Tatizo la Kukosa hamu ya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanaume wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu wanaume 4 kati ya 10 wanakabiliwa na tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kuwa na changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume.
Soma pia hizi makala:
Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa msisimko wa tendo la ndoa kwa wanaume, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili.
Kwa kuzingatia hilo, wataalamu wa afya na watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina mbalimbali ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mwanaume nguvu ya kufanya tendo la ndoa.
Vyakula 11 Vinavyoongeza Hamu Ya Tendo La Ndoa Kwa Wanaume:
Vifuatavyo ni vyakula 11 vinavyoongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanaume ambavyo ni pamoja na;
1) Pilipili.
Ndani ya pilipili kuna kompaundi iiwatyo capsaicin ambayo hufanya pilipili iwe na hali ya ukali. Capsaicin huwezesha ubongo kutoa homoni ya endorphins ambayo huleta hisia za raha wakati wa kufanya tendo la ndoa.
Pia pilipili husisimua mfumo wa fahamu (nerves) wa ubongo na katika kufanya hivyo humuwezesha mwanaume kusisimka haraka kimapenzi (kunyegeka) wakati wa tendo la ndoa.
2) Matunda Na Mboga Za Majani.
Ulaji wa matunda na mboga za majani una matokeo makubwa sana katika hamu ya tendo la ndoa kwa njia nyingi. Matunda na mboga za majani hupunguza kiwango cha mafuta (obesity). Kuongezeka kwa mafuta mwilini huzuia mzunguko wa damu kwa kubana mishipa ya damu.
Pia kula matunda na mboga za majani huhakikisha balansi ya uzito kwani unene uliozidi (obesity) kwa wanaume kuna matokeo mabaya katika kuzalisha homoni ya testosterone na hatimaye uume kushindwa kusimama na pia mwanaume anakuwa na hisia za mapenzi kidogo (low libido).
Tafiti zinaonesha kuwa wanandoa wanapozidi kunenepeana ndipo na hali ya kufurahia au kuwa na hamu ya tendo la ndoa huzidi kupungua. Kitalaamu inashauriwa kula milo (potions) 3-5 za matunda kwa siku.
3) Nafaka Zisizokobolewa.
Nafaka hasa zisizokobolewa kama mahindi, ngano, uwele, nk zina nyuzinyuzi (Dietary fibres) na sukari ngumu (Complex sugar) ambazo kusaidia kutunza uzito wa mwili. Nafaka hizo husaidia katika kuzalisha homoni ya testosterone kwenye damu. Pia nafaka hizo humuwezesha mwanaume kuwa na nguvu hatimaye kwenda masafa marefu wakati wa tendo.
Kula nafaka nzima kama vile brown bread badala ya white bread, pia kula nafaka halisi badala ya cornflakes ni jambo zuri linalokuhakikisha afya njema na mahusiano mazuri ya ndoa yako.
4) Tangawizi.
Tangawizi ni kiungo cha mboga ambacho husisimua sana na kusaidia mfumo wa mzunguko wa damu mwilini. Tangawizi zinajulikana sana kwa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi yaani uume hivyo kuwa na umuhimu sana katika kuboresha ufanyaji wa tendo la ndoa. Inaweza kuliwa mbichi, au kuliwa ikiwa imeungwa kwenye chakula au kusagwa na kuwa kama unga na kutumika kwenye chai.
5) Asali.
Baadhi ya vitamini vinavyopatikana kwenye asali ni pamoja na ascorbic acid, pantothenic acid, niacin na riboflavin, madini yanayopatikana kwenye asali ni pamoja na calcium, copper, iron, magnesium, manganese, phosphorus, potassium na zinc. Vitamini na madini hayo husaidia katika uzalishaji wa homoni ya testosterone na mbegu za kiume.
6) Karanga.
Karanga inasaidia kuchochea mfumo wa mzunguko wa damu katika mwili. Ongezeko la mzunguko wa damu kwenye uume humuwezesha mwanaume kupata msisimko wa mapenzi haraka hatimaye tendo la ndoa kuwa murua. Pia karanga zina madini muhimu kama vile magnesium, asidi ya folic na zinc ambayo ni muhimu sana katika uzalishaji wa mbegu za mwanaume.
7. Chaza (Oysters) Na Pweza.
Hawa ni aina ya samaki ambao hupatikana katika maji chumvi. Huwa na kiasi kikubwa sana cha madini ya zinc na haya madini ndiyo huhusika zaidi na uzalishaji wa homoni ya testosterone kwa wanaume.
Pia imethibitika kwamba wanaume wenye ukosefu wa madini ya zinc huwa na matatizo ya nguvu za kiume. Pia madini mengi ya zinc mwilini huongeza kiwango cha shahawa kwa wanaume.
8) Parachichi.
