Ujue Ugonjwa Wa Vidonda Vya Tumbo: Sababu, Dalili, Tiba, Madhara Na Jinsi Ya Kujikinga.

Vidonda Vya Tumbo:

Vidonda vya tumbo ni vidonda vinavyotokea kwenye ukuta wa tumbo. Vidonda vya tumbo vinajulikana kwa kitaalamu kama peptic ulcers.

Vidonda hivi hutokea kutokana na mashambulizi ya bakteria wanaoitwa Helicobacter pylori (H. pylori) au kulika kwa ukuta wa tumbo kunakotokana na athari za tindikali zilizopo tumboni (Hydrochloric Acid).

Picha Za Vidonda Vya Tumbo:

Aina Za Vidonda Vya Tumbo:

Vidonda vya tumbo vimegawanyika katika makundi makuu mawili ambayo ni;

1) Vidonda Vya Tumbo Kubwa.

 Hivi ni vidonda vya tumbo vinavyotokea ndani kwenye tumbo kubwa (stomach).

Vidonda hivi vya tumbo hujulikana kwa kitaalamu kama Gastric ulcers.

2) Vidonda Vya Utumbo Mdogo.

Hivi ni vidonda vya tumbo ambavyo hutokea kwenye sehemu ya juu ya utumbo mdogo inayoitwa duodenum.

Vidonda hivi vya tumbo hujulikana kwa kitaalamu kama Duodenal ulcers.

Sababu Za Vidonda Vya Tumbo:

Yafuatayo ni mambo yanayomuweka mtu katika hatari ya kupata vidonda vya tumbo ambayo ni pamoja na;

1) Bakteria waitwao Helicobacter pylori (H. pylori).

2) Matumizi ya mara kwa mara ya dawa za kupunguza maumivu kama asprin, (NSAIDs), (Advil, Aleve, na zingine).

3) Msongo wa mawazo.

4) Kula vyakula vinavyozalisha asidi kwa wingi.

5) Kunywa pombe na vinywaji vikali kupitiliza.

6) Uvutaji wa sigara.

7) Kutokula mlo kwa mpangilio.

8) Kansa ya tumbo.

Dalili Za Vidonda Vya Tumbo:

Zifuatazo ni dalili za vidonda vya tumbo ambazo ni pamoja na;

1) Kupata maumivu ya tumbo yanayokuwa kama ya moto (kuunguza) baada na kabla ya kula.

2) Kupatwa na kiungulia karibu na chembe ya moyo.

3) Tumbo kujaa gesi na kuvimbiwa.

4) Kichefuchefu na kutapika tena yawezekana kutapika damu.

5) Kupata haja kubwa ya rangi kahawia au nyeusi yenye harufu mbaya sana, pia haja yaweza kuchanganyikana na damu.

6) Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito.

7) Kushindwa kupumua vizuri.

Tiba Ya Vidonda Vya Tumbo:

Tatizo la Vidonda vya tumbo linatibika kufuatana na muda wa tatizo, mara nyingi wagonjwa wamekuwa wakizalau dalili za vidonda vya tumbo na kudhani kuwa hakuna madhara makubwa.

Dawa Za Hospital Za Vidonda Vya Tumbo:

Dawa zinazotolewa hospitali kwa ajili ya kutibu vidonda vya tumbo ni pamoja na;

a) Amoxicillin tabs.

b) Omeprazole tabs/pantoprazole tabs.

c) Metronidazole tabs (Flagyl).

Madhara Ya Vidonda Vya Tumbo:

Yafuatayo ni madhara yanayoweza kutokea endapo mgonjwa wa vidonda vya tumbo atashindwa kupata tiba mapema;

1) Kansa ya tumbo (Gastric cancer).

2) Kutoboka kwa kuta za tumbo (Gastro-intestinal perforation).

3) Kuvuja damu kwa kuta za tumbo (Gastro-intestinal bleeding).

4) Kutapika damu (hematemesis).

5) Upungufu wa damu (anaemia).

