Mambo Muhimu Usiyo yajua Kuhusu Kutokwa Na Uchafu Ukeni.

Kutokwa na uchafu ukeni ni mchanganyiko wa majimaji, seli, na vijidudu ambavyo hulainisha na kulinda uke. Mchanganyiko huu hutolewa kila mara kupitia seli ndani ya uke na seviksi na hutolewa nje ya mwili wa mwanamke kupitia uwazi wa uke (vaginal opening).

Uke hutoa aina mbalimbali za uchafu katika kujisafisha. Kutokwa na uchafu ukeni ni tukio la kawaida kabisa, japo kuna aina mbalimbali za uchafu ambazo zinaweza kuonyesha maambukizi. Uchafu usiokuwa wa kawaida unaweza kuwa wa kijani au njano na wenye harufu mbaya. Uchafu usio wa kawaida mara nyingi husababishwa na fangasi ama maambukizi ya bakteria (Pelvic Inflammatory Disease).

Soma pia hii makala: Ujue Ugonjwa Wa PID(Pelvic Inflammatory Disease).

Muonekano wa uke kwa ndani:

Muonekano wa uke kwa ndani
muonekano wa uke kwa ndani

Muonekano wa uke kwa nje:

External female genitalia

Mfumo wa uzazi wa mwanamke ukoje?

Huu ndio mfumo wa uzazi wa mwanamke.

mfumo wa uzazi wa mwanamke
female reproductive system. Internal view of the uterus with cross section.

Sababu Za Kutokwa Na Uchafu Ukeni:

Uchafu wa kawaida utokao ukeni hutokana na utendaji kazi wa mwili wenye afya, na ndio huwa njia pekee ya mwili kujisafisha kulinda uke. Ni jambo la kawaida uchafu kuongezeka kutoka kutokana na mazoezi, kazi nzito, nyege (hisia za kimapenzi) na msongo wa mawazo.Uchafu usio wa kawaida utokao ukeni mara nyingi husababishwa na maambukizi, ambayo ni pamoja na;

1. Bakteria Ukeni.

Maambukizi ya bakteria katika uke husababisha muongezeko wa kutokwa na uchafu ambao huwa una harufu mbaya, na wakati mwingine unakuwa kama shombo la samaki ingawa huwa hauonyeshi dalili yoyote. Wanawake wanaokuwa na wapenzi wengi (multiple sexual partners) mara nyingi wanakuwa katika hatari ya kupata maambukizi katika uke. Picha: Muonekano wa uchafu utokao ukeni kutokana na maambukizi ya bakteria.

uchafu ukeni

2. Ugonjwa Wa Malengelenge (Trichomoniasis).

Hii ni aina nyingine ya maambukizi katika uke ambayo husababishwa na protozoa aitwae Trichomonas Vaginalis. Maambukizi haya mara nyingi huenezwa kwa njia ya kujamiiana lakini pia unaweza kuenezwa kwa kuchangia taulo ama brashi la kuogea. Dalili za ugonjwa huu huonekana katika uchafu wenye rangi ya njano au kijani ambao huwa una harufu mbaya. Pia huwa kuna dalili za maumivu, uvimbe sehemu za mashavu ya uke kwa ndani ama nje, muwasho n.k, japo wengine huwa hawaonyeshi dalili zozote.

3. Maambukizi Ya Fangasi Ukeni.

Maambukizi ya fangasi ukeni hutoa dalili za uchafu mweupe wenye utando kama maziwa mgando pamoja na muwasho na hali kama ya kuungua moto ukeni. Hali ya kuwepo kwa fangasi ukeni huwa ni ya kawaida lakini ukuaji wake unaweza kuongezeka na kushindikana kwa hali fulani. Mambo yafuatayo yanaweza kuongeza hatari ya maambukizi ya fangasi ukeni: Msongo wa mawazo, kisukari, vidonge vya mpango wa uzazi, ujauzito, madawa ya vidonge ikiwa yanatumiwa Zaidi ya miaka 10.

4. Kisonono (Gonorrhea) Na Pangusa (Chlamydia).

Kisonono na pangusa ni maambukizi ya magonjwa ya zinaa ambayo yanaweza kusababisha kutokwa na uchafu usio kuwa wa kawaida ambao mara nyingi huwa wenye rangi ya njano, kijani au kijivu.

5. Maambukizi Ya Bakteria Katika Uke (Pelvic Inflammatory Disease-PID).

Maambikizi ya bakteria katika uke nayo pia huenezwa kwa njia ya kujamiina. Huonekana wakati bakteria wanapooenea kwenye uke hadi kwenye viungo vya uzazi. Maambukizi haya yanaweza kumfanya mwanamke kutokwa na uchafu mzito wenye harufu mbaya.

6. Saratani Ya Shingo Ya Kizazi (Cervical Cancer).

Maambukizi haya ambayo pia huenezwa kwa njia ya ngono yanaweza kusababisha tatizo la saratani ya shingo ya kizazi. Ingawa kunaweza kusiwepo na dalili zozote lakini aina hii ya saratani inaweza kutoa damu, uchafu wa kahawia au majimaji yenye harufu mbaya. Saratani ya shingo ya kizazi inaweza kuzuiwa kwa urahisi kabisa baada ya kupima maambukizi ya virusi waitwao Human Papilloma Virus (HPV) ambao ndio husababisha ugonjwa huu.

