Kuwashwa sehemu za siri kwa wanawake ni miongoni mwa changamoto za kiafya zinazowasumbua wanawake wengi bila kujali rika lao.
Tatizo la kuwashwa sehemu za siri kwa wanawake ni kubwa na hupelekea mwanamke kupata matatizo ya kisaikolojia kwa kuwa mara nyingi inakuwa vigumu wakati mwingine kusema kwa daktari kwamba nina tatizo sehemu zangu za siri.
Leo katika makala yetu tutazungumzia sababu zinazopelekea mwanamke kuwashwa sehemu za siri.
Sababu Zinazopelekea Mwanamke Kuwashwa Sehemu Za Siri:
Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazopelekea mwanamke kuwashwa sehemu za siri ambazo ni pamoja na;
1) Maambukizi Ya Fangasi Ukeni.
Maambukizi ya fangasi ukeni hujulikana kwa kitaalamu kama yeast infection. Maambukizi haya ni moja ya tatizo kwa wanawake linalosababishwa na fangasi waitwao candida albicans.
Dalili kuu za maambukizi haya ni pamoja na kuwashwa ukeni, kuvimba na kutoa uchafu mweupe kama maziwa ukeni.
Soma pia hii makala: Fangasi Ukeni Kwa Mjamzito: Kisababishi, Dalili, Matibabu, Madhara Na Jinsi Ya Kujikinga.
2) Ugonjwa Wa Kuvimba Uke.
Ugonjwa wa kuvimba uke hujulikana kwa kitaalamu kama vulvovaginitis.
Huu ni ugonjwa unaoathiri kwa kuvimbisha sehemu za nje za uke na uke wenyewe.
Dalili kuu za ugonjwa huu ni pamoja na kuwashwa ukeni, mkojo kuuma na kukereketa wakati wa kukojoa na kutokwa na uchafu ukeni.
3) Kuvimba Uke Baada Ya Hedhi Kukoma.
Kuvimba uke baada ya hedhi kukoma hujulikana kwa kitaalamu kama Postmenopausal Atrophic Vaginitis.
Huu ni ugonjwa wa kuvimba uke baada ya hedhi kukoma, hali hii huongeza maambukizi ukeni na huweza kusababisha muwasho ukeni na maumivu wakati wa tendo la ndoa.
4) Maambukizi Ya Trikomonasi (Trichomoniasis).
Maambukizi ya Trikomonasi (Trichomoniasis) ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na kimelea aitwaye Trichomonas vaginalis. Dalili kuu za ugonjwa huu ni pamoja na muwasho ukeni na kutokwa na uchafu ukeni.
5) Ugonjwa Wa Minyoo.
Ugonjwa wa minyoo hujulikanao kwa kitaalamu kama pinworm infection ni maambukizi ya minyoo wadogo sana wenye umbo la pini wanaoweza kuambukiza utumbo na kusambaa maeneo mbalimbali. Ugonjwa huu huwatokea sana watoto wa kati ya miaka 5 na 10.
6) Genital Warts.
Hivi ni vinyama vidogo vinavyoota kwenye ngozi au utando laini unaozunguka maeneo ya sehemu za siri.
Ugonjwa huu uenezwa kwa njia ya kujamiana na unasababishwa na virusi viitwavyo Human Papilloma Virus (HPV). Vinyama hivi vidogo vinavyoota kwenye ngozi au utando laini unaozunguka maeneo ya sehemu za siri vinaweza sababisha muwasho na maumivu.
7) Saratani Ya Sehemu Ya Nje Ya Uke.
Saratani ya sehemu ya nje ya uke ijulikanayo kwa kitaalamu kama vulvar cancer ni saratani ya sehemu ya nje ya uke inayo ambatana na kuwashwa sehemu ya nje ya uke.
8) Kisukari.
