Kisukari Husababishwa Na Nini?

Kisukari (Diabetes Mellitus) ni ugonjwa wa muda mrefu unaotokea pale ambapo mwili unashindwa kudhibiti viwango vya sukari kwenye damu kwa ufanisi. Kisukari kinaweza kutokea kwa sababu ya sababu mbalimbali, kulingana na aina ya kisukari. Hizi ndizo sababu kuu:

1) Kisukari Aina Ya 1 (Type 1 Diabetes).

Sababu Kuu: Kisababishi halisi (the exact cause) cha aina hii ya kisukari hakijulikani. Mara nyingi aina hii ya kisukarI inayotokana na mambo kadhaa ikiwemo:

A) Matatizo Ya Kinga Ya Mwili.

Mfumo wa kinga ya mwili hushambulia kimakosa seli za kongosho zinazozalisha insulini ziitwazo beta cells, hali inayosababisha ukosefu wa insulini kabisa.

B) Urithi Wa Vinasaba (Genetics).

Historia ya familia yenye Kisukari Aina ya 1 inaweza kuongeza hatari ya kupata aina hii ya kisukari.

3) Sababu Za Kimazingira.

Maambukizi ya virusi fulani kama vile enteroviruses yanaweza kusababisha mfumo wa kinga kufeli na kushambulia seli za kongosho.

 Kisukari Aina Ya 1 (Type 1 Diabetes).

2) Kisukari Aina Ya 2 (Type 2 Diabetes).

Sababu kuu: Mwili hauzalishi insulini ya kutosha, au mwili unashindwa kuitumia vizuri (insulin resistance).

Hutokana na mchanganyiko wa:

A) Mtindo Wa Maisha Usiofaa (Poor Lifestyle).

Lishe yenye sukari nyingi, ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi, kutofanya mazoezi, na unene kupita kiasi (obesity).

B) Vinasaba (Genetics).

Historia ya kisukari katika familia.

C) Umri.

Huonekana zaidi kwa watu wazima, ingawa sasa inatokea pia kwa watoto kutokana na mtindo wa maisha.

Kisukari Aina Ya 2 (Type 2 Diabetes)

3) Kisukari Cha Mimba (Gestational Diabetes).

Sababu kuu: Mabadiliko ya homoni wakati wa ujauzito yanaweza kuingilia uwezo wa mwili kutumia insulini.

Hutokea kwa baadhi ya wanawake wajawazito kutokana na aidha uzito kupita kiasi kabla ya ujauzito, umri mkubwa wa uzazi, zaidi ya miaka 35 (advanced maternal age), historia ya kisukari katika familia na na huweza kutoweka baada ya kujifungua, ingawa huongeza hatari ya kupata kisukari cha aina ya 2 baadaye.

Kisukari Cha Mimba (Gestational Diabetes).

Soma pia hii makala: Yajue Mambo 6 Muhimu Kuhusu Kisukari Cha Ujauzito.

HITIMISHO:

Ikiwa una dalili za kisukari, kama vile kiu cha mara kwa mara (polydipsia), kukojoa mara kwa mara (polyuria), njaa kupita kiasi (polyphagia), uchovu, au kupungua uzito ghafla, ni muhimu kumwona daktari kwa uchunguzi na ushauri.

kisukari