Upungufu wa nguvu za kiume ni hali ya kushindwa kufanya mapenzi kikamilifu au kushindwa kusimamisha uume vizuri. Shughuli ya tendo la ndoa huhusisha akili, homoni, neva, hisia na mishipa ya damu, misuli ya uume. Tafiti zinaonesha kuwa katika wanaume watano (5) basi mmoja kati yao ana tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
Upungufu wa nguvu za kiume huashiria kutokuwa sawa kiafya hivyo ni tatizo linalohitaji tiba.
Tatizo hili huwanyima sana watu raha na kupelekea kuwa na mawazo, migogoro katika mahusiano. Watu wenye changamoto hii mara zote wanahitaji dawa zisizo na madhara (virutubisho lishe) vilivyotokana na mimea na matunda na kubadilisha mitindo yao ya kimaisha (lifestyle changes) ili kuweza kurudisha hali zao na kuondoa tatizo.
Dalili Za Upungufu Wa Nguvu Za Kiume:
Zifuatazo ni baadhi ya dalili za upungufu wa nguvu za kiume;
1) Kukosa Hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa.
Tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa mwanaume ni mojawapo ya dalili za upungufu wa nguvu za kiume na linaweza kusababishwa na sababu nyingi sana. Sababu hizo zinaweza kuwa za kimaumbile au kisaikolojia au za mchanganyiko wa sababu za kimaumbile na sababu za kisaikolojia. Baadhi ya sababu za tatizo hili ni pamoja na;
a) Msongo Wa Mawazo (Depression).
Msongo wa mawazo ni ugonjwa wa kisaikolojia unaohusisha hali ya kuwa na mawazo makali kwa muda mrefu yanapelekea kukosa raha kutokana na kujihisi si mtu wa thamani au kukosa starehe katika vitu ulivyozoea kuvifanya na kukufurahisha hapo awali. Mawazo ya namna hii huathiri mwenendo wako wa maisha yako ikiwa ni pamoja na kukosa matamanio ya kimapenzi.
b) Matumizi Ya Madawa Na Pombe.
Matumizi ya baadhi ya madawa na unywaji wa pombe wa kupindukia vinaweza kupelekea tatizo hili la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Madawa yanayochangia tatizo hili ni pamoja na; Madawa ya presha ya kupanda (Anti hypertensive drugs), madawa ya kuondoa msongo wa mawazo, madawa yote yanayozuia ufanyaji kazi au uzalishaji wa testosterone kwa mfano cimetidine, finasteride na cyproterone n.k
c) Mawazo Mengi Na Uchovu.
Matatizo ya kikazi na hadhi yako kazini vinaweza kuchangia kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.Kama unabezwa sana kazini na kujiona hutimizi kazi yako ipasavyo au kama unachoka sana kazini pia vinaweza kupelekea kukosa hamu ya kufanya mapenzi pindi urudipo nyumbani kwani mahusiano ya kimapenzi yanahitaji yatengewe muda wa kutosha.
d) Kuwa Na Umri Mkubwa.
Kiwango cha homoni ya testosterone inayohusika na hisia za kimapenzi kwa mwanaume hupungua kwa asilimia 1-2 kila mwaka kadri mwanaume anavyozidi kuwa na umri mkubwa. Kiwango cha testosterone kikishuka katika mwili wa mwanaume humfanya asiwe na nguvu, ashindwe kutuliza mawazo kwenye jambo alifanyalo na apoteze hamu ya kufanya mapenzi.
e) Mahusiano Yaliyopo Baina Ya Mwanaume Na Mwanamke.
Matatizo ya kimahusiano kati ya mwanaume na mwanamke yana mchango mkubwa sana katika kusababisha tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa, mfano uwepo wa migogoro kati ya mume na mke, ukosefu wa amani na furaha katika mahusiano huchangia sana mwanaume kukosa hamu ya kufanya mapenzi.
