Kuwashwa Sehemu Za Siri Kwa Mwanamke husababishwa Na Nini?

Kuwashwa sehemu za siri kwa wanawake ni miongoni mwa changamoto za kiafya zinazowasumbua wanawake wengi bila kujali rika lao.

Tatizo la kuwashwa sehemu za siri kwa wanawake ni kubwa na hupelekea mwanamke kupata matatizo ya kisaikolojia kwa kuwa mara nyingi inakuwa vigumu wakati mwingine kusema kwa daktari kwamba nina tatizo sehemu zangu za siri.

Kuwashwa Sehemu Za Siri

Leo katika makala yetu tutazungumzia sababu zinazopelekea mwanamke kuwashwa sehemu za siri.

Sababu Zinazopelekea Mwanamke Kuwashwa Sehemu Za Siri:

Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazopelekea mwanamke kuwashwa sehemu za siri ambazo ni pamoja na;

1) Maambukizi Ya Fangasi Ukeni.

Maambukizi ya fangasi ukeni hujulikana kwa kitaalamu kama yeast infection. Maambukizi haya ni moja ya tatizo kwa wanawake linalosababishwa na fangasi waitwao candida albicans.

Dalili kuu za maambukizi haya ni pamoja na kuwashwa ukeni, kuvimba na kutoa uchafu mweupe kama maziwa ukeni.

Soma pia hii makala: Fangasi Ukeni Kwa Mjamzito: Kisababishi, Dalili, Matibabu, Madhara Na Jinsi Ya Kujikinga.

2) Ugonjwa Wa Kuvimba Uke.

Ugonjwa wa kuvimba uke hujulikana kwa kitaalamu kama vulvovaginitis.

Huu ni ugonjwa unaoathiri kwa kuvimbisha sehemu za nje za uke na uke wenyewe. 

Dalili kuu za ugonjwa huu ni pamoja na kuwashwa ukeni, mkojo kuuma na kukereketa wakati wa kukojoa na kutokwa na uchafu ukeni.

3) Kuvimba Uke Baada Ya Hedhi Kukoma.

Kuvimba uke baada ya hedhi kukoma hujulikana kwa kitaalamu kama  Postmenopausal Atrophic Vaginitis.

Huu ni ugonjwa wa kuvimba uke baada ya hedhi kukoma, hali hii huongeza maambukizi ukeni na huweza kusababisha muwasho ukeni na maumivu wakati wa tendo la ndoa.

4) Maambukizi Ya Trikomonasi (Trichomoniasis).

Maambukizi ya Trikomonasi (Trichomoniasis) ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na kimelea aitwaye Trichomonas vaginalis. Dalili kuu za ugonjwa huu ni pamoja na muwasho ukeni na kutokwa na uchafu ukeni.

Trichomonas vaginalis

5) Ugonjwa Wa Minyoo.

Ugonjwa wa minyoo hujulikanao kwa kitaalamu kama pinworm infection ni maambukizi ya minyoo wadogo sana wenye umbo la pini wanaoweza kuambukiza utumbo na kusambaa maeneo mbalimbali. Ugonjwa huu huwatokea sana watoto wa kati ya miaka 5 na 10.

pinworms

6) Genital Warts.

Hivi ni vinyama vidogo vinavyoota kwenye ngozi au utando laini unaozunguka maeneo ya sehemu za siri.

Ugonjwa huu uenezwa kwa njia ya kujamiana na unasababishwa na virusi viitwavyo Human Papilloma Virus (HPV). Vinyama hivi vidogo vinavyoota kwenye ngozi au utando laini unaozunguka maeneo ya sehemu za siri vinaweza sababisha muwasho na maumivu.

7) Saratani Ya Sehemu Ya Nje Ya Uke.

Saratani ya sehemu ya nje ya uke ijulikanayo kwa kitaalamu kama vulvar cancer ni saratani ya sehemu ya nje ya uke inayo ambatana na kuwashwa sehemu ya nje ya uke.

vulvar cancer

8) Kisukari.