Huu ni ugonjwa sugu wa kimetaboliki unaosababishwa na kasoro katika utengenezaji wa Insulin au utendaji kazi wake. Kisukari kilichokomaa kinaweza sababisha maumivu ya tumbo, kichefuchefu, kizunguzungu na kuwashwa sehemu za siri.
9) Urethritis.
Haya ni maambukizi kwenye urethra (mrija wa kutolea mkojo nje ya mwili). Maambukizi haya yanasababisha kuvimba kwa urethra. Dalili kuu za maambukizi haya ni pamoja na mkojo kuchoma, maumivu ya tumbo chini ya kitovu, kutokwa uchafu na kuwashwa sehemu za siri.
Kumbuka:
Magonjwa yaliyoandikwa hapo juu ni baadhi ya visababishi vya muwasho sehemu za siri kwa mwanamke. Magonjwa mengine yanayoweza kusababisha muwasho ukeni ni pamoja na kisonono, kaswende, genital herpes, magonjwa ya ngozi kwenye mashavu ya uke mfano pumu ya ngozi
Mbali na magonjwa visababishi vingine vinavyoweza kusababishwa muwasho ukeni ni pamoja na mzio (allergy), uchafu binafsi (poor personal hygiene) au manukato mbalimbali mfano manukato Ya kutia ndani ya uke.
Jinsi Ya Kutambua Kisababishi Cha Muwasho Sehemu Za Siri Kwa Mwanamke:
Ili uweze kutambua kisababishi cha muwasho ukeni, unatakiwa kufahamu vizuri kuhusu sifa za ya magonjwa yaliyoandikwa hapo juu haswa dalili zake na mwonekano wake na wakati mwingine unahitaji kuthibitisha kwa vipimo. Daktari wako anaweza kutambua kwa kuchukua historia yako na kufanya uchunguzi wa awali ukeni au kuagiza vipimo kufanyika.
Matibabu Ya Kuwashwa Sehemu Za Siri Kwa Mwanamke:
Endapo una muwasho ukeni, wasiliana na daktari wako kwa uchunguzi na tiba kabla ya kutumia dawa yoyote.
Kwa sababu kuna visababishi vingi vya miwasho ukeni, baada ya daktari wako kuchukua historia ya tatizo lako na kukufanyia vipimo atakupa tiba kutokana na kisababishi. Dawa utakazopewa zinaweza kuwa za kupunguza dalili ya muwasho na dawa za kutibu maambukizi ukeni au dawa za kutibu maambukizi tu.
Dawa zifuatazo huficha muwasho ukeni lakini kamwe hazitibu kisababishi;
- Hydrocortisone cream
- Diphenhydramine
- Benzocaine
- Ciclosporin
- Triamcinolone
- Doxepin
- Fluoxetine
- Sertraline
Endapo maambukizi ya fangasi ndio kisababishi cha muwasho ukeni, dawa za antifango zitatumika. Zinaweza kuwa kati ya;
- Terbinafine
- Butenafine
- Clotrimazole cream
- Miconazole
- Ketoconazole
- Econazole
- Luliconazole
- Naftifine
- Oxiconazole
- Tolnaftate
- Ciclopirox
- Itraconazole
- Sulconazole
- Griseofulvin
Kumbuka:
Dawa hizo zinaweza kuwa za kupaka, kunywa au kidonge cha kuweka ukeni, utashauriwa na daktari ni dawa gani itakufaa kulingana na umri wako, hali ya ujauzito na ukubwa wa tatizo.
Jinsi Ya Kujikinga Na Tatizo La Kuwashwa Sehemu Za Siri Kwa Mwanamke:
Mwanamke anapaswa kufanya mambo yafuatayo ili kujikinga na tatizo la kuwashwa sehemu za siri ambayo ni pamoja na;
1) Baada ya kukojoa au kujisaidia osha sehemu zako za siri kuanzia mbele (ukeni) kwenda nyuma (makalio) ili kuzuia bakteria kutoka njia ya haja kubwani kuingia ukeni.