Kama mahusiano yako na mpenzi wako yamekuwa ya miaka mingi sana, unaweza kuwa umemzoea mno mkeo kiasi kwamba ukaanza kukosa hamu ya kufanya naye tendo la ndoa. Hili nalo hutokea mara nyingi.
f) Matatizo Ya Kiafya.
Matatizo ya kiafya ya muda mrefu (chronic diseases) husababisha kupungua kwa hamu ya kufanya tendo la ndoa mfano tatizo la kisukari, tatizo la presha, tatizo la moyo, tatizo la kansa ya muda mrefu, na hali ya kuwa na unene uliozidi kiwango (obesity) n.k
2) Kutokuwa Na Uwezo Wa Kurudia Tendo La Ndoa Zaidi Ya Mara Moja.
Mwanaume mwenye changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume akishakamilisha mshindo mmoja wa tendo la ndoa basi anakua hana uwezo tena wa kurudia mshindo mwingine. Hali hii husababishwa na kutokuwepo na mshukumo wa damu wa kutosha kwenye mishipa ya uume.
3) Kutokuwa Na Uwezo Wa Kusimamisha Uume Kabisa.
Kwa kawaida uume wa mwanaume aliyekamilika (rijali) unaposimama, hutakiwa kuwa imara kama msumari, lakini kwa mwanaume mwenye changamoto ya upungufu za nguvu za kiume uume wake hata ukisimama hubakia kuwa lege lege na unaweza kusinyaa wakati wowote.
Tatizo hili ni matokeo ya kulegea kwa mishipa ya uume ambayo ndio huufanya uume usimame barabara.
4) Kuwahi Kufika Kileleni.
Kuwahi kufika kileleni ni hali ambayo inampata mwanaume mwenye changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume ambapo hutoa shahawa kabla ya kuanza tendo la ndoa au muda mfupi tu baada ya kuanza tendo la ndoa, bila yeye mwenyewe kukusudia. Kwa kawaida mtu mwenye tatizo la kuwahi kufika kileleni hutoa mbegu zake za kiume hata baada ya maandalizi kidogo sana.
5) Kuchoka Sana Baada Ya Tendo La Ndoa Na Hata Kukinai Kabisa/Hata Kusikia Kichechefu.
Hii ni moja wapo ya dalili za upungufu wa nguvu za kiume. Hali hii huwapata wanaume wenye changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume ambayo wakati mwingine huambatana na usingizi mzito (Kulala fofofo).
6) Kuhisi Maumivu Wakati Wa Tendo La Ndoa/Baada Ya Tendo La Ndoa.
Hii pia ni moja wapo ya dalili za upungufu wa nguvu za kiume, hali hii huweza kuchangiwa na kauthirika kwa tishu za uume ambazo hutokana na upigaji wa punyeto kupita kiasi.
7) Kuchelewa Sana Kufika Kileleni/Kushindwa Kufika Kileleni Kabisa.
Ni ile hali ya mwanaume kuchukua muda mrefu kutoa manii wakati wa kushiriki tendo la ndoa.
Kwa kawaida mwanaume anatakiwa afike kileleni/kutoa manii kwa muda usiozidi dakika 30 wakati wa kushiriki tendo la ndoa. Kwa hiyo mwanaume anaposhiriki tendo la ndoa na kuchukua muda mrefu bila kufika kileleni anahitaji uchunguzi ili kubaini chanzo cha tatizo.
Soma pia hii makala: Fahamu aina 7 za vyakula vinavyo ongeza kiwango cha mbegu za kiume.
Sababu Za Upungufu Wa Nguvu Za Kiume:
Zifuatazo ni baadhi ya sababu za tatizo la upungufu wa nguvu za kiume;
- Uzito kupita kiasi na unene uliozidi.
- Ulaji holela wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi.
- Uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe.
- Kuwa na mawazo na wasi wasi.
- Kuwa na tatizo la kibofu cha mkojo.
- Matumizi makubwa ya dawa zenye kemikali za kutibu magonjwa kama kansa, vidonda vya tumbo, kisukari, presha, magonjwa ya moyo nk.
