Baada ya tendo la ndoa, njia bora ya kusafisha uke ni kutumia maji safi ya vuguvugu (running water) kusafisha sehemu za nje za uke kwa uangalifu.


Epuka kutumia sabuni au kemikali kali ndani ya uke kwani sehemu ya ndani ya uke huwa na uwezo wa kujisafisha yenyewe kwa asili (vagina is self cleansing).
Muhimu ni kujisafisha ukeni kutoka mbele kwenda nyuma (front to back) ili kuzuia bakteria kama vile escherichia coli (E.coli) kutoka sehemu ya haja kubwa kuingia kwenye uke na kusababisha maambukizi kama vile uti kwa wanawake.
Baada ya kujisafisha ukeni, jikaushe sehemu hiyo vizuri kwa kutumia taulo laini na kavu ili kuzuia unyevu unaodumu ambao unaweza kusababisha maambukizi zaidi kama vile fangasi ukeni. Pia, kuvaa nguo za ndani (chupi) zenye pamba husaidia kupunguza unyevu na kuzuia ukuaji wa fangasi.
Zaidi ya hayo, ni vizuri kwenda haja ndogo baada ya tendo la ndoa kwani husaidia kusafisha njia ya mkojo na kuzuia bakteria kusababisha maambukizi ya njia ya mkojo.

Vidokezo Muhimu Vya Kuzingatia:
- Usitumie douches au sabuni zenye marashi au kemikali kali kujisafisha ndani ya uke.
- Usijisafishe ukeni kupita kiasi kwani kunaweza kusababisha mabadiliko ya pH ya uke.
- Fanya usafi wa sehemu za nje za uke tu kwa maji mara moja au mara mbili kwa siku au baada ya tendo la ndoa.
HITIMISHO:
Kwa ujumla, njia hii ni salama na inasaidia kuzuia maambukizi ukeni na matatizo ya afya ya uke. Ikiwa kuna dalili zisizo za kawaida kama kuwashwa, maumivu, au kutokwa na uchafu usio wa kawaida ukeni, wasiliana nasi kwa simu namba 0625 305 487 kwa msaada wa ushauri na tiba ya uhakika.
Leave a Reply