Yajue Maambukizi Ya Homa Ya Ini Na Jinsi Ya Kujikinga.

Ini ni kiungo muhimu sana ndani ya miili yetu, hufanya kazi zaidi ya 500 ; moja ya kazi ni kuchuja na kuondoa sumu kutoka kwenye damu.

Kutokana na sababu mbalimbali kama vile matumizi ya pombe kupita kiasi, sumu kwenye damu au maambukizi; ini hupata shida na kuvimba na kushindwa kufanya kazi vizuri. Hii hali huitwa homa ya ini. Homa ya ini hujulikana kwa kitaalamu kama Hepatitis.

Katika maeneo yetu, bara la afrika maambukizi ya virusi wa homa ya ini ndio sababu kuu ya shida kwenye ini. Virusi vya homa ya ini vipo vya aina 5 (A,B,C,D,E) ambapo aina mbili za virusi (B na C ) ndio sababu kuu za ugonjwa wa homa ya ini na husambaa kupitia damu na majimaji ya mwili.

Homa ya ini ni sawa janga linaloua kimya kimya kulingana na takwimu za vifo vya dunia inakadiriwa kirusi cha homa ya ini aina ya B pekee huua watu 600,000 hivi kila mwaka.

Kwa wastani zaidi ya watu bilioni mbili, yaani, asilimia 33 hivi ya watu wote ulimwenguni, wameambukizwa virusi vya HBV (Hepatitis B Virus), na wengi wao hupona baada ya miezi michache. Watu milioni 350 hivi huendelea kuwa na virusi hivyo mwilini, wengi huishi bila dalili na kuendelea kuambukiza watu wengine.

homa ya ini

Homa Ya Ini Inaambukizwa Kwa Njia Gani?

Virusi vya homa ya ini B na C husambaa kupitia damu, shahawa au maji maji mengine ya mwili.

Virusi hivi vina uwezo wa kusambaa na kuambukiza mtu mara 100 zaidi ya virusi vya ukimwi.

hepatitis b virus

Zifuatazo ni njia za usambaaji wa virusi hivi vya homa ya ini ambazo ni pamoja na;

1) Kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Mama aliye na maambukizi ya hepatitis b humuambukiza mtoto wakati wa kujifungua, iwapo hamna juhudi za matibabu za kuzuia maambukizi kuna uwezekano hadi asilimia 90 kwa mama kumuambukiza mtoto.

2) Kufanya mapenzi na mtu mwenye maambukizi ya virusi vya homa ya ini.

3) Kuchangia vifaa vyenye ncha kali kama sindano hasa kwa watumiaji wa madawa ya kulevya au wachora tattoo, miswaki.

4) Kuongezewa damu ambayo ina maambukizi ya homa ya ini.

5) Kunyonyana Ndimi ‘Denda’ na mtu mwenye maambukizi ya virusi vya homa ya ini.

6) Kuchangia taulo na mtu mwenye ugonjwa huu.

7) Kubadilishana nguo na mtu mwenye huu ugonjwa au kukumbatiana wakati mkiwa mnavuja jasho.

Tafiti za kitaalamu zinaonesha kuwa virusi hivyo ni hatari kuliko hata vya ukimwi kwa sababu vinaweza kuishi nje ya mwili wa binadamu (yaani nje ya mfumo wa damu) kwa siku saba. Virusi vya ukimwi (VVU) havina uwezo wa kuishi nje ya mfumo wa damu hata kwa dakika moja.

Kutokana na usugu wa HBV, maana yake ni kwamba kama kirusi kipo kwenye ngozi, kitaendelea kuwa hai kwa siku saba na katika kipindi hicho mtu anaweza kuambukizwa kwa njia ya damu au jasho.

Kwa wastani kirusi cha HBV kikishaingia mwilini, hupevuka ndani ya siku 75, hata hivyo upo uwezekano wa kupevuka kati ya siku 30 hadi 180. ndani ya siku 30 mpaka 60, mtu mwenye HBV anaweza kugundulika ikiwa atapimwa.

