Kaswende Ni Ugonjwa Gani?

Kaswende:

Kaswende ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na bakteria anayeitwa Treponema pallidum.

Kaswende

Ugonjwa huu pia hujulikana kwa kitaalamu kama Syphilis.

Ugonjwa huu huenea kwa njia ya kujamiiana na unaweza pia kuambukizwa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa ujauzito, hali inayojulikana kama kaswende ya kuzaliwa (congenital syphilis).

Dalili Za Kaswende:

Kaswende ina hatua kuu nne ambazo ni pamoja na:

1) Hatua Ya Kwanza (Primary Stage).

Dalili ya mwanzo ni kidonda kinachoitwa “chancres” ambacho hujitokeza kwenye sehemu za siri, mdomo, au sehemu nyingine za mwili baada ya siku 10 hadi 90 ya kuambukizwa. Kidonda hiki huwa hakina maumivu.

2) Hatua Ya Pili (Secondary Stage).

Ikiwa haitatibiwa, mgonjwa anaweza kupata vipele mwilini, homa, uchovu, maumivu ya viungo, na uvimbe wa tezi. Dalili hizi zinaweza kutoweka zenyewe, lakini ugonjwa bado unakua mwilini.

3) Hatua Ya Siri (Latent Stage).

Katika hatua hii, ugonjwa unaweza kutokuonyesha dalili yoyote, lakini bakteria bado wapo mwilini. Hatua hii inaweza kudumu kwa miaka kadhaa.

4) Hatua Ya Mwisho (Tertiary Stage).

Bila matibabu, kaswende inaweza kusababisha matatizo makubwa kama magonjwa ya moyo, mishipa ya damu, uharibifu wa ubongo, na hata kifo.

Dawa Ya Kaswende Ni Ipi?

Kaswende inatibika kwa kutumia dawa za antibiotiki, hasa penicillin (benzathine penicillin), ikiwa itatambuliwa mapema. Ni muhimu kutumia kinga wakati wa kujamiiana na pia kupimwa mara kwa mara kama hatua ya kuzuia maambukizi.

benzathine penicillin

HITIMISHO:

Je, ungependa kujua zaidi kuhusu madhara ya kaswende?

Kama jibu ni NDIYO, Soma hapa: Mambo Muhimu Usiyo yajua Kuhusu Ugonjwa Wa Kaswende.