2) Epuka matumizi ya vitu vyenye kemikali kama marashi ya uke katika kusafisha uke kwa maana uharibu hali ya asidi ya uke na kuua bakteria wanaolinda uke na kufanya iwe rahisi kushambuliwa na maradhi sehemu za siri.
3) Weka sehemu zako za siri katika usafi na ukavu, tumia sabuni kidogo katika kusafisha sehemu zako za siri na maji mengi. Kausha sehemu zako za siri kila baada ya kuoga au kuogelea na epuka kukaa na nguo mbichi kwa muda mrefu.
4) Vaa nguo isiyobana sana, iliyotengenezwa kwa pamba ili unyevunyevu usitokee na badili nguo za ndani (chupi) kila baada ya masaa 24.
5) Epuka ngono bila kuvaa mpira (kondomu) hasa ukiwa na hofu na mpenzi kuwa ana maradhi.
HITIMISHO:
Kwa msaada wa ushauri, vipimo na tiba ya magonjwa ya afya ya uzazi kwa wanaume na wanawake wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487.
Je Unasumbuliwa Na PID, Fangasi Sugu Au UTI Sugu Kwa Muda Mrefu Bila Kupata Suluhisho La Uhakika?
Kiasi ambacho umeshajikatia tamaa na huelewi ufanye nini ili kutatua changamoto yako inayokunyima usingizi?
Kama jibu ni NDIYO, basi usiwe na wasiwasi kwani nimekuletea suluhisho la changamoto yako…
Huhitaji kuendelea kutumia dawa za mahospitali ambazo umekuwa ukitumia kwa muda mrefu bila kupona…
Suluhisho halisi kwa changamoto yako aidha ni PID, FANGASI SUGU au Uti sugu utalipata kupitia kitabu (soft copy) kitakachokupa muongozo wa kujitibia changamoto yako uwapo mazingira ya nyumbani kwako…
Gharama ya kitabu hicho mara zote ni TZS 10,000/= ila kwa kuwa leo hii ni sherehe ya kumbukizi ya siku yangu ya kuzaliwa (birthday) nitakupatia kwa bei ya OFA ya TZS 3000/= tu (okoa 7,000/= nzima)…
Ili Kupata OFA hiyo Lipia kwenda Tigo Pesa namba 0653211873 (Isaya Febu Msemwa) Kisha nitumie muamala wako WhatsAPP Kwa kubonyeza hapa: https://wa.me/+255625305487
PS: Ofa hii itaisha kesho saa 6:00 mchana, weka oda yako mapema Kwani ukiikosa leo, kuipata tena mpaka mwakani tarehe kama ya leo.
Mbona Mimi nimepata fangas nikatumia dawa na ikarud Tena na uke unatoa uchf mwingi San nikaambiea ni kichelew kupata matibabu inakua pid na nimepatiwa doz ya sindano na dawa za kunywa na kuweka ukeni
Kwa msaada wa dawa asilia ya kutibu fangasi ukeni na pid wasiliana nasi 0625305487
Mm nawashwa sana sehem za sir siku hiz 2 wala skuwahi kufanya tendo la ndoa imenitokea nawashwa sana na matoka maji maji yanayonifanya niwe na msongo ss sjui sababu choo mana nimeenda sehem kutembea
Nenda hospitali iliyokaribu nawe ukafanyiwe check up ili kujua shida ni nini
Nawashwa sehem za Siri kias kwamba napata msongo wa mawazo na pia Nina shida ya kupata mtoto
Tupigie 0625305487 kwa msaada wa tiba
Inshallah Mwenyezi MUNGU akufanyie wepesi Mary update mtoto
Na mimi nawashwa Sana sehemu za Siri nimeenda sipitali kaa tatu Leo ndo nimeona uchafu mwingi sna umemwagikaa ni Nini jamani
H