Yajue Mambo 9 Muhimu Kuhusu Kansa Ya Mapafu.

Kansa ya mapafu ni ugonjwa ambao unatokea pale seli za mapafu zinapoanza kugawanyika na kukua bila mpangilio (udhibiti). Ugonjwa huu unajulikana kwa kitalaamu kama Lung cancer (Lung carcinoma).

Kansa ya mapafu ni kansa ambayo huchukua namba mbili kwa kuwapata watu wengi zaidi duniani kote huku namba moja ikiwa kansa ya matiti yaani Breast cancer kwa takwimu za mwaka 2020. Zaidi ya watu milioni 2.2 wamegundulika wana kansa hii ndani ya mwaka 2020. Huku idadi ya wanaume  ikiwa ni kubwa zaidi kuliko wanawake. Kwa upande wa kusababisha vifo, kansa ya mapafu imechukua namba moja kwa takwimu za Mwaka 2020, huku ikisababisha vifo Milioni 1.80.

Kulingana na patholojia, kansa ya mapafu hugawanywa katika makundi mawili, ”small cell lung carcinoma (SCLC) ” na ”non-small cell lung carcinoma (NSCLC) ”.

Soma pia hizi makala:

Kansa Ya Mapafu Husababishwa Na Nini?

Uvutaji wa sigara ndiyo sababu kuu inayoongoza kwa kusababisha saratani ya mapafu. Kadri unavyovyuta sigara nyingi zaidi kwa siku na kadri unavyoanza kuvuta sigara katika umri mdogo zaidi, ndivyo hatari ya kupata saratani ya mapafu inavyoongezeka.

uvutaji wa sigara

Hata hivyo, saratani ya mapafu imetokea kwa watu ambao hawajawahi kuvuta sigara. Kupumua moshi wa sigara toka kwa watu wengine wanaovuta huongeza hatari ya kupata kansa ya mapafu. Kulingana na Shirikisho la Kansa la Marekani, wastani wa watu wazima 3,000 wasiovuta sigara wanakufa kila mwaka kutokana na saratani ya mapafu kwa sababu ya kupumua moshi wa sigara kutoka kwa wengine wanaovuta.

Kumbuka: Saratani ya mapafu husababisha vifo vingi kwa wanaume na wanawake. Kila mwaka, watu wengi zaidi hufa kwa kansa ya mapafu kuliko saratani ya matiti, koloni, na saratani ya tezi dume kwa pamoja. Saratani ya mapafu huwapata watu wazima. Ni nadra kuwapta watu chini ya umri wa miaka 45. 

Tabia Hatarishi Zinazochangia Kupata Kansa Ya Mapafu:

Tafiti zimegundua sababu zifuatazo huongeza hatari ya kupata kansa ya mapafu;

1) Uvutaji Wa Tumbaku.

Moshi wa tumbaku husababisha kansa ya mapafu. hii ndio sababu kubwa zaidi inayopelekea kutokea kwa kansa ya mapafu. Kemikali hatari zilizopo kwenye moshi wa tumbaku ziitwazo nikotini huharibu seli za mapafu.

Hii ndiyo sababu uvutaji wa sigara kiko, au cigar husababisha kansa ya mapafu, na ndio sababu moshi kutoka kwa watu wengine unaweza kusababisha kansa kwa watu wasiovuta. Kadri mtu anapovuta moshi huu wa sigara ndivyo hatari yake ya kupata kansa ya mapafu inavyoongezeka.    

2) Radoni.

Radoni ni gesi yenye miali nunurishi (radioactive) ambayo huwezi kuiona, haina harufu, au ladha. Inaundwa kwenye udongo na miamba. Watu wanaofanya kazi katika migodi wanaweza kuvuta gesi hii hatari ya radon bila kujua. Katika maeneo mengine ya nchi, radon inapatikana kwenye nyumba. Radon huharibu seli za mapafu, na watu wanaovuta radon huwa katika hatari kubwa ya kansa ya mapafu.

3) Asbestos.

Watu wanaofanya kazi katika viwanda vya ujenzi na kemikali wako kwenye hatari kubwa ya kupata kansa ya mapafu. Kukutana na asbestos, aseniki, kromium, nickel, masizi, lami, na vitu vingine vinaweza kusababisha kansa ya mapafu. Hatari ni kubwa zaidi kwa wale waliokutana na kemikali hizi kwa muda mrefu zaidi.  Hatari ya kupata kansa ya mapafu ni maradufu kwa watu wanaovuta sigara.

4) Uchafuzi Wa Hewa Uliokithiri.

