Mvurugiko wa mzunguko wa hedhi ni tatizo ambalo huanza ghafla au polepole ambapo mwanzo mwanamke alikuwa akipata siku zake katika utaratibu unaoeleweka lakini mara haelewi au hajielewi namna mzunguko wake unavyoenda.
Mvurugiko wa mzunguko wa hedhi ni kitendo cha mwanamke kuanza kuona siku zake bila mpangilio maalumu na matokeo yake ni kuwa mwanamke atashindwa kutimiza malengo yake ya uzazi kwa kutumia mzunguko huo kwa sababu ya kutokueleweka.
Mvurugiko wa mzunguko wa hedhi unaweza kupelekea ghafla tu ukapata hedhi mahali usipotarajia jambo litakalokufanya ubaki na woga na huelewi nini cha kufanya kwani hukuwa umejiandaa kwa tukio hilo. Wakati mwingine unaweza kupitiliza mwezi hata miezi kadhaa bila kuona kabisa siku zako na hata ukipima ujauzito unakutwa huna ujauzito wala dalili za ujauzito huna.
Madhara ya kuvurugika kwa mzunguko ni pamoja na;kushindwa kupata ujauzito, maambukizi katika kizazi na kuziba kwa mirija ya uzazi.
Mchoro wa mzunguko wa hedhi/Duara la mzunguko wa hedhi:
Soma pia hii makala: Mambo 4 Usiyo yajua Kuhusu Mvurugiko Wa Homoni Kwa Wanawake.
Faida Za Kuwa Na Mzunguko Wa Hedhi Ulio Sawa:
Mzunguko wa hedhi ulio sawa utamsaidia mwanamke kufanya yafuatayo;
a) Kupata ujauzito alioupangilia.
b) Kuepuka kupata ujauzito ambao hakuupangilia.
c) Kuamua jinsia ya mtoto anayemtaka.
Visababishi Vya Mvurugiko Wa Mzunguko Wa Hedhi:
Ni rahisi kugundua kama mzunguko wako wa hedhi umevurugika ikiwa tu unaufahamu vizuri mzunguko wako wa hedhi ulio sahihi. Kufahamu mzunguko wako unahitaji uifahamu siku ambayo ulianza kuona damu hadi siku utakapoona tena katika mzunguko unaofuata. Karibu kila mwanamke huwa na mzunguko wake wa hedhi usiofanana na wa mwanamke mwingine.
Tatizo linaweza kuanza kwa kurukaruka siku, mwanamke pia anaweza kupoteza siku yaani mwezi mwingine anaona na mwezi mwingine haoni, au anaingia mara mbili kwa mwezi au anaona damu ya hedhi kwa siku nyingi hata zaidi ya siku arobaini mfululizo. Damu yake inaweza kutokea kidogo kidogo kila siku au nyingi huku ikiambatana na mabonge mabonge na maumivu pia. Maumivu haya ya wakati wa hedhi huenea chini ya tumbo mpaka miguuni na kiunoni ambayo kitaalamu hujulikana kama “dysmenorrhea”.
Kuvurugika kwa hedhi kunaweza kutokea kutokana na sababu zifuatazo;
A) Mabadiliko Ya Mazingira.
Mabadiliko ya mazingira hupelekea mfumo wa mwili hubadilika pia hali ambayo kitalaamu hujulikana kama “adaptive mechanism”, hasa mwanamke akitoka sehemu ya joto kwenda mikoa ya baridi au toka mikoa ya baridi kwenda mikoa ya joto.
B) Msongo Wa Mawazo (Depression).
C) Hofu.
D) Mabadiliko Ya Kisaikolojia.
E) Uvimbe Kwenye Kizazi.
F) Matatizo Kwenye Mfumo Wa Homoni.
G) Matatizo Kwenye Vifuko Vya Mayai.
H) Mimba Kuharibika.
I) Maambukizi Sugu Kwenye Kizazi.
Jinsi Ya Kurekebisha Mvurugiko wa Mzunguko Wa Hedhi:
Kabla ya yote unapopatwa na tatizo hili kwa muda mrefu ni vizuri ukaonana na daktari uweze kupata uchunguzi wa kutosha kubaini nini hasa inaweza kuwa ndiyo sababu hasa ya tatizo kwa upande wako. Pia hospital unaweza kupewa vidonge vya uzazi ili kurekebisha hedhi yako.
Ila pia unaweza kutumia vyakula Vifuatavyo kama njia mbadala ya kurekebisha mvurugiko wa mzunguko wako wa hedhi uwapo katika mazingira yako ya nyumbani;
1. Papai.
Papai ni moja ya chakula kizuri sana katika kutibu tatizo la kuvurugika kwa hedhi. Papai Iina viinilishe muhimu kama carotene, chuma ( iron), Kalsium (calcium),vitamini A na C ambavyo husaidia kulainisha na kunywea kirahisi kwa kuta za mji wa uzazi.
