Yajue Matunda 8 Anayotakiwa Kula Mama Mjamzito.

Mama Mjamzito:

Mwanamke anapokuwa mjamzito anashauriwa  sana kula matunda katika mlo wake wa kila siku. Ulaji wa matunda kwa mama mjamzito una faida nyingi kwa mama mwenyewe pamoja na mtoto aliye tumboni kwa sababu matunda ni chanzo bora cha vitamini, madini na nyuzi nyuzi (dietary fibres).

Wakati wa ujauzito mama anahitaji virutubisho ambavyo hutokana pia na ulaji wa matunda zaidi kwa ajili ya maendeleo yake ya kiafya pamoja na mtoto aliye tumboni. Lishe bora itokanayo na ulaji wa matunda kwa mama mjamzito huimarisha afya ya mama na humsaidia mtoto aliye tumboni kukua vizuri kimwili na kiakili.

mama mjamzito

Leo katika makala yetu tutazungumzia matunda anayotakiwa kula mama mjamzito kwa ajili ya maendeleo yake ya kiafya pamoja na mtoto aliye tumboni.

Matunda Kwa Mama Mjamzito:

Yafuatayo ni baadhi ya matunda anayoshauriwa kula mama mjamzito kwa ajili ya maendeleo yake kiafya pamoja na mtoto aliye tumboni, matunda haya ni pamoja na;

1) Parachichi.

Mama mjamzito anashauriwa kula parachichi kama sehemu ya mlo wake wa kila siku, kwa sababu parachichi ni chanzo kikubwa sana cha mafuta mengi mwilini maarufu kama fatty acids ambayo husaidia katika ukuaji wa ubongo, ngozi, misuli ya mtoto aliye tumboni. Pia ulaji wa parachichi kwa mama mjamzito humsaidia kuepukana na tatizo la kukosa/kupata choo kigumu.

parachichi

Soma pia hii makala: Faida Za Parachichi Kwa Mjamzito.

2) Ndizi Mbivu.

Ndizi mbivu ni chakula kizuri sana wakati wa ujauzito. Ndizi mbivu zina viwango vikubwa vya madini ya kalishiamu na potasiamu ambayo yanamsaidia mama mjamzito kuepukana na changamoto ya kukaza kwa misuli ya miguu. Ikiwa mama mjamzito una hamu ya tunda lenye sukari lililo salama kwako na mtoto aliye tumboni, ndizi mbivu ni chaguo sahihi. Lakini kama una kisukari kilichosababishwa na ubebaji mimba (gestational diabetes), chagua kula ndizi za kupikwa (mbichi).

ndizi mbivu

3) Tikiti Maji.

Tunda hili lina kiwango kikubwa cha maji kuliko tunda linguine lolote-92%. Ikiwa unapambana na tatizo la kukosa maji mwili wakati wa ujauzito, unashauriwa kula tunda hili. Tikiti maji lina madini ya potasiamu, zinki na foliki asidi kwa ajili ya kupambana na misuli ya miguu kukaza hasa wakati wa usiku na kusaidia ukuaji wa uti wa mgongo wa mtoto tumboni.

tikiti maji

4) Machungwa.

Chungwa linaweza kuwa tamu au chachu, ladha hizi zina pendwa na wanawake wengi ambao wanasubuliwa na kichefuchefu wakati wa ujauzito. Machungwa yana kiwango kikubwa cha maji, ni chanzo kizuri sana cha vitamini C. Vitamini hii inachangia kukuza kinga ya mwili kwa mama mjamzito na mtoto aliye tumboni, na pia inasaidia kujenga tishu muhimu kwa ajili ya ukuaji wa kimwili wa mtoto aliye tumboni.

machungwa

Soma pia hii makala: Faida Za Machungwa Kwa Mjamzito.

5) Embe.

Mama mjamzito anashauriwa pia kula embe kwani embe ni chanzo kizuri sana cha vitamini C. Vitamini C husaidia kuongeza kinga ya mwili kwa mama mjamzito na mtoto aliye tumboni.

embe

6) Tufaha (Apple).

Mama mjamzito anashauriwa pia kula tufaha au apple katika mlo wake wa kila siku. Matunda haya yana vitamini A na C, maji ya kutosha na nyuzi nyuzi (dietary fibers) ambazo humsaidia mama mjamzito kuepukana na tatizo la kukosa/ kupata choo kigumu.

apple

7) Peasi.