Uchafuzi wa hewa unaweza kuongeza hatari ya kupata kansa ya mapafu. Watu wanaovuta sigara na wanaoishi katika maeneo yenye uchafuzi mkubwa wa hewa wako kwenye hatari maradufu ya kupata saratani ya mapafu.

5) Historia Ya Kansa Ya Mapafu Kwenye Familia.

Watu wenye baba, mama, kaka, au dada aliye na kansa ya mapafu wanaweza kuwa katika hatari zaidi ya kupata ugonjwa huu, hata kama hawavuti sigara.

6) Historia Ya Kuugua Kansa Ya Mapafu.

Watu ambao wameshawahi kuugua kansa ya mapafu wako katika hatari zaidi ya kupata tena kansa nyingine.

7) Umri Zaidi Ya Miaka 65.

Watu wengi huwa na umri zaidi ya miaka 65 wakati wanapogunduliwa kuwa na kansa ya mapafu.

Hatua Za Ukuaji Wa Kansa Ya Mapafu:

Mara nyingi saratani zipo katika madaraja (stages) ili kuonesha kwa kiasi gani saratani imesambaa kwenye mwili. Uwezekano wa kupona saratani yako unategemea ni mapema kiasi gani umechunguzwa na kuanza tiba. Hii ni kwasababu saratani ya mapafu huanza kuleta dalili ikiwa tayari imesambaa. Saratani ya mapafu ina hatua kuu nne ambazo ni;

1) Stage 1.

Saratani imepatikana kwenye mapafu lakini bado hajisambaa nje ya mapafu.

2) Stage 2.

 Saratani ipo kwenye mapafu na imeanza kusambaa kwenye tezi za karibu za kutoa taka/ lymph nodes.

3) Stage 3.

Saratani ipo kwenye mapafu, kwenye tezi za kutoa taka na kwenye mapafu na pia katikati ya mapafu.

4) Stage 3A.

Saratani ipo kwenye mapafu na kwenye tezi lakini kwenye pafu moja pekee ambako ilianzia.

5) Stage 3B.

Saratani imesambaa kwenye tezi za kutoa taka za kwenye pafu la pili naeneo la juu karibu na mfupa wa kola.

6) Stage 4.

Saratani imesambaa kwenye mapafu, na kwenye viungo vya karibu na mapafu.

Dalili Za Kansa Ya Mapafu:

Mara nyingi katika hatua ya mwanzo kansa ya mapafu haina dalili. Lakini kadri kansa inavyozidi kukua, dalili huanza kujitokeza kama zifuatazo;    

1) Kikohozi kinachozidi kuwa kibaya zaidi siku hadi siku.  

2) Kupata shida kupumua. 

3) Maumivu  ya kifua yasiyoisha.

4) Kukohoa damu.    

5) Kukwaruza kwa sauti.

6) Maambukizi ya mara kwa mara ya mapafu, kama vile nimonia.    

7) Kuhisi umechoka sana wakati wote.    

8) Kupungua kwa uzito bila sababu ya msingi.

Kumbuka: Katika hali ya kawaida dalili hizi hazitokani na kansa. Matatizo mengine ya kiafya yanaweza kusababisha baadhi ya dalili hizi. Mtu yeyote mwenye dalili hizi anapaswa kumuona daktari atambuliwe na kutibiwa mapema iwezekanavyo.

Utambuzi Wa Kansa Ya Mapafu:

Ikiwa una dalili zinazofanana na za kansa ya mapafu, daktari ni lazima achunguze na kugundua kama dalili hizo zinatokana na kansa kweli au sababu nyingine. Daktari anaweza kukuliza kuhusu historia binafsi na historia ya kimatibabu ya familia yako. Daktari anaweza kuagiza vipimo vya damu, na anaweza pia kufanya vipimo vifuatavyo;

1) Uchunguzi Wa Mwili.

Daktari atachunguza mwili, atasikiliza jinsi unavyopumua, na kuchunguza kama kuna maji kwenye mapafu. Daktari anaweza kuchunguza kama tezi zako za limfu zimevimba na kama ini limevimba.

2) X-Ray Ya Kifua (CXR).

 Picha za eksirei ya kifua zinaweza kuonesha uvimbe au maji kifuani.

CXR

3) CT scan.

