Madhara Ya Kushiriki Tendo La ndoa Wakati Wa hedhi Kwa Wanaume Na Wanawake.

Kushiriki tendo la ndoa wakati wa hedhi kunaweza kuwa na athari mbaya kwa afya ya wanaume na wanawake.

Tendo La ndoa Wakati Wa hedhi

Leo katika mada yetu ya blogu hii tuta zungumzia madhara ya kushiriki tendo la ndoa wakati wa hedhi kwa wanaume na wanawake. Ungana nami katika kuchambua madhara haya.

A) Madhara Kwa Wanawake:

Yafuatayo ni baadhi ya madhara yanayoweza kutokea kwa wanawake kutokana na kushiriki tendo la ndoa wakati wa hedhi ambayo ni pamoja na:

1) Maumivu Na Kutokwa Na Damu Nyingi Zaidi.

Wakati wa hedhi, baadhi ya wanawake wanaweza kuwa na maumivu zaidi ya tumbo (dysmenorrhea) na kutokwa na damu nyingi zaidi.

Kushiriki tendo la ndoa wakati huu kunaweza kuongeza maumivu na kusababisha kutokwa na damu nyingi zaidi.

2) Hatari Ya Kupata Maambukizi.

Kwa wanawake, kushiriki tendo la ndoa wakati wa hedhi kunaweza kuongeza hatari ya kupata maambukizi ya uke au njia ya mkojo kutokana na mlango wa uzazi (cervix) kuwa wazi zaidi kwa bakteria ikiwa wapenzi wao wana maambukizi. Mfano wa maambukizi hayo ni pamoja na Pelvic inflammatory Disease (PID), maambukizi ya zinaa (STIs) n.k

3) Saratani Ya Shingo Ya Kizazi.

Kushiriki tendo la ndoa wakati wa hedhi kunaweza kuongeza hatari ya kuambukizwa virusi vya HPV (Human Papilloma Virus), ambavyo vinasababisha saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake.

4) Kuziba Kwa Mirija Ya Uzazi.

Kwa wanawake, kushiriki tendo la ndoa wakati wa hedhi kunaweza kuongeza hatari ya kuziba kwa mirija ya uzazi (fallopian tubes), hali ambayo inaweza kusababisha ugumba au matatizo ya uzazi.

5) Hatari Ya Kupata Ujauzito.

Ingawa ni nadra, kuna hatari ya kupata mimba wakati wa hedhi. Manii (sperms) inaweza kuishi kwa siku kadhaa (mpaka siku 5) ndani ya mwili wa mwanamke, na inawezekana kutokea ovulation (kutoa yai) mapema.

B) Madhara Kwa Wanaume:

Yafuatayo ni baadhi ya madhara yanayoweza kutokea kwa wanaume kutokana na kushiriki tendo la ndoa wakati wa hedhi ambayo ni pamoja na:

1) Hatari Ya Kupata Maambukizi.

Wanaume wanaweza kuwa katika hatari ya kupata maambukizi ya zinaa wakati wa tendo la ndoa kipindi cha hedhi, ikiwa wapenzi wao wana hayo maambukizi.

2) Matatizo Ya Tezi Dume.

Kwa wanaume kushiriki tendo la ndoa wakati wa hedhi kunaongeza hatari ya damu ya hedhi kuingia kwenye tezi dume, hali ambayo inaweza kusababisha ugumba au matatizo ya tezi dume mfano prostatitis.

3) Athari Ya Kisaikolojia.

Baadhi ya wanaume wanaweza kuhisi wasiwasi au kutojisikia vizuri kushiriki tendo la ndoa wakati wa hedhi kutokana na kuvuja damu, harufu, au maumivu ambayo wapenzi wao wanaweza kuhisi.

4) Tatizo La Uume Kusimama Lege Lege.

Wakati wa tendo la ndoa kipindi cha hedhi, uchafu unaotoka ukeni ukiingia kwenye mishipa ya damu ya uume  unaweza kupelekea tatizo la uume kusimama lege lege, hali ambayo hujulikana kwa kitaalamu kama erectile dysfunction.

Soma pia hizi makala:

HITIMISHO:

Mwanaume mpende mpenzi wako kwa moyo wa dhati, jifunze kuwa mvumilivu siku 3-4 za mwanamke wako kuwa kwenye kipindi cha hedhi hata sio nyingi, heshimu hedhi ya mpenzi wako, mjali, msikilize anahitaji nini na sio kumlazimisha kufanya nae mapenzi katika kipindi cha hedhi.

Ni mimi mwenye kujali afya yako Dr. Isaya Febu.