Mtu mwenye homa ya ini ana wastani mdogo wa kuishi kuliko mwenye ukimwi. Kwa maana hiyo, mwenye maambukizi ya virusi vya homa ya ini hufariki dunia haraka kuliko mwenye VVU.

Sababu Zinazosababisha Homa Ya Ini:

Yafuatayo ni makundi ya watu ambao wapo katika hatari zaidi ya kupata maambukizi ya homa ya ini;

1) Watoto wachanga waliozaliwa na mama aliye na maambukizi ya virusi vya homa ya ini.

2) Watu wanaofanya biashara ya ngono.

3) Wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume wenzao.

4) Watu wanaojidunga dawa za kulevya.

5) Mtu mwenye mpenzi ambaye anaishi na maambukizi ya virusi vya homa ya ini.

6) Wafanyakazi wa sekta ya afya.

7) Watu wa familia wenye ndugu anayeishi na maambukizi ya kudumu ya virusi vya homa ya ini.

8) Wagonjwa wa figo wanaotumia huduma za kusafisha damu (dialysis).

Dalili Za Homa Ya Ini:

Kwa kawaida dalili za mwanzo za homa ya ini hutokea ndani ya miezi 6 baada kuambukizwa,na hutokea kwa baadhi ya watu hazitokei kwa kila mtu.

Mgonjwa mwenye maambukizi ya virusi vya homa ya ini hupata dalili zifuatazo;

1) Uchovu.

2) Kichefuchefu.

3) Mwili kuwa dhaifu.

4) Homa kali.

5) Kupoteza hamu ya kula.

6) Kupungua uzito.

7) Maumivu makali ya tumbo upande wa ini.

8) Macho na ngozi kuwa vya njano.

9) Mkojo mweusi/mkojo kuwa na rangi iliyokolea kama coca-cola.

jaundice

Kumbuka:

Kuna kundi dogo la wagonjwa wa homa ya ini hupata ugonjwa mkali wa ini na kusababisha ini kushindwa kabisa kufanya kazi pia huweza kusababisha kifo. Hii hatua huitwa “fulminant liver failure”.

Watu wenye maambukizi ya kudumu ya virusi vya homa ya ini mara nyingi huwa hawana dalili, kadri muda unavyoenda virusi husababisha ini kusinyaa (liver cirrhosis) na kushindwa kufanya kazi vyema. Pia maambukizi ya virusi vya homa ya ini huchangia pia kupata saratani ya ini ambayo hujulikana kwa kitaalamu kama hapatocellular carcinoma.

Soma pia hii makala: Mambo 9 Muhimu Usiyo yajua Kuhusu Saratani.

liver cirrhosis

Watu Wanaohitajika Kupimwa Homa Ya Ini:

Watu wanaohitajika kupimwa homa ya ini ni wale wanaoishi kwenye maeneo yenye maambukizi ya virusi vya homa ya ini kwa zaidi ya asilimia 2. Tanzania ni moja ya nchi zenye kiwango cha maambukizi ya virusi vya homa ya ini kwa wastani wa 5% hivyo watanzania wote ni muhimu kupima. Watu kutoka makundi yafuatayo ni sharti kupimwa kama wana maambukizi ya virusi wa homa ya ini;  

1) Watu wote wanaotumia dawa za kulevya na kujidunga.

2) Wafanyakazi katika sekta ya afya.

3) Watu wote wanaoishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi.

4) Watu wote ndani ya familia wanaoshi na ndugu aliyeambukizwa virusi vya homa ya ini.

5) Watu wote wanaotumia dawa za kufubaza kinga ya mwili (immunosuppressive therapy)

6) Watu wote wenye ugonjwa wa figo wanahitaji kuanza dialysis.

7) Akina mama wajawazito wote.

8) Wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume wenzao.

Tiba Ya Homa Ya Ini:

Hadi sasa magonjwa mengi yanayosababishwa na Virusi hayana tiba maalumu, matibabu ni kwa madhara tu mgonjwa anayoyapata, hivyo njia sahihi ya kuepukana na magonjwa haya mara nyingi huwa ni kuchukua tahadhari juu ya maambukizi na kupata chanjo.