Aina nyingine ya chakula ambacho husaidia kuongeza uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa ni Parachichi. Tunda hili lina uwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa testosterone, homoni ya kiume. Inatajwa kuwa wanaume wanaotumia tunda hili kwa wingi huwa na msisimko mkali wa kimapenzi.
9) Ndizi Mbivu.
Ndizi mbivu zina kiwango kikubwa cha potasiamu ambacho husaidia kuongeza uzalishaji wa testosterone, homoni ya kiume na kuboresha hamu ya tendo la ndoa kwa wanaume.
Tryptophan iliyopo ndani ya ndizi mbivu husaidia kuongeza utengenezaji wa serotonin, homoni inayoboresha hisia na kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanaume.
10) Tende.
Tende ni aphrodisiac ya asili, hivyo kula tende kunaweza kusaidia kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanaume. Tende zina kiwango kikubwa cha madini ya chuma, vitamini c, folate nk.
11) Tikiti Maji.
Tikiti maji lina kiasi kikubwa cha asidi ya amino (L-citrulline) ambayo inachochea mtiririko wa damu kwenye uume. Wanaume wenye tatizo la uume kutosimama na hamu ya chini ya tendo la ndoa (low libido) wanaweza kunufaika kupitia L-citrulline kwa kula tikiti maji.
HITIMISHO:
Vyakula vingine vinavyoweza kuongeza hamu ya tendo la ndoa ni pamoja na kitunguu swaumu, chokoleti nyeusi, soya, mbegu za maboga.
Lakini pia, kwa uhitaji wa updates, vitabu (e-books) bure kuhusu afya jisajili (subscribe) kupitia email yangu kwa kubonyeza hii link: https://isayafebu.beehiiv.com/subscribe
Je Unasumbuliwa Na PID, Fangasi Sugu Au UTI Sugu Kwa Muda Mrefu Bila Kupata Suluhisho La Uhakika?
Kiasi ambacho umeshajikatia tamaa na huelewi ufanye nini ili kutatua changamoto yako inayokunyima usingizi?
Kama jibu ni NDIYO, basi usiwe na wasiwasi kwani nimekuletea suluhisho la changamoto yako…
Huhitaji kuendelea kutumia dawa za mahospitali ambazo umekuwa ukitumia kwa muda mrefu bila kupona…
Suluhisho halisi kwa changamoto yako aidha ni PID, FANGASI SUGU au Uti sugu utalipata kupitia kitabu (soft copy) kitakachokupa muongozo wa kujitibia changamoto yako uwapo mazingira ya nyumbani kwako…
Gharama ya kitabu hicho mara zote ni TZS 10,000/= ila kwa kuwa leo hii ni sherehe ya kumbukizi ya siku yangu ya kuzaliwa (birthday) nitakupatia kwa bei ya OFA ya TZS 3000/= tu (okoa 7,000/= nzima)…
Ili Kupata OFA hiyo Lipia kwenda Tigo Pesa namba 0653211873 (Isaya Febu Msemwa) Kisha nitumie muamala wako WhatsAPP Kwa kubonyeza hapa: https://wa.me/+255625305487
PS: Ofa hii itaisha kesho saa 6:00 mchana, weka oda yako mapema Kwani ukiikosa leo, kuipata tena mpaka mwakani tarehe kama ya leo.
Hongera and thanks for the tip.means alot
karibu sana mkuu.
Hongera sana kwa utafiti huu maana kaa unakuta una Itaji kuendelea lakini uume hautaki
Asante…karibu sana mkuu
Mnapatkana wapi
Sinza madukani, Dar es salaam
Je kuna dawa zake pia au ndo ukizingatia hivyo vyakula umepona?
Dawa zake zipo pia
Dawa gani mkuu inasaidia kama supplement ya hivyo vyakula
garlic na chelated zinc
Barikiwa Mkuu
We thank for your information
Asante kwa Elimu Iringa Mjini mnapatikana wapi
Tunapatikana isakalilo Mgovano (karibu na Gereza)
Hizo aisee za dawa kwa arusha mnapatikana wapi na zinafanya kazi kwa mda gani mkuu
Kwa arusha hatuna tawi, tunapatikana dodoma mjini (majengo sokoni) na DSM. Kwa mawasiliano zaidi piga 0625305487
Kando na kuenda hospitali n vyakula vipi mwanaume anaweza kula ili akuwe na mboro kubwa?
Hakuna
Thanks
mbeya mjin mnapatikana sehemu gani
Hey Mimi mume wangu Ni Hana hata hisia ya kunishika Na kucheza Na mm Na akifanya Basi hawezi kwenda round mbili Na hiyo moja pia Ni ya haraka
Nimejifunza vituvingi saaana ahsante vitaninufaisha
mbeya mjini mnapatikana sehemu gani ? nijuze nahitaji hiyo dawa
Tunapatikana Mbeya mjini, soweto karibu na mkulu hotel