- Tabia za kujichua kwa muda mrefu.
- Umri hasa wazee.
Njia Za Kuongeza Wingi Wa Mbegu Za Kiume:
Zifuatazo ni baadhi ya njia za kuongeza wingi wa mbegu za kiume;
1. Kula Lishe Bora.
Chakula unachokula kina mchango mkubwa katika kutibu tatizo la kuwa na kiwango kidogo cha mbegu za kiume(Low sperm count). Kama utarekebisha tu aina ya chakula unachokula kunaweza kupelekea kutibu changamoto ya kuwa na kiwango kidogo cha mbegu za kiume ambapo unashauriwa kupunguza matumizi ya sukari na vyakula vya ngano, badala yake ongeza zaidi matumizi ya matunda, mboga mboga. Hii inaweza kukusaidia kutibu tatizo la kuwa na kiwango kidogo cha mbegu za kiume kwa haraka sana.
2. Epuka Matumizi Yaliyokithiri Ya Vyakula/Vinywaji Vyenye Kafeini Kwa Wingi.
Kama unasumbuliwa na tatizo la kuwa na kiwango kidogo cha mbegu za kiume ni vyema ukaepuka matumizi yaliyokithiri ya vyakula au vinywaji vyote vyenye kafeini kwa wingi. Mfano wa vyakula/vinywaji vyenye kafeini kwa wingi ni pamoja na chai ya kahawa, soda nyeusi zote, malta, redbull, chokoleti n.k
3. Tumia Kitunguu Swaumu Kwa Wingi.
Kitunguu swaumu kina ‘Selenium’ na pia kinasaidia kuondoa sumu mwilini, mambo haya mawili muhimu yanasaidia kuongeza spidi ya mbegu za kiume. Pia kitunguu swaumu kina ‘Allicin’ ambayo husaidia kuongeza msukumo wa damu kwenda kwenye uume. Hivyo unashauriwa kuongeza matumizi ya kitunguu swaumu kwenye chakula unachopika. Vile vile unaweza kutafuna punje 2 mpaka 3 za kitunguu swaumu kila unapoenda kulala au unaweza kukatakata (chop) hizo punje 2 au 3 vipande vidogo vidogo kisha unywe na maji.
4. Ulaji Wa Ndizi.
Ndizi ni chakula kizuri kwa ajili ya afya ya uume wako. Ndizi zina kimeng’enya kimoja kiitwacho ‘Bromelain’ ambacho husaidia kuziweka sawa homoni zinazohusiana na tendo la ndoa (testosterone). Pia ndizi zina Magnesium, vitamini B1 na vitamini C, vitu ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya kutengeneza mbegu za kiume.
5. Ulaji Wa Mbegu Za Maboga.
Mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini ya zinki ambayo ni muhimu katika kutengenezwa kwa mbegu za kiume na homoni ya testosteroni. Pia mbegu za maboga zina vitamini B, C, D, E, na K ambazo zote ni muhimu katika kuongeza idadi ya mbegu za kiume. Vile vile mbegu za maboga zina madini ya kalsiamu, Potasiamu, Phosphorasi na Niacin.
6. Ulaji Wa Mboga Za Majani Kwa Wingi.
Mboga za majani zinapunguza homoni ya ‘estrogen’ na hivyo kufanya homoni ya ‘testosterone’ ipatikane kwa wingi na hivyo kupelekea kuongezeka kwa mbegu za kiume.
7. Ulaji Wa Vyakula Vyenye Foliki Asidi Kwa Wingi.
Vyakula vyenye foliki asidi kwa wingi ni pamoja na karoti, Parachichi, Ufuta, maharage, papai, bamia. Hivvyo isipite siku bila kula parachichi walau moja na kutafuna karoti walau moja ikiwa unachangamoto ya kuwa na kiwango kidogo cha mbegu za kiume. Tafiti zinaonesha kuwa wanaume walioongeza ulaji wa vyakula vyenye foliki asidi na zinki waliongeza uwingi wa mbegu zao za kiume kwa zaidi ya asilimia 74 kwa muda wa wiki 2 tu.