Huu ni ugonjwa sugu wa kimetaboliki unaosababishwa na kasoro katika utengenezaji wa Insulin au utendaji kazi wake. Kisukari kilichokomaa kinaweza sababisha maumivu ya tumbo, kichefuchefu, kizunguzungu na kuwashwa sehemu za siri.

9) Urethritis.

Haya ni maambukizi kwenye urethra (mrija wa kutolea mkojo nje ya mwili). Maambukizi haya yanasababisha kuvimba kwa urethra. Dalili kuu za maambukizi haya ni pamoja na mkojo kuchoma, maumivu ya tumbo chini ya kitovu, kutokwa uchafu na kuwashwa sehemu za siri.

Kumbuka:

Jinsi Ya Kutambua Kisababishi Cha Muwasho Sehemu Za Siri Kwa Mwanamke:

Ili uweze kutambua kisababishi cha muwasho ukeni, unatakiwa kufahamu vizuri kuhusu sifa za ya magonjwa yaliyoandikwa hapo juu haswa dalili zake na mwonekano wake na wakati mwingine unahitaji kuthibitisha kwa vipimo. Daktari wako anaweza kutambua kwa kuchukua historia yako na kufanya uchunguzi wa awali ukeni au kuagiza vipimo kufanyika.

Matibabu Ya Kuwashwa Sehemu Za Siri Kwa Mwanamke:

Endapo una muwasho ukeni, wasiliana na daktari wako kwa uchunguzi na tiba kabla ya kutumia dawa yoyote.

Kwa sababu kuna visababishi vingi vya miwasho ukeni, baada ya daktari wako kuchukua historia ya tatizo lako na kukufanyia vipimo atakupa tiba kutokana na kisababishi. Dawa utakazopewa zinaweza kuwa za kupunguza dalili ya muwasho na dawa za kutibu maambukizi ukeni au dawa za kutibu maambukizi tu.

 Dawa zifuatazo huficha muwasho ukeni lakini kamwe hazitibu kisababishi;

  • Hydrocortisone cream
  • Diphenhydramine
  • Benzocaine
  • Ciclosporin
  • Triamcinolone
  • Doxepin
  • Fluoxetine
  • Sertraline

Endapo maambukizi ya fangasi ndio kisababishi cha muwasho ukeni, dawa za antifango zitatumika. Zinaweza kuwa kati ya;

  • Terbinafine
  • Butenafine
  • Clotrimazole cream
  • Miconazole
  • Ketoconazole
  • Econazole
  • Luliconazole
  • Naftifine
  • Oxiconazole
  • Tolnaftate
  • Ciclopirox
  • Itraconazole
  • Sulconazole
  • Griseofulvin

Kumbuka:

Jinsi Ya Kujikinga Na Tatizo La Kuwashwa Sehemu Za Siri Kwa Mwanamke:

Mwanamke anapaswa kufanya mambo yafuatayo ili kujikinga na tatizo la kuwashwa sehemu za siri ambayo ni pamoja na;

1) Baada ya kukojoa au kujisaidia osha sehemu zako za siri kuanzia mbele (ukeni) kwenda nyuma (makalio) ili kuzuia bakteria kutoka njia ya haja kubwani kuingia ukeni.

2) Epuka matumizi ya vitu vyenye kemikali kama marashi ya uke katika kusafisha uke kwa maana uharibu hali ya asidi ya uke na kuua bakteria wanaolinda uke na kufanya iwe rahisi kushambuliwa na maradhi sehemu za siri.

3) Weka sehemu zako za siri katika usafi na ukavu, tumia sabuni kidogo katika kusafisha sehemu zako za siri na maji mengi. Kausha sehemu zako za siri kila baada ya kuoga au kuogelea na epuka kukaa na nguo mbichi kwa muda mrefu.

4) Vaa nguo isiyobana sana, iliyotengenezwa kwa pamba ili unyevunyevu usitokee na badili nguo za ndani (chupi) kila baada ya masaa 24.

5) Epuka ngono bila kuvaa mpira (kondomu) hasa ukiwa na hofu na mpenzi kuwa ana maradhi.

HITIMISHO:

Kwa msaada wa ushauri, vipimo na tiba ya magonjwa ya afya ya uzazi kwa wanaume na wanawake wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487.

vipimo vya mfumo wa uzazi