Aina Za Uchafu Unaotoka Ukeni:

Zipo aina mbalimbali za uchafu unaotoka ukeni. Aina hizi hutofautiana katika rangi na muonekano. Baadhi ya uchafu unaotoka huwa wa kawaida lakini mwingine unaweza kuonyesha hali ya utando ambao unahitaji matibabu.

1. Uchafu Mweupe ukeni.

Uchafu mweupe kidogo hasa unaotoka mwanzoni mwa mzunguko wa hedhi kwa mwanamke huwa ni wa kawaida. Hata hivyo ikiwa uchafu huu utaambatana na muwasho na una ute kama maziwa ya mgando, huu sio wa kawaida na unahitaji matibabu.

Sababu ya kutoka uchafu mweupe ukeni.

Aina hii ya uchafu ukeni yaweza kuwa dalili ya maambukizi ya fangasi.

Picha: Muonekano wa uchafu mweupe utokao ukeni.

uchafu mweupe

2. Uchafu Mwepesi Wa Majimaji.

Uchafu mwepesi wa majimaji huwa ni wa kawaida na unaweza hukaonekana muda wowote ndani ya mwezi. Unaweza kuwa mzito wakati mwingine hutokana na mazoezi au kazi nzito. Picha: Muonekano wa uchafu mwepesi wa majimaji kwenye nguo ya ndani (chupi).

uchafu mwepesi wa majimaji

3. Uchafu Mweupe Wenye Kuvutika.

Uchafu ukeni unapokuwa mweupe lakini wenye utando na wenye muonekano kama makamasikamasi kama vile ute wa yai, ni ishara ya kwamba mwanamke yuko katika hali ya siku za hatari. Hii huwa ni aina ya kawaida ya uchafu utokao ukeni. Picha: Muonekano wa uchafu mweupe wenye kuvutika.

uchafu mweupe wenye kuvutika

4. Uchafu Wa Kahawia ukeni.

Uchafu wa kahawia au wenye damu mara nyingi huwa ni wa kawaida hasa unapoonekana baada ya kutoka hedhini. Uchafu unaochelewa kutoka baada ya hedhi unaweza kuonekana wa kahawia badala ya kuwa na rangi nyekundu. Pia unaweza ukaona kiwango kidogo cha uchafu wenye damu katikati ya mwezi ambao huwa kama matone ya damu. Kama matone ya damu yanatoka katika kipindi cha kawaida na umekuwa ukifanya tendo la ndoa na mpenzi wako bila kutumia kinga basi hii inaweza kuwa dalili ya Ujauzito. Kutokwa na matone ya damu wakati wa awali wa ujauzito yaweza kuwa ishara ya kuporomoka kwa mimba hivyo yafaa kumuona daktari mapema sana hospitali.

Lakini kwa upande mwingine, uchafu unaotoka ukeni wenye rangi ya njano au damu unaweza kuwa ishara ya tatizo la saratani ya shingo ya kizazi (cervical cancer). Ndio mana wanawake wanashauriwa kupata vipimo vya saratani ya shingo ya kizazi kila mwezi. Picha: Muonekano wa uchafu wenye rangi ya kahawia/wenye damu.

uchafu wenye rangi ya kahawia/damu

5. Uchafu Wa Njano/Kijani.

Uchafu wa njano au kijani hasa unapokuwa na mabonge ama uliombatana na harufu mbaya huwa sio wa kawaida. Aina ya uchafu huu yaweza kuwa dalili za maambukizi ya ugonjwa wa malengelenge (Trichomoniasis) ambao kwa kawaida husambaa ama kuenea kwa njia ya Kujamiiana. Picha: Muonekano wa uchafu wa njano/kijani kwenye nguo ya ndani (chupi).

uchafu wa njano/kijani

Soma pia hizi makala:

HITIMISHO:

Unapoona dalili za kutokwa na uchafu ukeni usiokuwa wa kawaida pamoja na dalili zingine kama vile homa, maumivu ya tumbo chini ya kitovu, kupungua kwa uzito wamwili, uchovu, au kukojoa mara kwa mara, basi yafaa ufike hospitali umuone daktari haraka Iwezekanavyo. Lakini pia tumekuandalia programu maalumu ya kutumia virutubisho lishe vilivyotokana na mimea na matunda kwa wale wanaosumbuliwa na maambukizi ya fangasi ukeni. Ikiwa utahitaji virutubisho lishe kwa ajili ya kutibu maambukizi ya fangasi ukeni wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487.

Lakini pia, kwa uhitaji wa updates, vitabu (e-books) bure kuhusu afya jisajili (subscribe) kupitia email yangu kwa kubonyeza hii link: https://isayafebu.beehiiv.com/subscribe

Ni mimi mwenye kujali afya yako Dr. ISAYA FEBU.

vipimo vya mfumo wa uzazi