8. Kunywa Maji Mengi Kila Siku.
Hili ni suluhisho rahisi lisilohitaji gharama yoyote kwa wale wanaosumbuliwa na changamoto ya kuwa na kiwango kidogo cha mbegu za kiume. Kutokunywa maji ya kutosha kila siku kuna uhusiano wa moja kwa moja na kupungua kwa uwingi wa mbegu za kiume. Hivyo kama utatekeleza njia zote zilizotajwa hapo juu halafu ukasahau kunywa maji hesabu umekosea sana. Kutegemeana na uzito wako unaweza kunywa maji walau lita 2 mpaka lita 3 kwa siku, hii itakusaidia kwani mbegu za kiume zimetengenezwa kwa maji, na pia zipo kwenye hali ya kimiminika.
9. Parachichi.
Parachichi lina uwezo mkubwa wa kuzalisha vitamin E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni za kiume. Tafiti zinaonesha kuwa watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwa na msisimko mkubwa wa kimapenzi.
10. Tikiti Maji.
Matunda haya pia yana uwezo mkubwa wa kuongeza nguvu za kiume. Tikiti lnapaswa kuliwa pamoja na mbegu zake, angalau vipande viwili au vitatu kwa siku.
11. Komamanga.
Haya ni aina ya matunda ambayo ndani yake yana mbegu nyekundu. Koma manga lina tajwa kuwa na virutubisho muhimu vya kusisimua misuli ya uume na kuamsha hisia za kushiriki tendo la ndoa.
12. Pweza Na Chaza.
Aina hizi za viumbe wa baharini, huwa na madini ya zinki na chumvi ambayo ambayo yanatajwa kusaidia uzalishaji wa vichocheo vinavyosababisha msisimko wa mwili wakati wa tendo la ndoa. Unashauriwa kujenga utaratibu wa kunywa supu ya pweza mara kwa mara na matokeo yake utayaona.
13. Pilipili.
Pilipili zina uwezo mkubwa wa kumaliza changamoto ya upungufu wa mguvu za kiume. Unaweza kuchangaya pilipili kwenye chakula au ukala hivyo hivyo kwa kutafuna kiasi kidoogo mara kwa mara. Pilipili zina virutubisho ambavyo husaidia kuongeza msukumo wa damu kwenye mishipa ya uume na kuamsha hisia za mapenzi.
14. Kunazi (Blueberries).
Haya ni matunda madogo madogo jamii ya zabibu ambayo huliwa na binadamu. Matunda haya yameelezwa kuwa na nguvu kama ilivyo dawa ya Viagra. Tafiti za kitaalamu zinaonesha kuwa matunda haya yana vichocheo ambavyo hulainisha mishipa ya damu na kufanya damu isambae kwa kasi kuelekea kwenye viungo vya kiume.
15. Ufanyaji Wa Mazoezi Mara Kwa Mara.
Mazoezi ya nusu saa mara tatu kwa wiki kwa wanaume yana uwezo wa kuongeza kiwango cha uzalishaji wa mbegu za kiume kwa mujibu wa wanasayansi ambapo wanaume ambao wameendelea na zoezi la kukimbia kila wakati, mbegu zao za kiume huwa na afya njema kulinganan na watafiti wa jarida la maswala ya uzazi. Watafiti wanasema ni muhimu kufanya mazoezi hayo kwa kiwango cha wastani, kwa sababu mazoezi ya kupita kiasi hudhuru kiwango cha uzalishaji wa mbegu hizo za kiume.
