Punyeto Ni Nini?
Punyeto kwa mwanaume ni kitendo mwanaume cha kujipa raha ya kimapenzi kwa kusugua au kusisimua uume wake hadi kufikia mshindo (orgasm). Hii inaweza kufanyika kwa kutumia mkono, vifaa maalum mfano vibrators, au hata kwa msaada wa mawazo na vichocheo vya hisia kama picha au video (pornography).



Punyeto kwa mwanamke ni kitendo cha mwanamke kujipa raha ya kimapenzi kwa kutumia mikono yake au vitu vingine mfano vibrators kwa kusisimua sehemu zake za siri, hasa kisimi (clitoris) na uke, hadi kufikia mshindo (orgasm). Ingawa punyeto ni tabia inayozungumziwa na kujulikana kwa wanaume, wanawake pia hushiriki katika tabia hii.



Baadhi ya wanaume na wanawake hufanya kitendo hicho (kujichua) kwa sababu tofauti zikiwemo: Kupata starehe ya kimapenzi (kuburudika na kujipa raha), kupunguza hamu ya ngono wakati hakuna mwenza, kuepuka magonjwa ya zinaa (STIs) na mimba isiyotarajiwa.
Leo katika mada yetu ya blogu hii tutazungumzia madhara ya punyeto kwa wanaume na wanawake. Ungana nami katika kuchambua madhara haya.
Madhara Ya Punyeto Kwa Mwanaume:
Baadhi ya madhara yatokanayo na kupiga punyeto kwa wanaume ni pamoja na:
1) Uraibu (Addiction).
Wanaume wanaopiga punyeto mara kwa mara sana wanaweza kuwa na uraibu (addiction), hali inayowafanya washindwe kuacha hata wakitaka. Uraibu huu unaweza kuathiri kazi, mahusiano, na maisha ya kila siku.

2) Msongo Wa Mawazo Na Hatia.
Baadhi ya wanaume hujihisi na hatia au aibu baada ya kupiga punyeto, hasa ikiwa imani zao za kidini au kijamii haziungi mkono tabia hiyo jambo ambalo linaweza pia kusababisha msongo wa mawazo (stress), unyogovu (depression), au kujitenga na watu (social withdrawal).

3) Kupungua Kwa Hamu Ya Ngono.
Kupiga punyeto mara nyingi sana kunaweza kufanya mwanaume apoteze hamu ya kushiriki tendo la ndoa na mwenza wake, kwa sababu mwili unazoea msisimko wa kujipa raha peke yake.

4) Kupungua Kwa Ubora Wa Manii (Kwa Muda Mfupi).
Ikiwa unapiga punyeto mara nyingi sana, mwili wako hautakuwa na muda wa kutengeneza mbegu zenye nguvu, na hivyo ubora wa manii unaweza kupungua kwa muda. Lakini baada ya kupumzika kwa siku chache, uzalishaji wa manii hurudi kuwa wa kawaida.

5) Tatizo La Kuwahi Kufika Kileleni.
Kuwahi kufika kileleni kwa mwanaume ni hali ambayo hutokea pale mwanaume anapopata mshindo (anapofika kileleni) mapema zaidi kuliko yeye au mwenza wake wanavyotarajia, mara nyingi ndani ya dakika chache baada ya kuanza tendo la ndoa.

Mara nyingi mwanaume anayejichua (kupiga punyeto) huwa anafanya haraka kwa kujificha ili asikutwe na mtu hivyo mwili wake unaweza kuzoea kufika kileleni haraka hata wakati wa tendo la ndoa.
Tatizo hili linalojulikana kwa kitaalamu kama premature ejaculation linaweza kuathiri maisha ya ndoa na mahusiano kwa ujumla kwani limekua likiwapata wanaume wengi wanaojihusisha na kupiga punyeto mara kwa mara na kupelekea kujisikia aibu mbele za wenzi wao pale wanaposhindwa kuendelea kabisa kufanya tendo la ndoa baada ya hali hii kutokea.

6) Kupoteza Muda Mwingi.
Ikiwa unatumia muda mwingi kwenye punyeto badala ya shughuli muhimu kama kazi, masomo, au mahusiano, inaweza kuathiri maendeleo yako binafsi.

Madhara Ya Punyeto Kwa Mwanamke:
Baadhi ya madhara yatokanayo na kupiga punyeto kwa wanawake ni pamoja na:
1) Maambukizi Ukeni.
Matumizi ya mikono au vifaa visivyo safi wakati wa kupiga punyeto vinaweza kuingiza bakteria kwenye uke, na kusababisha maambukizi ukeni kama vile maambukizi ya njia ya mkojo (UTI) au maambukizi ya fangasi ukeni (vaginal yeast infection).
2) Uke Mlegevu.
Kujichua mara nyingi kwa mwanamke kunaweza kusababisha uke kuwa mlegevu, hali ambayo inaweza kuathiri hisia wakati wa tendo la ndoa.
3) Maumivu Ya Via Vya Uzazi.
Ikiwa punyeto inafanywa na mwanamke mara kwa mara na kwa nguvu kupita kiasi, inaweza kusababisha maumivu kutokana na msuguano mwingi katika via vya uzazi mfano clitoris kwa muda mrefu.
4) Kupungua Kwa Hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa Na Mwenza.
Wanawake wanaweza kukosa hisia au hamu ya kushiriki tendo la ndoa na wenzi wao kutokana na kuzoea raha ya punyeto, ambayo inaweza kuathiri uwezo wao wa kufika kileleni wakati wa ngono.
5) Kupoteza Furaha Ya Tendo La Ndoa.
Baadhi ya wanawake wanaweza kupata hali ya kutoridhishwa na mwenza wao baada ya kuzoea aina fulani ya raha wanayoipata kupitia punyeto.
6) Kujisikia Hatia Au Aibu.
Katika baadhi ya jamii au dini, punyeto huonekana kama jambo lisilokubalika, na hivyo inaweza kusababisha hisia za hatia au aibu kwa mwanamke. Hii inaweza kusababisha hali ya kiakili ya kujihukumu au kujiona kuwa na makosa, ambayo inaweza kuathiri ustawi wa kisaikolojia.
7) Uraibu (Addiction).
Tabia ya kujichua (punyeto) pia inaweza kupelekea mwanamke kupata uraibu (addiction), hali ambapo mwanamke anakuwa na hitaji la mara kwa mara la kujichua, kiasi kwamba tabia hii inaingilia au kuathiri maisha ya kila siku, kazi, au mahusiano.
HITIMISHO:
Ikiwa mwanaume au mwanamke umekuwa mraibu wa punyeto na unahitaji kupata muongozo utakaokusaidia kuacha kabisa kitendo hicho+kujitibia madhara yatokanayo na kufanya kitendo hicho kwa muda mrefu wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487.
Leave a Reply