Zijue Dalili Za Pid Sugu.

PID sugu ni hali ambapo maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke yameendelea kwa muda mrefu au yamekuwa yakijirudia mara kwa mara.

Pid Sugu

Dalili za PID sugu zinaweza kuwa sawa na zile za PID ya kawaida lakini zinaweza kuwa kali zaidi na mara nyingi huleta madhara ya kudumu kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke. Baadhi ya dalili za PID sugu ni pamoja na:

1) Maumivu ya mara kwa mara au ya kudumu katika eneo la chini ya kitovu

2) Kupata maumivu ya mgongo

3) Kupata utoko mchafu sehemu za siri, utoko huu huambatana na harufu mbaya

4) Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa

5) Kupata maumivu/kutokwa na damu wakati wa tendo la ndoa 

6) Kutokwa damu bila mpangilio wakati wa hedhi

7) Kupata homa

8) Wakati fulani kuhisi kichefuchefu kama mwanamke mjamzito na kutapika

Soma pia hii makala: “Jinsi Ya Kutokomeza P.I.D Bila Ya Kuchoma Sindano…

HITIMISHO:

Kumbuka kwamba dalili hizi zinaweza kutofautiana kwa kila mwanamke na mara nyingine zinaweza kuwa za kudumu au kutoweka kwa muda fulani kabla ya kujirudia.

Ni muhimu kuonana na daktari ili kufanya vipimo na kutambua matibabu sahihi ikiwa una wasiwasi wowote kuhusu PID au maambukizi ya muda mrefu ya mfumo wa uzazi.

Matibabu sahihi ni muhimu ili kuzuia madhara zaidi kwa afya yako ya uzazi.

vipimo vya mfumo wa uzazi