Haya Ndiyo Mambo 6 Muhimu Usiyo yajua Kuhusu Saratani ya shingo ya kizazi.

Saratani ya shingo ya kizazi ni aina ya saratani (kansa) inayoshambulia seli zilizoko ndani ya ngozi laini inayozunguka shingo ya kizazi. Shingo ya kizazi (cervix) ni sehemu ya kizazi kati ya uke (vagina) na mji wa mimba (uterus). Shingo ya kizazi ina kazi nyingi ikiwemo; Kupitisha mbegu za kiume kuelekea katika mji wa uzazi na hatimaye mirija ya uzazi (fallopian tubes) ili kupevusha yai (ovum), kupitisha damu ya hedhi, mlango anaopitia mtoto wakati wa kuzaliwa.

Saratani ya shingo ya kizazi hujulikana kwa kitaalamu kama cervical cancer.

saratani ya shingo ya kizazi

Saratani Ya Shingo Ya Kizazi Husababishwa Na Nini?

Saratani ya shingo ya kizazi husababishwa na aina ya kirusi kinachoitwa ‘Human Papilloma Virus’ HPV, kirusi hiki huambukizwa kwa njia ya kujamiiana na mtu mwenye maambukizi.

Soma pia hizi makala:

Tabia Hatarishi Zinazochangia Mwanamke Kupata Saratani Ya Shingo Ya Kizazi:

Zifuatazo ni tabia hatarishi zinazomuweka mwanamke katika hatari ya kupata saratani ya shingo ya kizazi ambazo ni pamoja na;

1) Kuanza ngono katika umri mdogo (chini ya miaka 18).

2) Uvutaji wa sigara.

3) Kuwa na wapenzi wengi au kujamiiana na mtu mwenye wapenzi wengi.

4) Matumizi ya mafuta mengi kwenye chakula au kula vyakula vyenye mafuta kwa wingi.

5) Kutokula mboga za majani na matunda.

6) Upungufu wa kinga mwilini.

Dalili Za Saratani Ya Shingo Ya Kizazi:

Saratani ya shingo ya shingo ya kizazi huanza na kuendelea kwa muda mrefu bila kuonesha dalili zozote. Dalili ambazo zinaweza kujitokeza wakati ugonjwa upo katika hatua za mwisho ni pamoja na;

1) Kutokwa na damu isiyo ya hedhi.

2) Kutokwa na damu ukeni baada ya kujamiiana.

3) Kutokwa na damu ukeni kwa wanawake waliokwisha kukoma hedhi.

4) Damu iliyochanganyikana na majimaji ya uke.

5) Matone ya damu au damu kutoka kipindi kisicho cha hedhi.

6) Kutokwa na majimaji au uchafu ukeni wenye harufu mbaya wakati mwingine ukiwa umechanganyika na damu.

7) Maumivu wakati wa kujamiiana (dyspareunia).

8) Maumivu chini ya tumbo, nyonga na kiunoni.

9) Kukojoa mkojo wenye damu (hematuria).

10) Upungufu wa damu (anaemia).

Namna Ya Kugundua Saratani Ya Shingo Ya Kizazi:

Mara nyingi saratani ya shingo ya kizazi huchukua muda mrefu mpaka kuonesha dalili.

Vipimo vya uchunguzi vinavyofanyika ni pamoja na;

1) Pap Smear.

Kipimo hiki ni rahisi na hakina madhara yoyote. Inashauriwa kufanya kipimo hiki mara moja kwa mwaka.

pap smear

2) Colposcopy.

Hiki ni kipimo kinachotumia darubini (colposcope) kuangalia seli zilizondani ya ngozi inayozunguka shingo ya kizazi.

colposcopy

Tiba Ya Saratani Ya Shingo Ya Kizazi:

Matibabu ya saratani ya shingo ya kizazi hutolewa kulingana na hatua ya ugonjwa.

Ugojwa ukiwa katika hatua za mwanzo huweza kutibika kabisa (ingawa kuna uwezekano wa kujirudia).

Hatua za mwisho za ugonjwa huu huwa haziwezi kupona kabisa. Kinachofanyika mara nyingi ni kutoa matibabu yatayotuliza dalili na maumivu na kumuwezesha mgonjwa kuishi vizuri.

Huduma za matibabu hutolewa kwa njia zifuatazo:

1) Upasuaji katika hatua za mwanzo za ugonjwa.

2) mionzi.

3) Dawa za saratani.

4) Mionzi pamoja na dawa za saratani.

Madhara ya saratani ya shingo ya kizazi:

Yafuatayo ni madhara yanayoweza kutokea endapo magonjwa mwenye saratani ya shingo ya kizazi atashindwa kupata matibabu mapema (advanced cervical cancer complications);

1) Figo kushindwa kufanya kazi (kidney failure).

2) Fistula.

3) Kutokwa na damu kwenye uke.

Jinsi Ya Kujikinga Na Saratani Ya Shingo Ya Kizazi:

Wanawake wanashauriwa kufanya mambo yafuatayo ili kujikinga na saratani ya shingo ya kizazi ambayo ni pamoja na;

1) Kupata chanjo ya ‘Human papilloma virus’.

2) Kuepuka ngono katika umri mdogo.

3) Kuwa na mwenzi mmoja mwaminifu.

4) Kutumia kondomu kila mara unapojamiiana.

5) Epuka kuvuta sigara.

6) Kufanyiwa uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi angalau mara moja kwa mwaka.

7) Tibu kikamilifu magonjwa ya zinaa (STIs).

8) Punguza matumizi ya mafuta mengi kwenye chakula.

HITIMISHO:

Kwa msaada wa ushauri, vipimo na tiba ya magonjwa ya afya ya uzazi kwa wanaume na wanawake wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487.

Ni mimi mwenye kujali afya yako Dr. ISAYA FEBU.

vipimo vya mfumo wa uzazi