Chanjo Ya Homa Ya Ini Ya Tanzania.

Chanjo dhidi ya homa ya ini hutolewa kwa watoto wote kama ilivyo kwenye mpango wa chanjo wa taifa, pia hutolewa kwa watu wazima ambao hawajawahi kupata chanjo.

Chanjo hutolewa kwa njia ya sindano, ambapo huwa ni sindano 3; sindano ya kwanza hutolewa baada ya kupimwa kujua kama hauna maambukizi tayari, sindano ya pili hutolewa baada ya mwezi mmoja na sindano ya 3 baada ya miezi 6.

Makundi ambayo ni lazima kupatiwa chanjo ya homa ya ini pamoja na;

1) Watoto.

2) Watu wote wanaotumia dawa za kulevya na kujifungua.

3) Watu wote wanaoishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi.

4) Watu wote ndani ya familia wanaoshi na ndugu aliyeambukizwa virusi vya homa ya ini.

5) Watu wote wanaotumia dawa za kufubaza kinga ya mwili (immunosuppressive therapy).

6) Wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume wenzao.

7) Watu wote wanaofanya biashara ya ngono.

8) Watu wote ambao wana mpenzi zaidi ya mmoja ndani ya miezi 6.

9) Watu wenye maradhi ya kudumu ya ini.

10) Watu wengine wote wanahitaji kujikinga dhidi ya virusi vya homa ya ini.

Kumbuka: Chanjo hii kama zilivyo chanjo nyingine unapopatiwa  (chomwa) kuna maumivu kidogo sehemu unayochomwa yanayoisha kwa muda mfupi sana na haina madhara yeyote.

Usalama Wa Chanjo.

Chanjo hii ni salama baada ya kudhitishwa na shirika la Afya ulimwenguni (WHO) na mamlaka  mbalimbali za udhibiti wa dawa Nchini.

Kwa Nini Ni Muhimu Kupima Ili Kujua Kama Una Maambukizi Ya Virusi Vya Homa Ya Ini?

Watu wengi huishi na maambukizi ya virusi vya homa ya ini bila kufahamu. Kwa kawaida katika kipindi fulani cha maisha mtu 1 kati ya watu 3 huambukizwa virusi vya homa ya ini. Baada ya kuambukizwa, kuna kundi la watu hubaki na maambukizi ya kudumu ya virusi vya homa ya ini ambayo huwa hayana dalili yoyote na kuendelea kuua ini kimyakimya. Dalili huja kuonekana waziwazi miaka mingi baada ya mtu kuambukizwa. Huonekana wakati tayari ini limenyauka au lina kansa.

Hivyo mtu aliye na maambukizi ya kudumu ya virusi vya homa ya ini aina B akianza matibabu mapema, anaweza kuzuia ini lake lisiharibike sana. Pia kwa wenye maambukizi ya virusi aina C matibabu ya dawa kwa wiki 12 humaliza virusi vyote.

Madhara Ya Homa Ya Ini:

Kwa wastani watu 25 kati ya 100 walioambukizwa virusi vya homa ya ini wakiwa watoto na 15 kati ya 100 waliopata maambukizi ya kudumu ya homa ya ini baada ya utoto hufariki wakiwa na umri mdogo kwa ugonjwa wa ini, ini kushindwa kufanya kazi (liver failure) au saratani ya ini (hepatoma).

hepatoma

Jinsi Ya Kujikinga Na Homa Ya Ini:

Njia bora ya kujikinga na maambukizi ya homa ya ini ni kuhakikisha unapata chanjo ya homa ya ini kwa utaratibu unaotolewa na mtaalamu wa afya katika hospitali au kituo cha afya kilichokaribu nawe.

HITIMISHO:

Kwa msaada wa ushauri, vipimo na tiba ya magonjwa ya afya ya uzazi wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487.

  

vipimo