Unashauriwa kula papai kila siku, nusu papai au papai zima kutegemea na ukubwa wake au uwezo wako. Lakini pia unashauriwa kutumia papai katika mlo wako wa kila siku sio mpaka uugue.
2. Mdalasini.
Mdalasini unayo sifa ya kuondoa tatizo la damu kuganda sifa inayoweza kusaidia kuondoa tatizo la maumivu wakati wa hedhi. Mdalasini ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi (fibers), kalsiamu (calcium), chuma (iron) manganizi (manganese).
Jinsi Ya Kutumia Mdalasini Kutibu Mvurugiko Wa Mzunguko Wa Hedhi;
Changanya kijiko kidogo kimoja cha mdalasini ya unga na kijiko kidogo kimoja cha asali katika glasi moja ya maji ya uvuguvugu na unywe kutwa mara 2 siku za mwanzoni unapoanza au kukaribia kuingia katika siku zako.
3. Tangawizi.
Tangawizi ni dawa ya asili yenye maajabu katika kutibu tatizo la mvurugiko wa hedhi. Tangawizi hufanya kazi mhimu kabisa katika kushusha kiwango cha homoni inayosababisha maumivu ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘prostaglandins’. Tangawizi husaidia pia katika kupigana na uchovu uletwao na mzunguko wa hedhi katika siku zile za mwanzo au siku 2 hivi kabla ya kuanza siku zako na huweza pia kufanya mzunguko usio sawa wa hedhi kuwa sawa.
Jinsi Ya Kutumia Tangawizi Kutibu Mvurugiko Wa Mzunguko Wa Hedhi;
Tengeneza chai ya tangawizi ukitumia tangawizi mbichi, kunywa kikombe kimoja kutwa mara 3 wakati wa siku zako au siku yoyote tu kama kinga. Kamulia ndimu kidogo ndani yake na utumie asali kupata radha badala ya sukari. Unaweza pia kuongeza tangawizi kwenye vyakula na mboga mboga nyingi unazopika kila siku.
4. Mrehani (Basil).
Mrehani au Basil kwa Kiingereza ni mmea mwingine mzuri sana katika kuondoa maumivu wakati wa hedhi na kurekebisha mzunguko wa hedhi kwa ujumla. Mmea huu unatumika sana jikoni kwenye mahotel ya kitalii Dar na Zanzibar. Unao sifa kuu ya kuzuia au kuondoa maumivu mwilini.
Jinsi Ya Kutumia Mrehani Kutibu Mvurugiko Wa Mzunguko Wa Hedhi;
Ongeza kijiko kikubwa kimoja cha majani freshi ya mrehani yaliyokatwakatwa na kisu (chop) kwenye kikombe kimoja cha maji ya moto, funika vizuri na usubiri ipowe. Kunywa yote ikishapoa na ufanye zoezi hili kutwa mara 3 kwa wiki 3 mpaka 4 au mpaka tatizo lako limeisha.
Tengeneza juisi ya majani haya. Yatwange kwenye kinu au kwenye blenda ya umeme kupata majimaji yake kisha chota vijiko vya chai viwili uweke ndani ya kikombe kimoja cha maji ya moto na unywe yote. Fanya zoezi hili kutwa mara 3. Unaweza pia kuongeza majani freshi ya mrehani kwenye vyakula vingi unavyokula kila siku.
5. Maji Ya Kunywa.
Matatizo ya kiafya karibu yote mwilini chanzo chake kikubwa ni mwili kutokuwa na maji ya kutosha. Jitahidi ujijengee desturi ya kunywa maji mengi walau lita 2 mpaka lita 3 kila siku.
HITIMISHO:
Mvurugiko wa mzunguko wa hedhi mara nyingine husababishwa na mvurugiko wa homoni. Mvurugiko wa homoni kwa wanawake ni kitendo cha kuongezeka au kupungua kwa homoni katika mwili wa mwanamke, hivyo kufanya mabadiliko katika mwili wa mwanamke. Hivyo ikiwa changamoto yako ya mvurugiko wa mzunguko wa hedhi imetokana na mvurugiko wa homoni tunakushauri utumie virutubisho vilivyotokana na mimea na matunda, virutubisho hivi vitamaliza kabisa changamoto yako na kukurudisha katika hali yako ya awali ya kupata hedhi katika mpangilio mzuri. Kupata virutubisho hivyo wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487.
Leave a Reply