HITIMISHO:
Ikiwa unasumbuliwa na changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume unashauriwa kufanya mazoezi angalau dakika 30 kwa siku, kula vyakula asilia na usipendelee kula vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi, tibu magonjwa yanayokuweka hatarini kama kisukari, magonjwa ya moyo, punguza unene uliozidi, lala vizuri kwa muda mzuri masaa 7 hadi 9, epuka uvutaji wa sigara na matumizi ya pombe yaliyothiri, kunywa maji ya kutosha n.k
Pia kama utahitaji virutubisho lishe vilivyotokana na mimea na matunda kwa ajili ya kutatua changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume bonyeza hapa: “Hii ndiyo Siri Wanayoitumia Wanaume Wengi Kuongeza Nguvu Za Kiume.”
Je Unasumbuliwa Na PID, Fangasi Sugu Au UTI Sugu Kwa Muda Mrefu Bila Kupata Suluhisho La Uhakika?
Kiasi ambacho umeshajikatia tamaa na huelewi ufanye nini ili kutatua changamoto yako inayokunyima usingizi?
Kama jibu ni NDIYO, basi usiwe na wasiwasi kwani nimekuletea suluhisho la changamoto yako…
Huhitaji kuendelea kutumia dawa za mahospitali ambazo umekuwa ukitumia kwa muda mrefu bila kupona…
Suluhisho halisi kwa changamoto yako aidha ni PID, FANGASI SUGU au Uti sugu utalipata kupitia kitabu (soft copy) kitakachokupa muongozo wa kujitibia changamoto yako uwapo mazingira ya nyumbani kwako…
Gharama ya kitabu hicho mara zote ni TZS 10,000/= ila kwa kuwa leo hii ni sherehe ya kumbukizi ya siku yangu ya kuzaliwa (birthday) nitakupatia kwa bei ya OFA ya TZS 3000/= tu (okoa 7,000/= nzima)…
Ili Kupata OFA hiyo Lipia kwenda Tigo Pesa namba 0653211873 (Isaya Febu Msemwa) Kisha nitumie muamala wako WhatsAPP Kwa kubonyeza hapa: https://wa.me/+255625305487
PS: Ofa hii itaisha kesho saa 6:00 mchana, weka oda yako mapema Kwani ukiikosa leo, kuipata tena mpaka mwakani tarehe kama ya leo.
Asante sana kwa elimu hii, ndugu nina tatizo la kutokuwa na hamu ya kuganya mapenzi kabisa, halikadhalika nawahi sana kufika kileleni, uume unasimama lege lege sana. Msaada tafadhali
Unahitaji kutumia virutubisho ambavyo vitatatua kabisa changamoto yako, Kupata virutubisho hiyo Wasiliana nasi kwa simu namba 0625305487
Mbona kila kitu kimeelezwa hapo juu,
Unaweza kusoma upya na ukafuata maelekezo ya wataalamu!
Hey
Nimekupata sana kiongoz
Tatizo
Tiba ipo mkuu
Oky tumehelewa penye tatizo tutazidi kusaidiana
Sawa..karibu sana
Ukitaka kupata vipimo unapataje maan me Niko Zanzibar
Kwa zanzibar tunapatikana mwanakwerekwe, karibu na Sheri ya Gapco
Naomba mnisaidie juu ya changamoto ya nguvu za kiume na kuimalika katika tendo
piga 0625305487
Kwamba KARANGA hazipo kwenye orodha ya vyakula vinavyoongeza sparm sio?
Kuongeza sperm na kuongeza wingi wa mbegu ni vitu viwili tofauti!
Unaweza kuwa Na sperm nying lakn tunaposema sperm count au kiwango cha mbegu kikawa kidogo sana,
Hivyo Kura karanga mbichi kunaimarisha pia wingi wa shahawa na ulinzi wa mbegu za kiume.
