasa kwenye viungo wa uzazi.

green tea

4) Pilipili.

Ndani ya pilipili kuna kompaundi iitwayo capsaicin ambayo hufanya pilipili iwe na hali ya ukali. Capsaicin huwezesha ubongo kutoa homoni ya endorphins ambayo huleta hisia za raha wakati wa kufanya tendo la ndoa.

Pia pilipili husisimua mfumo wa fahamu (nerves) wa ubongo na katika kufanya hivyo humuwezesha mwanamke kusisimka haraka kimapenzi (kunyegeka) wakati wa tendo la ndoa.

pilipili

 5) Tangawizi.

Tangawizi ni kiungo cha mboga ambacho husisimua sana na kusaidia mfumo wa mzunguko wa damu mwilini. Tangawizi zinajulikana sana kwa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi yaani uke hivyo kuwa na umuhimu sana katika kuboresha ufanyaji wa tendo la ndoa. Inaweza kuliwa mbichi, au kuliwa ikiwa imeungwa kwenye chakula au kusagwa na kuwa kama unga na kutumika kwenye chai.

tangawizi

6) Asali.

Baadhi ya vitamini vinavyopatikana kwenye asali ni pamoja na ascorbic acid, pantothenic acid, niacin na riboflavin, madini yanayopatikana kwenye asali ni pamoja na calcium, copper, iron, magnesium, manganese, phosphorus, potassium na zinc. Vitamini na madini hayo husaidia katika uzalishaji wa homoni ya estrojeni na hivyo kuongeza hamu ya tendo la ndoa.

asali

 7) Parachichi.

Aina nyingine ya chakula ambacho husaidia kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake ni Parachichi. Tunda hili lina uwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa estrojeni, homoni ya kike. Inatajwa kuwa wanawake wanaotumia tunda hili kwa wingi huwa na msisimko mkali wa kimapenzi.

parachichi

8) Ndizi Mbivu.

Ndizi mbivu zina kiwango kikubwa cha potasiamu ambacho husaidia kuongeza uzalishaji wa estrojeni, homoni ya kike na kuboresha hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake.

Tryptophan iliyopo ndani ya ndizi mbivu husaidia kuongeza utengenezaji wa serotonin, homoni inayoboresha hisia na kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake.

ndizi mbivu

9) Tikiti Maji.

Tikiti maji lina kiasi kikubwa cha asidi ya amino (L-citrulline) ambayo inachochea mtiririko wa damu kwenye uke. Wanawake wenye tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa wanaweza kunufaika kupitia L-citrulline kwa kula tikiti maji.

tikiti maji

 10) Karanga.

Karanga inasaidia kuchochea mfumo wa mzunguko wa damu mwilini. Ongezeko la mzunguko wa damu kwenye uke humuwezesha mwanamke kupata msisimko wa mapenzi haraka hatimaye tendo la ndoa kuwa murua. Pia karanga zina madini muhimu kama vile magnesium, asidi ya folic na zinc ambayo ni muhimu sana katika uzalishaji wa estrojeni, homoni ya kike.

karanga

11) Mbegu Za Maboga.

Mbegu za maboga zina phytosterol ambayo inajulikana kuboresha uzalishaji wa homoni ya kike, estrojeni katika mwili. Mbegu hizi pia zina mafuta yenye asidi ya omega-3 ambayo husaidia kuboresha mzunguko wa damu katika uke na hivyo kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake.

mbegu za maboga

12) Kitunguu Saumu.

Kitunguu swaumu kina ‘Allicin’ ambayo husaidia kuongeza msukumo wa damu kwenda kwenye uke na hivyo kuongeza hamu ya tendo la ndoa. Hivyo unashauriwa kuongeza matumizi ya kitunguu swaumu kwenye chakula unachopika kila siku. Vile vile unaweza kutafuna punje 2 mpaka 3 za kitunguu swaumu kila unapoenda kulala au unaweza kukatakata (chop)  hizo punje 2 au 3 vipande vidogo vidogo kisha unywe na maji.

kitunguu saumu

HITIMISHO:

Vyakula vingine vinavyoweza kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake ni pamoja na, chokoleti, apple, straw berries n.k

Kwa msaada wa ushauri, vipimo na tiba ya magonjwa ya afya ya uzazi kwa wanawake wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487.

vipimo vya mfumo wa uzazi