Ukomo wa hedhi kwa wanawake ni mabadiliko ya asili ya mwili yanayowatokea wanawake kwa sababu ya kupungua kwa kiwango cha homoni ya kike ‘’estrojeni’’. Ukomo wa hedhi kwa wanawake hujulikana kwa kitaalamu kama Menopause.
Mwanzoni, damu ya hedhi inaanza kuwa nyepesi, baadae inaanza kukosekana kabisa kwa baadhi ya miezi na hatimae inakoma kabisa kutoka. Mwanamke husemekana kuwa amefikia ukomo wa hedhi kama hajapata hedhi kwa angalau mwaka mmoja. Baadhi ya wanawake hawapati dalili zozote, lakini kuna wengine wanapata matatizo mbalimbali kwa sababu ya ukomo wa hedhi, hii ni pamoja na kupatwa na vipindi vya joto la mwili kupanda ghafla, kuvuja jasho jingi sana usiku na ukavu wa uke.
Kukoma hedhi hutokea pale ovari zinapokuwa na umri mkubwa na kuzalisha kwa kiwango kidogo homoni ambazo haziwezi kufanya kazi zake kama mwili unavyotaka au unavyohitaji.
Mwili huanza kupata mabadiliko mbalimbali yatokanayo na uzalishaji mdogo wa homoni ya Estrogen, progesterone, testosterone, follicle Stimulating Hormone (FSH) na Luteinizing Hormone (LH).
Soma pia hizi makala:
Mojawapo ya dalili inayoonekana mapema ni kupotea kwa vifuko vya mayai (ovarian follicles) ambavyo husaidia kuzalisha mayai ya mwanamke kwenye ukuta wa ovari hivyo kuruhusu mzunguko Wa damu au kutungika kwa mimba kutokea.
Ukomo Wa Hedhi Ni Miaka Mingapi?
Kwa kawaida mwanamke anafikia ukomo wa hedhi akiwa na miaka 45 mpaka 55. Japo wanawake wengi huwa wanaacha kupata hedhi katika umri wa miaka 51.
Kumbuka: Mwanamke anaweza kukoma kupata hedhi kwa muda kama mimba ilitoka, alijifungua kabla ya muda au alijifungua kwa njia ya upasuaji.
Hata hivyo tafiti zinaonesha baadhi ya wanawake bado wanapata hedhi hatakama wana umri wa miaka 60 ingawa kwa kawaida wanapaswa kuwa wameacha kupata hedhi katika umri wa miaka 45 mpaka 55. Mwanamke anaweza kupata matatizo ya hedhi si kwasababu ni mzee.
Dalili Za Mwanamke Kufika Ukomo Wa Hedhi:
Kuna mambo mengi ambayo yanaweza kukusaidia kuweza kujua lini utaanza kikomo cha hedhi ikiwa ni pamoja na sababu za kijenetiki na afya ya ovari kwa ujumla.
Perimenopause huanza au hutokea kabla ya menopause na hiki ni kipindi ambacho homoni huanza kubadilika kujiandaa kwa ajili ya menopause.
Inaweza kuanza muda wowote kwa miezi michache mpaka miaka kadhaa. Wengi Wa wanawake huanza Perimenopause baada au wakati wa miaka yao ya 40 ingawa wengine wanaweza wasipitie hatua hii na kwenda moja kwa moja kwenye menopause.
Zaidi ya 1% ya wanawake huanza menopause kabla ya miaka 40 na zaidi ya 5% huanza menopause kati ya miaka 40 na 45 na hii kitaalamu hujulikana kama Early/Premature Menopause.
Wakati Wa perimenopause hedhi hutokea lakini inakuwa sio ya kawaida, inaweza ikachelewa, inaweza ikaruka kipindi kimoja nk. Pia damu inaweza kuwa nzito au nyepesi.
Hivyo lazima ujue;
Menopause ni kukosa au kukwama kwa mzunguko wa hedhi kwa zaidi ya mwaka mmoja au miezi 12.
Post menopause ni miaka au kipindi kinachoendelea baada ya menopause kuanza.
Kila menopause kwa mwanamke hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke. Dalili huwa mbaya zaidi pale inapotokea ghafla au ndani ya kipindi cha muda mfupi.
Kuna hali ambazo pia huweza kuathiri afya ya ovari kama kansa au dizaini ya maisha (lifestyle) fulani kama uvutaji wa sigara husababisha kuongezeka kwa muda kwa dalili za menopause kuendelea kuonekana. Zaidi ya dalili na mabadiliko ya menopause, dalili za perimenopause na post menopause zote zinafanana.
Baadhi ya dalili za perimenopause ni pamoja na;
1) Kutotokea kwa hedhi mara kwa kwa mara au miezi kwa miezi.
2) Damu kutoka nzito sana au nyepesi sana ukifananisha na ulivyozoea.
3) Mwili kupata joto la ghafla na kupotea (30sec – 10min)
4) Kutokwa na Jasho usiku mwili mzima.
Kumbuka: Inakadiriwa zaidi ya 75% hupata dalili hizo za Perimenopause wakifikia menopause.
Dalili za menopause zilizozoeleka ni pamoja na;
1) Joto la ghafla mwilini kwa sekunde 30 mpaka Dakika 10 na hali hii huendelea mpaka mwaka mmoja hadi miwili.
2) Kutokwa na jasho jingi mwilini hasa wakati Wa usiku.
3) Ngozi kubadilika rangi na kuwa nyekundu.
4) Kuwa mkavu ukeni.
5) Kukosa usingizi (Insomnia).
6) Usingizi wa mang’amung’amu.
7) Kuwa na mood au muonekano usiokuwa wa kawaida.
8) Maumivu kipindi au wakati wa tendo la ndoa.
9) Kutokwa na damu isiyokuwa ya kawaida (nzito, nyepesi au yenye mabonge).
10) Kukosa nguvu na kulegea.
Dalili zingine zinazoweza kuonekana ni pamoja na: Viungo kuuma, maumivu ya mgongo, matiti kuwa makubwa au kuongezeka saizi, maumivu ya matiti, mapigo ya moyo kwenda mbio, maumivu ya kichwa, kizunguzungu, kuwa na ngozi kavu, kuwasha kwa ngozi, kuongezeka uzito na kunenepeana, kukojoa mara kwa mara, usingizi usioeleweka, kuwa na wasiwasi au hofu, Kupoteza kumbukumbu, Kushindwa kufanya jambo moja kwa wakati na kulimaliza, msongo wa mawazo, kukosa hamu au hisia na tendo la ndoa.
Tiba Ya Ukomo Wa Hedhi:
Hakuna matibabu kamili ya hili tatizo ya ukomo wa hedhi ingawa kuna baadhi ya dawa unaweza kutumia zikasaidia kupunguza baadhi ya dalili na hupatikana hospital au baadhi ya maduka ya dawa au kwa wataalamu wa afya.
HITIMISHO:
Kwa ushauri na tiba ya magonjwa ya afya ya uzazi wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487.
Is there any possibility for woman to conceive during the period of premenopause?
While perimenopause precedes menopause, there is still a menstrual cycle during this time. The menstrual cycle might become more irregular, but as long as a woman is still actively menstruating, there is still a chance of becoming pregnant