Saratani ya matiti ni aina ya saratani inayotokea katika tishu za matiti.
Saratani ya matiti hujulikana kwa kitaalamu kama Breasts cancer.
Sababu za kutokea kwa saratani ya matiti hazijulikani kikamilifu, lakini kuna mambo kadhaa ambayo yanaweza kuongeza hatari ya kupata saratani ya matiti.
Zifuatazo ni sababu na mambo yanayochangia hatari ya kupata saratani ya matiti:
1) Jinsia.
Wanawake wana hatari kubwa zaidi ya kupata saratani ya matiti kuliko wanaume.
Takwimu zinaonesha kwamba katika kila wagonjwa 100 wa saratani ya matiti, mgonjwa 1 huwa ni mwanaume.
Hii ni kwa sababu tishu za matiti za kike zina seli nyingi za kupokea homoni za estrogen na progesterone, ambazo zinaweza kusababisha mabadiliko ya saratani.
2) Umri.
Hatari ya kupata saratani ya matiti huongezeka kadri umri unavyoongezeka.
Wanawake wanaozeeka zaidi wako katika hatari kubwa.
3) Historia Ya Saratani Ya Matiti Katika Familia.
Kama kuna historia ya saratani ya matiti katika familia, hasa kwa mama, dada, au binti, hatari ya kupata saratani ya matiti inaweza kuwa kubwa.
4) Maumbile Na Vinasaba.
Kuna aina fulani za kasoro za maumbile ambazo zinaweza kuongeza hatari ya saratani ya matiti, kama vile uwepo wa mabadiliko katika jeni kama BRCA1 na BRCA2.
5) Mzunguko Wa Hedhi.
Kuanza hedhi mapema au kumaliza hedhi baada ya umri wa miaka 55 kunaweza kuongeza hatari ya saratani ya matiti.
6) Matumizi Ya Dawa Za Kupanga Uzazi.
Kuna ushahidi kuwa saratani ya matiti ina uhusiano na matumizi ya muda mrefu ya vidonge vya kupanga uzazi.
7) Unene Kupita Kiasi Na Lishe Isiyofaa.
Unene kupita kiasi na lishe isiyofaa zinaweza kuongeza hatari ya kupata saratani ya matiti.
8) Uvutaji Wa Sigara Na Unywaji Wa Pombe.
Uvutaji sigara na unywaji wa pombe kupita kiasi kunaweza kuongeza hatari kupata ya saratani ya matiti.
9) Kupata Mimba Katika Umri Mkubwa.
Kupata mimba katika umri mkubwa kunaweza kuongeza hatari ya saratani ya matiti.
10) Maradhi Mengine Ya Matiti.
Matatizo ya matiti, kama vile ugonjwa wa fibroadenoma au ugonjwa wa breast cysts, yanaweza kuongeza hatari ya kupata saratani ya matiti.
Soma pia hizi makala:
HITIMISHO:
Ni muhimu kuelewa kuwa ugonjwa wa saratani ya matiti unaweza kutokea kwa wanawake bila sababu yoyote inayojulikana, na pia unaweza kutokea kwa wanawake wenye sababu nyingi za hatari.
Kwa hiyo, ni muhimu kwa wanawake wote kufanya uchunguzi wa mara kwa mara wa matiti na kuzingatia afya yao ya jumla.
Uchunguzi wa mapema na matibabu ya saratani ya matiti yanaweza kuokoa maisha.
Leave a Reply