6) Kujisaidia kinyesi cheusi kama cha mbuzi (black orTarry stool).

7) Kuvurugika kwa mfumo wa mmeng’enyo wa chakula (obstructed digestion).

Jinsi Ya Kujikinga Na Vidonda  Vya Tumbo:

1) Jijengee tabia ya kunywa maji mengi kila siku.

2) Punguza mawazo, fanya mazoezi yatakupunguzia na mawazo.

3) Punguza (balansi) kiwango cha halemu (cholesterol).

4) Usivute sigara.

5) Punguza au acha kunywa pombe.

6) Kula vizuri vyakula bora hasa asilia na sio vyakula vyenye kemikali.

7) Tenga muda wa kutosha wa kupumzika–unashauriwa kulala masaa 7 hadi 9 kila siku.

Vyakula vya mtu mwenye vidonda vya tumbo:

Vyakula Vya Mtu Mwenye Vidonda Vya Tumbo:

Vifuatavyo ni vyakula anavyoshauriwa kutumia mgonjwa mwenye changamoto ya vidonda vya tumbo ambavyo ni pamoja na;

1) Asali.

Asali ina kemikali iitwayo ‘flavonoids‘ ambayo inaaminika kwamba ina umuhimu mkubwa sana kwenye tiba ya vidonda vya tumbo. Kemikali hii husaidia kupunguza uzalishaji wa tindikali tumboni, hydrochloric acid.

asali

2) Kitunguu saumu.

Kitunguu saumu ni dawa nzuri sana ya kuzuia uzalianaji wa bakteria wanaoshambulia kuta za tumbo, helicobacter pylori. Sio lazima kitunguu saumu kitafunwe kizima, bali mgonjwa mwenye vidonda vya tumbo anaweza kukitumia kwenye chakula na hata kutia kwenye chai.

kitunguu saumu

3) Broccoli.

Mboga nyingi za majani kama vile broccoli, spinachi, chainizi na nyinginezo zina utajiri mkubwa wa vitamini A. Vitamini A mwilini huongeza uzalishaji wa ute (mucus) ambao hulinda kuta za tumbo dhidi ya mashambulizi ya bakteria, helicobacter pylori na tindikali, hydrochloric acid.

broccoli

4) Yoghurt.

Wataalamu huitwa yoghurt ‘probiotics’ hawa ni bakteria wazuri wenye faida nyingi mwilini hasa kwenye mmeng’enyo wa chakula. Yoghurt zinapunguza uzalianaji wa bakteria wanaoshambulia kuta za tumbo, pia huongeza uzalishaji wa ute (mucus) ambao hulinda kuta za tumbo dhidi ya tindikali inayozalishwa kwa wingi tumboni.

yoghurt

5) Mafuta Ya Samaki.

Baadhi ya tafiti zinashauri wagonjwa wa vidonda vya tumbo wale mafuta yatokanayo na samaki (Omega-3 fatty acid) ambayo yameonekana kutoa ahueni kwa wagonjwa hao. Pia matumizi ya mafuta ya samaki kwa mtu ambaye si mgonjwa wa vidonda vya tumbo yanamsaidia kumwekea kinga dhidi ya vidonda vya tumbo na magonjwa mengine ya tumbo.

Vyakula Hatari Kwa Vidonda Vya Tumbo:

Vifuatavyo ni vyakula hatarishi kwa mgonjwa anayesumbuliwa na changamoto ya vidonda vya tumbo kwani hufanya hali ya mgonjwa kuwa mbaya zaidi;

1) Maziwa.

Mgonjwa mwenye vidonda vya tumbo anatambua kuwa akinywa maziwa maumivu yanapungua. Hii ni faida, lakini tafiti zinaonyesha kuwa maziwa yanaongeza uzalishwaji wa tindikali tumboni. Tindikali hizi zinavyozalishwa kwa wingi huchubua ukuta wa tumbo na kufanya hali ya mgonjwa kuwa mbaya zaidi.

maziwa

2) Pombe.

