Yajue Mazoezi Ya Kuongeza Nguvu Za Kiume.

Upungufu wa nguvu za kiume ni hali ya mwanaume kushindwa kusimamisha uume kabisa, uume kuwa legevu na kushindwa kuingia ukeni hata ukiwa umesimama pamoja na kutoa shahawa nyepesi au kidogo.

Tatizo la kukosa nguvu za Kiume kwa wanaume limekua tatizo ambalo linakua kila siku na kusababisha matatizo makubwa ndani ya ndoa ikiwemo ndoa kuvunjika na malumbano yasiyoisha ndani ya ndoa. Mara nyingine tunadhani kukosa nguvu za kiume kunasababishwa na kutokula lishe bora kumbe hata kutokufanya mazoezi kunaweza sababisha tatizo hili.

Soma pia hii makala: Zijue Dalili 7 Za Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Tiba Zake.

Tafiti za hivi karibuni zinaonesha kufanya mazoezi kunaweza kupunguza au kumaliza kabisa tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume ingawa kwa baadhi ya wanaume yanaweza yasiwasaidie hasa wenye maradhi ya moyo.

Kwa wanaume wenye shida ya unene kupitiliza pamoja na tatizo la nguvu za kiume, matokeo ya tafiti yanaonesha wakiamua kupunguza uzito na kuongeza mazoezi hupata matokeo chanya kwenye nguvu za kiume kwa kuongeza uwezo wa uume kusimama kwa zaidi ya 1/3 ya kundi hili.

Faida Ya Kufanya Mazoezi Kwa Wanaume:

Mazoezi yanasaidia kusafisha mishipa ya damu na hivyo kuongeza kiasi cha utiririkaji wa damu kwenda kwenye uume, hivyo mwanaume asipofanya mazoezi anaweza kuwa katika hatari ya upungufu wa nguvu za kiume . Mazoezi ni mazuri kwa afya. Mazoezi ya kegel ni moja wapo ya mazoezi yanayosaidia kuongeza nguvu za kiume.

Baadhi ya Video clips zifuatazo hapa chini zinaonesha mazoezi yanayosaidia kuongeza nguvu za kiume kwa haraka.

Kumbuka: Chukua unga wa tangawizi nusu kijiko cha kahawa + limao moja, kamua maji ya limao weka kwenye glass ya maji ya baridi/moto kunywa maji hayo mara moja kwa siku baada ya mazoezi ya kegel.

HITIMISHO:

Ikiwa unashindwa kusimamisha uume, uume unasinyaa haraka, unakosa kabisa hamu ya tendo la ndoa, unawahi kufika kileleni au unachelewa sana kufika kileleni isivyo kawaida unapaswa kutafuta msaada wa kitaalamu haraka. Kwa msaada wa ushauri, vipimo na tiba ya magonjwa ya afya ya uzazi kwa wanaume wasiliana nasi kwa simu namba 0625 304 587.

Lakini pia, kwa uhitaji wa updates, vitabu (e-books) bure kuhusu afya jisajili (subscribe) kupitia email yangu kwa kubonyeza hii link: https://isayafebu.beehiiv.com/subscribe

vipimo vya mfumo wa uzazi kwa wanaume