Peasi ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi zinazosaidia kupambana na tatizo la kukosa choo. Peasi pia ni chanzo kizuri cha vitamini C, pamoja na madini chuma, magnesiamu na foliki asidi. Ulaji wa tunda hili kwa mama mjamzito husaidia kuboresha afya mama mwenyewe na mtoto aliye tumboni.

peasi

8) Komamanga.

Komamanga lina kiwango kikubwa cha kirutubisho kiitwacho polyphenol. Tafiti pia zimeonesha kuwa ulaji wa komamanga wakati wa ujauzito unasaidia katika kuongeza kinga ya mwili kwa mtoto aliye tumboni. 

komamanga

Faida Za Kula Matunda Wakati Wa Ujauzito:

Zifuatazo ni baadhi ya faida za kula matunda wakati wa ujauzito ambazo ni pamoja na;

1) Matunda Huongeza Virutubisho Muhimu Katika Mwili.

Mtoto wako anahitaji virutubisho fulani ili kukua vizuri. Virutubisho vinavyotolewa na matunda ni pamoja na vitamini C na foliki asidi. Vitamini C ni muhimu kujenga tishu, inasaidia kukuza kinga ya mwili ya mtoto na kuruhusu uhifadhi wa madini chuma yanayotumika kuzuia anemia. Foliki asidi inasaidia kujenga uti wa mgongo na pia kumkinga mtoto anayekua dhidi ya kasoro katika neva za fahamu na hivyo kuepusha dosari katika ubongo, mgongo na uti wa mgongo (neural tube defects).

2) Matunda Yanasaidia Kukidhi Hamu Ya Vyakula Vitamu.

Utofauti mmojawapo wa matunda ni kuwa matamu au machachu, ladha zote hizi ni pendwa kwa wajawazito. Kuchagua tunda badala ya peremende au biskuti humsaidia mama mjamzito kumaliza hamu katika njia ya kuridhisha na salama kwa afya.

3) Matunda Yanasaidia Kudhibiti Sukari Katika Damu.

Matunda yana nyuzinyuzi (dietary fibers) zinazosaidia kuratibu ufyonzaji wa sukari katika mfumo wa damu.

4) Matunda Yanasaidia Kuongeza Maji Mwilini.

Unahitaji kunywa maji ya kutosha ukiwa mjamzito. Tunda lina zaidi ya asilimia 80 ya maji, hivyo ikiwa umechoka kunywa maji kila saa unaweza kuchagua kula matunda kuhakikisha mwili wako unakaa na maji.

5) Matunda Yanasaidia Kukabiliana Na Tatizo La Kukosa Choo.

Ukiwa mjamzito, umeng’enyaji wa chakula unakua polepole, hali hii inaweza sababisha kukosa choo- lalamiko la kawaida kipindi cha ujauzito. Ikiwa unatumia virutubisho vyenye madini ya chuma yanaweza kusababisha kukosa choo. Tatizo kubwa la kukosa choo linaweza kusababisha “hemorrhoids”. Njia nzuri ya kuondokana na tatizo la kukosa choo ni ulaji wa vyakula ambavyo ni vyanzo vizuri vya nyuzi nyuzi na kunywa maji (matunda yana vyote viwili-maji na nyuzi nyuzi).

6) Matunda Husaidia Kuzuia Kichefuchefu.

Ikiwa mwanamke anapata changamoto ya kichefuchefu wakati wa ujauzito, ni ngumu kuweka chakula tumboni kwa muda mrefu. Vyakula vitamu na baridi ni vizuri ikiwa mwanamke mjamzito ana pambana na magonjwa ya asubuhi, mama mjamzito anashauriwa kutunza matunda ya kutosha kwenye friji kwa ajili ya kifungua kinywa.

Soma pia hii makala: Mama Mjamzito: Vijue Vyakula Anavyopaswa Kula Na Vyakula Hatarishi Kwa Afya Yake Na Mtoto Aliye tumboni.

HITIMISHO:

Kiasi Gani Cha Matunda Nile Nikiwa Mjamzito?

Ingawa ulaji wa matunda ni afya, lakini ikumbukwe matunda ni chanzo cha sukari, ambayo inatakiwa kuwekwa kikomo ukiwa mjamzito. Inashauriwa mjamzito kula matunda mara 2-4 kwa siku.

Kwa msaada wa ushauri, vipimo na tiba ya magonjwa ya afya ya uzazi kwa wanaume na wanawake wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487.