Ni muhimu Kula pia hizo karanga mbichi, ongezea hapo
Swala la hormone liko vp hili. au linachangia vp upungufu wa nguvu za kiume
I’m not that much of a internet reader to be honest but your sites really nice, keep it up! I’ll go ahead and bookmark your site to come back down the road. All the best
thanks in advance,,,you’re warmly welcome
I like this every day nitafanya hivi . By following the instructions from doctor isaya
You’re warmly welcome
jamn,naombeni msaada,,jana nilikuwa nafany atendo la ndoa nikaenda raundi moja lakin siku zote naenda zaidi ya raundi hio,,,na nikaamka asubuhi sijaona uume kuamkaa,,je mnanisaidiaje kwa hili,ndugu zangu
Vp docter je tatizo hilo linaweza kufanya uumpe mwanamke mimba
Matatizo ya nguvu za kiume hayamaanishi moja kwa moja kuwa huwezi kumpa mwanamke mimba. Uwezo wa kumpa mwanamke mimba unaweza kutofautiana kutokana na sababu mbalimbali, lakini mara nyingi, hata kama kuna matatizo ya nguvu za kiume, bado inawezekana kwa mwanamume kuwa na uwezo wa kumfanya mwanamke apate mimba. Hata hivyo, masuala ya uzazi yanaweza kuhusisha mambo mengi na inashauriwa kutafuta ushauri wa kitaalam kutoka kwa daktari ili kuelewa zaidi hali yako na njia bora za kushughulikia suala hilo.
Je ukiwa n tatizo hilo una uwezo w kuumpa mwanamke mimba
Matatizo ya nguvu za kiume hayana moja kwa moja uhusiano na uwezo wa kumpa mwanamke mimba. Upungufu wa nguvu za kiume unaweza kuathiri tendo la ndoa, lakini siyo moja kwa moja uzazi. Hata hivyo, inaweza kufanya iwe vigumu kufanya tendo la ngono ambalo ni sehemu muhimu ya kupata ujauzito. Ni muhimu kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari ili kutatua tatizo la nguvu za kiume na kushughulikia masuala ya uzazi ikiwa ni lazima.
Dah me namesoma alafu nishaelewa vyote naweza kufanya lakin hapo kw kuacha sigara sidhan kama nitaweza ila me sijawai kabisa kuvuta sigara me natumia bhang
Inabid uache kaka
Hi there! Do you use Twitter? I’d like to follow you if that would
be okay. I’m definitely enjoying your blog and look forward to new updates.
Follow me on Twitter: @febu_isaya
Kiukweli nimependa somo hili hadi wakati nasoma nilikuwa natabasamu. Na je naomba kuuliza ikiwa haujawahi kufanya mapenzi lakini ikatokea uko na mwanamke akawa na vishawishi vingi vya kukufanya utamani kufanya mapenzi lakini uume ukawa unatoa ute ute na hausimami na uko na hamu hapo inakuaje manake na hilo ni upungufu wa nguvu za kiume?
Hapana…
ushauri wenu ni mzur sana nimeelewa swali langu mimi ninapo shiriki tendo nachelewa kumwanga shahawa pia nikifika kileleni sirudii tena kwa mda ule tatizo ni nini hapo doctor??
Doctor na changamoto ya kutopata stimulation kwa mwanamke nikiwa nakula mzigo sipati utamu WA uke hii changamoto inanifanya nishidwe kufika kileleni je tatizo langu linaweza kutatuliwa nikikutafuta
Ndio…suluhisho la changamoto yako lipo wasiliana nasi kwa simu namba 0625305487
Dct nisha 2mia dawa nyng lkn sija pona sina ya kufanya tendo na ht ni kilazimisha ina simama ikiwa legelege some time ikatae kabisa
Pole sana yusuph faraji, kwa msaada wa tiba nicheki 0625305487
Ht mm nina chnga moto lkn hii yng imezid kiu jumla nisha tumia dawa nyngi lkn bdo sina hamu na tendo pia ina simama ikiwa legevu sana
Na je mnashaaur tutumie virutubisho kwa mda gana ili kuimarisha mbegu after then tufanye tendo
Virutubisho vitumike kwa muda wa mwezi mmoja na wiki kadhaa huku ukiendelea kushiriki tendo la ndoa kama kawaida