Sababu Zinazoweza Kuchangia Upungufu Wa Mbegu Za Kiume.

Mbegu za kiume ni muhimu kwa uzazi wa mwanaume. Upungufu wa mbegu za kiume unaotambulika kitaalamu kama oligospermia, ni hali ambayo kiasi cha mbegu za kiume (manii) katika shahawa za mwanaume kipo chini ya viwango vya kawaida.

Kawaida, hali hii inaweza kuhusishwa na uwezo mdogo wa mwanaume kutungisha mimba (ugumba).

mbegu za kiume

Leo katika mada yetu ya blogu hii tutazungumzia sababu kadhaa zinazoweza kuchangia upungufu wa mbegu za kiume. Ungana nami katika kuchambua sababu hizi.

Sababu Za Upungufu Wa Mbegu Za Kiume:

Sababu za upungufu wa mbegu za kiume zinaweza kutofautiana kwa kila mwanaume lakini zinaweza kujumuisha mambo kama vile:

1) Mazingira Na Mitindo Ya Maisha.

Mambo kama vile mionzi, kemikali hatarishi katika mazingira, uvutaji wa sigara, matumizi ya pombe kupita kiasi, au matumizi ya madawa ya kulevya yanaweza kuathiri ubora na wingi wa mbegu za kiume.

2) Matatizo Ya Afya.

Matatizo ya kiafya kama vile matatizo ya homoni, joto kubwa kwenye korodani ambalo linaweza kusababishwa na matumizi ya nguo zinazobana sana, matatizo ya tezi, au matatizo ya kuzaliwa nayo yanaweza kusababisha upungufu wa mbegu za kiume.

gynecomastia

3) Matumizi Ya Dawa.

Baadhi ya dawa zinaweza kuathiri uzalishaji wa mbegu za kiume. Kwa mfano, baadhi ya dawa za kutibu shinikizo la damu, antidepressants, na dawa za chemotherapy zinaweza kusababisha upungufu wa mbegu za kiume.

chemotherapy

4) Matatizo Ya Maumbile.

Matatizo katika mfumo wa uzazi au maumbile kama vile uvimbe katika mshipa wa damu karibu na korodani (varicoceles), matatizo ya kuzaliwa nayo kwenye njia ya kupitishia mbegu (vas deferens), au matatizo mengine ya maumbile yanaweza kuathiri uzalishaji wa mbegu za kiume.

varicocele

Soma pia hii makala: Fahamu Kiwango Sahihi Cha Mbegu Za Kiume Kutungisha Mimba.

HITIMISHO:

Iwapo una wasiwasi wa upungufu wa mbegu za kiume, ni vyema kushauriana na daktari. Kwa kawaida, vipimo vya damu na manii hufanyika ili kubaini sababu ya tatizo.

Matibabu yanaweza kutofautiana kutoka kubadilisha mtindo wa maisha hadi matibabu ya dawa au hata upasuaji, kulingana na chanzo cha upungufu huo. Katika baadhi ya visa, mtaalamu wa uzazi au daktari wa endokrinolojia ya uzazi anaweza kutoa ushauri na matibabu yanayofaa kwa hali ya mtu binafsi.