Kuota Vinyama Ukeni:
Vinyama ukeni ni vinyama vidogo vinavyoota katika maeneo ya uke, mara nyingi vinyama hivi huota kwenye sehemu za nje za uke (vulva) au ndani ya uke (cervix). vinyama hivi huenezwa kwa njia ya kujamiiana.
Vinyama ukeni pia hujulikana kama masundosundo/visunzua ukeni au kitaalamu kama genital warts.
Ugonjwa huu husambazwa kwa mgusano wa ngozi kwa ngozi hasa wakati wa ngono, japo migusano mingine ya maeneo athirika isiyohusisha ngono inaweza pia kuwa chanzo cha kusambaa kwake.
Mara baada ya kuambukizwa, ugonjwa huu huweza kuchukua mpaka muda wa wiki sita hadi miezi 6 kwa vinyama ukeni kuwa dhahiri, ingawa baadhi ya wagonjwa wanaweza kukaa hata miaka kadhaa bila kuwa na dalili yoyote ile.
Kisababishi Cha Vinyama Ukeni:
Vinyama ukeni husababishwa na virusi wajulikanao kwa kitaalamu kama Human papilloma virus (HPV).
Ripoti ya shika la afya duniani (WHO) zinasema kwamba kuna aina zaidi ya 100 ya virusi wa papilloma waliokwisha kugunduliwa mpaka sasa ambapo kati ya hao ni aina mbili tu, HPV-6 na HPV-11 ambao ndio husababisha vinyama ukeni.
Leo katika mada yetu ya blogu hii tutazungumzia sababu mbalimbali zinazochangia kuota vinyama ukeni. Ungana nami katika kuchambua sababu hizi.
1) Kuwa Na Wapenzi Wengi.
Ikiwa una wapenzi wengi (multiple sexual partners) na hautumii kinga (condom) wakati wa kushiriki ngono basi unajiweka katika hatari ya kupata vinyama ukeni.
2) Kufanya Ngono Isiyo Salama Na Mwathirika Wa Masundosundo.
Ikiwa unashiriki ngono isiyo salama na mwanaume aliyeathirika na virusi wa Hpv basi unajiweka katika hatari kubwa ya kupata vinyama ukeni.
3) Ngono Katika Umri Mdogo.
Wanawake wanaoanza ngono mapema wapo kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata vinyama ukeni kutokana na kinga za mwili kuwa chini sana.
4) Matumizi Makubwa Ya Sigara Na Pombe.
Tafiti zinaonesha kwamba wanawake wenye matumzi makubwa ya pombe na sigara wanajiweka katika hatari ya kupata vinyama ukeni.
Uvutaji wa sigara huathiri mfumo wa kinga ya mwili, na kufanya mwili uwe na uwezo mdogo wa kupambana na maambukizi ya virusi kama vile HPV. Wanawake wanaovuta sigara wapo kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata maambukizi sugu ya HPV na hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kukuza vinyama ukeni.
Matumizi ya pombe kwa kiasi kikubwa yanaweza kudhoofisha kinga ya mwili, kuathiri maamuzi ya mtu, na kuongezeka kwa tabia hatarishi kama vile kufanya ngono bila kinga, ambayo huongeza hatari ya maambukizi ya HPV na vinyama ukeni.
Kwa hiyo, ingawa uvutaji wa sigara na unywaji pombe si sababu za moja kwa moja za kupata vinyama ukeni, tabia hizi zinaweza kudhoofisha kinga ya mwili na kuongeza hatari ya kuambukizwa HPV.
5) Upungufu Wa Kinga Mwilini (immunosuppression).
Kuwa na upungufu katika mfumo wa kinga mwilini kutokana na magonjwa mbalimbali kama vile kisukari, HIV, cancer au kwa sababu ya matumizi ya dawa fulani humuweka mwanamke katika hatari kubwa ya kupata vinyama ukeni. Pia hali ya kuwa na lishe duni (malnutrition) husababisha kushuka kwa kinga ya mwili hivyo kupelekea mwanamke kuwa katika hatari ya kupata vinyama ukeni.
6) Ujauzito.
Wakati wa ujauzito, mabadiliko ya homoni, mabadiliko katika mfumo wa kinga ya mwili yanaweza kuongeza uwezekano wa kupata vinyama ukeni.
7) Kuchangia Vitu Binafsi Na Mwathirika Wa Masundosundo.
Kuchangia (kushea) vitu binafsi kama vile taulo, nguo za ndani, na vifaa vya usafi wa mwili vinavyotumiwa na mtu mwenye masundosundo vinaweza kuhamasisha kuenea kwa HPV na kusababisha kupata vinyama ukeni.
HITIMISHO:
Ikiwa utahitaji virutubisho kwa ajili ya kutokomeza changamoto ya kuota vinyama sehemu za uke, genital warts bonyeza hapa: “Jinsi Ya Kutibu Ugonjwa Wa Kuota Vinyama Sehemu Za Siri Bila Kufanya Upasuaji.”
Leave a Reply