Fangasi Kwa Mwanaume.

Fangasi kwa mwanaume inahusu maambukizi ya fangasi kwenye mwili wa mwanaume, ambayo yanaweza kutokea sehemu mbalimbali, lakini mara nyingi huathiri maeneo ya ngozi yenye unyevunyevu kama vile sehemu za siri, mapaja ya ndani, na kwapa.

fangasi sehemu za siri
fangasi kwenye uume

Aina ya fangasi inayojulikana zaidi kwa kuathiri wanaume ni candida albicans, fangasi hawa mara nyingi huishi kwenye ngozi na mwili wa binadamu bila kusababisha madhara (normal flora), lakini wakati mwingine wanaweza kuongezeka zaidi (overgrowth) kutokana na sababu mbalimbali mfano hali za kiafya zitokanazo na kushuka kwa kinga ya mwili kama vile VVU/UKIMWI, kansa, kisukari kisichodhibitiwa na kusababisha maambukizi yajulikanayo kama candidiasis.

candida albicans

Sababu Za Fangasi Kwa Mwanaume:

Sababu za fangasi kwa mwanaume zinaweza kujumuisha:

1) Kutumia antibiotics kwa muda mrefu, ambazo huua bakteria wazuri (normal flora) wanaosaidia kuzuia ukuaji wa fangasi.

2) Kiwango kikubwa cha unyevunyevu au jasho sehemu za siri.

3) Kutozingatia usafi binafsi.

4) Ugonjwa wa kisukari kisichodhibitiwa (uncontrolled diabetes).

5) Mfumo dhaifu wa kinga ya mwili kutokana na VVU/UKIMWI, kansa.

6) Kuvaa nguo za ndani (boksa) zinazobana sana au zilizotengenezwa kwa nyuzi ambazo huzuia hewa kupita.

7) Chemotherapy.

Dalili Za Fangasi Kwa Mwanaume:

Dalili za fangasi kwa mwanaume zinaweza kujumuisha:

1) Maumivu au kuwasha kwenye uume, haswa kwenye govi au kichwa cha uume.

2) Ngozi kuwa na madoa mekundu au kubadilika rangi, haswa kwenye sehemu za siri au mapaja ya ndani.

3) Kutoa ute au usaha kutoka kwenye uume au ngozi iliyoathirika.

4) Harufu mbaya au kujikuna mara kwa mara kwenye eneo lililoathirika.

5) Kujisikia muwasho mkali au maumivu wakati wa kukojoa au kujamiana.

Matibabu Ya Fangasi Kwa Mwanaume:

Matibabu ya fangasi kwa mwanaume mara nyingi yanahusisha matumizi ya dawa za kupaka (antifungal creams) kama vile clotrimazole au miconazole, na wakati mwingine dawa za kumeza kama fluconazole iwapo maambukizi ni makubwa.

Soma pia hii makala: Dawa Ya Fangasi Sehemu Za Siri Kwa Mwanaume.

HITIMISHO:

Ikiwa unahisi dalili za fangasi, ni vizuri kumuona daktari kwa ajili ya uchunguzi sahihi na matibabu yanayofaa.