Punyeto Ni Nini?
Punyeto kwa mwanaume ni kitendo cha mwanaume kujipa raha ya kimapenzi kwa kusugua au kusisimua uume wake hadi kufikia mshindo (orgasm). Hii inaweza kufanyika kwa kutumia mkono, vifaa maalum mfano vibrators, au hata kwa msaada wa mawazo na vichocheo vya hisia kama picha au video (pornography).



Sababu Kuu Za Wanaume Kupiga Punyeto:
Baadhi ya sababu zinazopelekea wanaume kupiga punyeto ni pamoja na:
1) Kupunguza Msongo Wa Mawazo (Stress Relief).
Kupiga punyeto hutoa homoni za furaha kama vile dopamine na endorphins, ambazo husaidia kupunguza msongo wa mawazo na kumfanya mtu ajisikie vizuri.
Wanaume wengine hutumia punyeto kama njia ya kupunguza msongo wa mawazo ya maisha ya kila siku, kazi, au masomo.


2) Kuburudika Na Kujipa Raha.
Punyeto ni njia rahisi ya kupata raha ya kimapenzi bila mshirika (mwanamke) na inaweza kufanyika wakati wowote na mahali popote panapotoa faragha, bila mahitaji ya uhusiano wa kimapenzi. Hivyo baadhi ya wanaume hupiga punyeto kwa lengo na kujiburudisha na kujipa raha wenyewe.

3) Ukosefu Wa Mwenza Wa Kufanya Naye Ngono.
Wanaume ambao hawana wapenzi au hawako kwenye uhusiano wa kimapenzi mara nyingi hutumia punyeto kama njia mbadala ya kujiridhisha kingono.


4) Kupunguza Hamu Kubwa Ya Ngono.
Baadhi ya mwanaume ambao wako kwenye mazingira ambayo haiwezekani kushiriki ngono, hupiga punyeto kwa lengo la kujiridhisha kingono ili kudhibiti hamu zao.
Lakini pia, kwa wanaume wanaojizuia kufanya ngono kabla ya ndoa au wale walio kwenye mahusiano ya umbali mrefu (long distance relationship) hupiga punyeto kama njia mbadala ya kujiridhisha kingono.

4) Kupunguza Hatari Ya Magonjwa Ya Zinaa (STIs).
Kwa wale wanaume wasio na wapenzi au wanaoepuka mahusiano ya kimapenzi yasiyo salama, hupiga punyeto kama njia mbadala na salama ya kupata raha bila kuhatarisha maambukizi ya magonjwa ya zinaa.

5) Kuchunguza Mwili Na Hisia Za Kimapenzi.
Baadhi ya wanaume hupiga punyeto kwa lengo la kujifunza kuhusu miili yao na maeneo yanayowapa msisimko zaidi.

6) Kuboresha Usingizi.
Baada ya kufikia mshindo, mwili hutoa homoni za utulivu kama vile prolactin, ambazo husaidia mtu kujisikia usingizi haraka na kupumzika vizuri. Hivyo baadhi ya wanaume hupiga punyeto kama njia mbadala ya kupata usingizi haraka.


Madhara Ya Kupiga Punyeto Kwa Mwanaume:
Baadhi ya madhara yatokanayo na kupiga punyeto kwa wanaume ni pamoja na:
1) Uraibu (Addiction).
Wanaume wanaopiga punyeto mara kwa mara sana wanaweza kuwa na uraibu (addiction), hali inayowafanya washindwe kuacha hata wakitaka. Uraibu huu unaweza kuathiri kazi, mahusiano, na maisha ya kila siku.

2) Msongo Wa Mawazo Na Hatia.
Baadhi ya wanaume hujihisi na hatia au aibu baada ya kupiga punyeto, hasa ikiwa imani zao za kidini au kijamii haziungi mkono tabia hiyo jambo ambalo linaweza pia kusababisha msongo wa mawazo (stress), unyogovu (depression), au kujitenga na watu (social withdrawal).

3) Kupungua Kwa Hamu Ya Ngono.
Kupiga punyeto mara nyingi sana kunaweza kufanya mwanaume apoteze hamu ya kushiriki tendo la ndoa na mwenza wake, kwa sababu mwili unazoea msisimko wa kujipa raha peke yake.

4) Kupungua Kwa Ubora Wa Manii (Kwa Muda Mfupi).
Ikiwa unapiga punyeto mara nyingi sana, mwili wako hautakuwa na muda wa kutengeneza mbegu zenye nguvu, na hivyo ubora wa manii unaweza kupungua kwa muda. Lakini baada ya kupumzika kwa siku chache, uzalishaji wa manii hurudi kuwa wa kawaida.

5) Tatizo La Kuwahi Kufika Kileleni.
Kuwahi kufika kileleni kwa mwanaume ni hali ambayo hutokea pale mwanaume anapopata mshindo (anapofika kileleni) mapema zaidi kuliko yeye au mwenza wake wanavyotarajia, mara nyingi ndani ya dakika chache baada ya kuanza tendo la ndoa.

Mara nyingi mwanaume anayejichua (kupiga punyeto) huwa anafanya haraka kwa kujificha ili asikutwe na mtu hivyo mwili wake unaweza kuzoea kufika kileleni haraka hata wakati wa tendo la ndoa.
Tatizo hili linalojulikana kwa kitaalamu kama premature ejaculation linaweza kuathiri maisha ya ndoa na mahusiano kwa ujumla kwani limekua likiwapata wanaume wengi wanaojihusisha na kupiga punyeto mara kwa mara na kupelekea kujisikia aibu mbele za wenzi wao pale wanaposhindwa kuendelea kabisa kufanya tendo la ndoa baada ya hali hii kutokea.

6) Kupoteza Muda Mwingi.
Ikiwa unatumia muda mwingi kwenye punyeto badala ya shughuli muhimu kama kazi, masomo, au mahusiano, inaweza kuathiri maendeleo yako binafsi.

HITIMISHO:
Ikiwa unahisi unakumbana na madhara hayo hapo juu, unaweza kujaribu kupunguza au kuacha taratibu ili kuboresha afya yako na maisha yako kwa ujumla. Ikiwa kama mraibu wa punyeto unahitaji kupata muongozo wa kuacha kabisa kufanya kitendo hicho na kujitibia madhara yaliyotokana na kufanya kitendo hicho kwa muda mrefu wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487.

Leave a Reply