Madaktari mara nyingi hutumia CT scan kupiga picha ya kifua. Mashine ya eksirei iliyounganishwa na kompyuta hupiga picha kadhaa, picha hizi zinaweza kuonesha uvimbe, maji , au tezi za limfu zilizovimba.

ct scan

Vipimo Vya Kansa Ya Mapafu:

Njia pekee ya uhakika ya kujua kama kuna kansa kwenye mapafu ni kwa daktari kuchunguza sampuli za seli au tishu. Mwanapatholojia huchunguza sampuli kwa darubini na hufanya vipimo vingine. Kuna njia nyingi za kukusanya sampuli. Daktari anaweza kuamuru ufanye moja au zaidi ya vipimo vifuatavyo ili kukusanya sampuli;

1) Sputum Cytology.

Kipimo hiki kinausisha makohozi kutoka kwenye mapafu. Maabara huchunguza sampuli za makohozi kuangalia seli za kansa.  

sputum cytology

2) Thoracentesis.

Daktari hutumia sindano ndefu kutoa maji kifuani. Maabara huchunguza maji hayo kama kuna seli za saratani.   

thoracentesis

3) Bronchoscopy.

Daktari huingiza tube nyembamba yenye kamera (bronchoscope) kwenye mapafu kupitia puani au mdomoni. Hii humpa furusa daktari kuchunguza njia ya hewa na mapafu. Daktari anaweza pia kuchukua sampuli ya seli kutoka katika sehemu ya mapafu anayoishuku kwa ajili ya kuipima.

4) Fine-Needle Aspiration Biopsy.

Daktari hutumia sindano nyembamba ili kuchukua tishu au maji kutoka kwenye mapafu au tezi za limfu.

5) Thoracoscopy.

Daktari wa upasuaji atatoboa matundu kadhaa kifuani ili kuruhusu tube yenye kamera kuingia ndani ya kifua kwa ajili ya uchunguzi. Kipimo hiki humpatia fursa daktari kuyakagua mapafu bila kufungua kifua chote na kama ataona eneo lisilo la kawaida anaweza kuchukua nyama ndogo (biopsy) kwa ajili ya uchunguzi.

6) Thoracotomy.

Huu ni upasuaji mkubwa,vdaktari wa upasuaji hufungua kifua ili kuyakagua vyema mapafu na ikiwezekana kuiondoa kabisa sehemu ya mapafu yenye kansa. Tezi za limfu na tishu nyingine zinaweza kuondolewa pia.

Matibabu Ya Kansa Ya Mapafu:

Wagonjwa wenye kansa ya mapafu wana chaguzi nyingi za matibabu. Uchaguzi wa matibabu hutegemea hatua ya saratani. Chaguzi za matibabu ni pamoja na,upasuaji, tiba ya mionzi, tibakemikali, au mchanganyiko wa njia hizi. Kabla ya kuanza kwa matibabu, uliza kuhusu madhara yatokanayo na matibabu kwa sababu mara nyingi matibabu ya saratani huharibu seli na tishu zenye afya pia. Athari za matibabu hazifanani kwa watu wote na zinaweza kubadilika kulingana na aina ya tiba.

1) Upasuaji.

Kama hatua ya kansa na afya ya mgonjwa kwa jumla inaruhusu, upasuaji ni tiba kuu ya saratani ya mapafu. Uvimbe wote na sehemu ya seli zenye afya zinazouzunguka huondolewa.

2) Tiba ya mionzi (Radiotherapy).

Hii ni tiba ya kansa inayoua seli za saratani au kuzizuia kukua kwa kutumia mionzi ya yenye nguvu sana.    

3) Tibakemikali (Chemotherapy).

Tiba hii hutumia madawa kuua seli za saratani au kuzizuia zisikue au kuongezeka.    

4) Matibabu Ya Kulenga (Targeted Therapies).

Aina hii ya tiba hutumia dawa zinazolenga  kupunguza ukuaji wa mishipa ya damu kwenye uvimbe na madawa yanayolenga kuzuia epidermal growth factor receptor ambayo huchochea ukuaji wa uvimbe wa kansa.

Jinsi Ya Kujikinga Na Kansa Ya Mapafu:

Takwimu za epidemiolojia zinaonesha kufanya mambo yafuatayo kunapunguza maradufu hatari ya kupata kansa ya mapafu;

1) Epuka uvutaji wa sigara au kupumua moshi wa watu wengine wanaovuta.    

2) Punguza au epuka kabisa kukutana gesi ya radon.    

3) Epuka kukutana na kemikali zinazosababisha kansa ya mapafu unapokua mahali pa kazi au mahali pengine.    

4) Kula chakula bora, matunda na mboga za majani kwa wingi.    

5) Kwa wavutaji wa sigara wa sasa au wa zamani, watumie dozi kubwa ya vitamini au madawa yenye vitamini nyingi.

HITIMISHO:

Kwa msaada wa tiba na ushauri wa magonjwa ya afya ya uzazi wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487.