Unywaji wa pombe unaweza kuathiri na kuharibu kuta za tumbo na utumbo. Hali hii inaweza kusababisha hali ya mgonjwa kuwa mbaya zaidi.

pombe

3) Kahawa.

Kahawa inaweza kusababisha kuongezeka kwa uzalishwaji wa tindikali tumboni. tindikali hizi zikizalishwa kwa wingi tumboni zinaweza kuchubua ukuta wa tumbo na hufanya hali ya mgonjwa kuwa mbaya zaidi.

kahawa

4) Vyakula Vyenye Mafuta Na Fati Kwa Wingi.

Vyakula vyenye mafuta na fati kwa wingi kama vile nyama nyekundu, ice cream, nazi na mafuta ya nazi, chipsi, parachichi nk huchukua muda mrefu kumeng’enywa na kupelekea uzalishaji wa tindikali kwa wingi tumboni. Tindikali hiyo huchubua kuta za tumbo na kusababisha maumivu ya tumbo kwa mgonjwa.

Vyakula Vyenye Mafuta Na Fati Kwa Wingi


5) Vyakula Vyenye Viungo Vingi.

Vyakula vilivyopikwa na kuungwa viungo vingi vya aina mbalimbali kama vile pilipili kali za aina zote na viungo vingine vyenye ladha ya ukali ambavyo hutiwa ndani ya mboga ama chakula ili kuongeza ladha ni hatarishi kwa mgonjwa mwenye changamoto ya vidonda vya tumbo kwani vyakula hivi pia huchochea ongezeko la uzalishwaji wa tindikali tumboni ambayo huchubua kuta za tumbo na kufanya hali ya mgonjwa kuwa mbaya zaidi.


6) Vyakula Vyenye Chumvi Nyingi.

Utafiti uliowahi kufanywa nchini marekani umeonesha kuwepo kwa uhusiano kati ya ulaji wa vyakula vyenye chumvi nyingi na vidonda vya tumbo. Mgonjwa anashauriwa kuepuka ulaji wa vyakula vyenye chumvi nyingi hususani vyakula vya kusindika ambavyo huwekwa chumvi nyingi ili visiharibike haraka kwani vyakula hivyo huchochea ongezeko la uzalishaji wa tindikali tumboni ambayo huchubua kuta za tumbo na kufanya hali ya mgonjwa kuwa mbaya zaidi.

Vyakula Vyenye Chumvi Nyingi


7) Vyakula Vya Kuoka.

Vyakula vya kuoka kama vile mikate, keki ni miongoni mwa vyakula hatarishi kwa mgonjwa mwenye changamoto ya vidonda vya tumbo kwa sababu vyakula hivi huchukua muda mrefu kumeng’enywa na huchochea uzalishaji wa tindikali kwa wingi tumboni jambo ambalo hupelekea mgonjwa kupata maumivu ya tumbo.

vyakula vya kuoka


8) Vyakula Vyenye Uchachu.

Matunda yenye uchachu kama vile limao, chungwa yametajwa kuwa hatarishi kwa mgonjwa mwenye changamoto ya vidonda vya tumbo kwani matunda haya huchochea ongezeko la uzalishaji wa tindikali tumboni ambayo huchubua kuta za tumbo na kufanya hali ya mgonjwa kuwa mbaya zaidi.

vyakula vyenye uchachu

HITIMISHO:

Tumekuandalia programu inayohusisha matumizi ya virutubisho vilivyo tengenezwa kutokana na mimea na matunda kwa ajili ya kuondoa chanzo na kutibu kabisa vidonda vya tumbo. Ikiwa utahitaji virutubisho hivyo kwa ajili ya kutokomeza changamoto yako ya vidonda vya tumbo bonyeza hapa: “Hili Ndilo Suluhisho Bora Ukiwa Unataka Kutibu Vidonda Vya Tumbo.”. Pia jipatie kitabu (soft copy) kinacholelezea ugonjwa wa vidonda vya tumbo na jinsi ya kujikinga kwa gharama nafuu kabisa ya Tshs 7000/= tu.

vipimo vya mfumo wa uzazi